Mamlaka za Uteuzi wa Viongozi zinadhihirisha wazi kuna tatizo kwenye utaratibu wa "Vetting"

Kwenye suala la tumpe muda hapo mkuu natofautiana na wewe, Nchi haiongozwi kama Familia, ndio maana kuna OBR pale washauri kibao wanamwacha afanye makosa hadharani?
Anachofanya ni kwa mujibu wa katiba, rais hapaswi kutoa sababu zozote za uteuzi au utenguzi wa nafasi yoyote. Kwa vile katiba ni yetu, sisi tukiamua tunataka rais wetu awe anatoa sababu za uteuzi na utenguzi, tunampangia. Should We Demand More Right to Information Kwenye Teuzi za Key Posts? Ziwe Endorsed na Bunge With Security of Tenure? Mawaziri Wasiwe Wabunge?

Hilo la vetting, ni kweli kuna tatizo, ila kwa vile vetting hafanyi yeye, then nimeshauri Rais Samia, sio malaika ni binadamu anaweza kukosea. Tusimlaumu, kumshutumu na kumponda kwa makosa ya kukoseshwa. Tumvumilie tumpe muda
P
 
Kwa muda wa miaka 3 ya utawala wa Rais Samia, kumekuwa na Teuzi na Tenguzi au kubadilishwa kwa nafasi za Kiutawala kwa wanaoteuliwa na wakati mwingine bila hata kuelezwa sababu.

Samia amekuwa akiteua na kutengua au kuwarejesha watu walioondolewa kazini kwa sababu mbalimbali. Na wapo ambao ameendelea kuwakumbatia licha ya kuwa na kashfa mbaya kiuongozi.

Baadhi ya Viongozi hao ni pamoja na Makonda, Chalamila, Biswalo Mganga, Kingai na wengine wengi.

Hapa tu inaonesha aidha kuna shida katika idara ya Usalama wa Taifa eneo la Mahusiano kwa Umma au Rais anapuuza makandokando yaliyopo nyuma ya anaowateua kwa maslahi yake binafsi.
Tatizo ni connection na networking huku weledi,uadilifu ukiachwa kando kwa sababu ama za kimaslahi,kiitikadi ama ukabila ama uswahiba🤔
 
Mkuu OKW BOBAN SUNZU, naunga mkono hoja, tungekuwa na good, real and true intelligentsia, baada ya bandiko kama hili Elections 2015 - Mgombea wa Urais Kwa tiketi ya CCM, 2015 "Could Be" John Pombe Magufuli watu wangefanya their homework well, with tharaly background check, they would have known the truth!, but wale jamaa zetu, yale ni manunga embe!, good for nothing!.

Na ili kuzuia such mistakes zisijirudie, nimeshauri let's employ modern technology of DNA Ili kuepuka possibility ya kutawaliwa na wageni, kuna haja kutumia DNA kuthibitisha asili halisi za viongozi wetu wakuu? ili makosa yale yasijirudie!.
Biteko, Bashungwa needs to be screened tharaly!.
P
Kaka Pascal hoja yako ni nzito sana, inamaana Nzilankende alikuwa siyo Mtanzania plus hao uliowataja?

Sent from my V2111 using JamiiForums mobile app
 
Hata uwe na CV iliyoshiba pages 1000 lakini kama hauna connection sahau teuzi Mkuu.

Nape aliteuliwa Waziri akiwa hana hata Shahada ndiyo amepata kama sio mwaka jana basi mwaka juzi.

Kwahiyo hakuna Vetting inafanyika zaidi ya Connection tu
Na matokeo ya haya ni kuongozwa na ma-zuzu.
 
Kwa muda wa miaka 3 ya utawala wa Rais Samia, kumekuwa na Teuzi na Tenguzi au kubadilishwa kwa nafasi za Kiutawala kwa wanaoteuliwa na wakati mwingine bila hata kuelezwa sababu.

Samia amekuwa akiteua na kutengua au kuwarejesha watu walioondolewa kazini kwa sababu mbalimbali. Na wapo ambao ameendelea kuwakumbatia licha ya kuwa na kashfa mbaya kiuongozi.

Baadhi ya Viongozi hao ni pamoja na Makonda, Chalamila, Biswalo Mganga, Kingai na wengine wengi.

Hapa tu inaonesha aidha kuna shida katika idara ya Usalama wa Taifa eneo la Mahusiano kwa Umma au Rais anapuuza makandokando yaliyopo nyuma ya anaowateua kwa maslahi yake binafsi.
Kuna tatizo kubwa, kama tungekuwa serious na vetting hata huyu SSH asingepewa umakamu wa Rais in the first place, kikitokea cha kutokea anakuwa Rais. Pale angekuwa labda majaliwa.

Level yake ilibidi iishie kama naibu waziri wa kina mama, watoto na jinsia au kwenye NGO moja ya kuomba misaada na kuandaa makongamo, warsha, semina na kusafiri safiri duniani.
 
Tatizo siyo vetting
Tatizo ni teuzi za kufafijiana.

Baada ya kufariki yule simba wa yuda, mama aliamuakuwarejesha wale waliotemwana mfumo.

Ameanza kuona matokeo yake ndo anakumbuka shuka kumekucha.

Tatizo ni yeye SSH. Hata vetting ikiwa vizuri sijui kama anatiliab ushauri maanani.

Yeye anchagua na kutengua jinsi anavyojisikia na inategemea anaamkaje, au madhara yakishakuwa makubwa sana kama issue ya umeme, wizara ya nishati au issue ya DP world ndio anafanya maamuzi.
 
Hata uwe na CV iliyoshiba pages 1000 lakini kama hauna connection sahau teuzi Mkuu.

Nape aliteuliwa Waziri akiwa hana hata Shahada ndiyo amepata kama sio mwaka jana basi mwaka juzi.

Kwahiyo hakuna Vetting inafanyika zaidi ya Connection tu
Uko sahihi sana, maana hata hata hao wafanya vetting wanapatikana kwa connections!
 
Tatizo ni yeye SSH. Hata vetting ikiwa vizuri sijui kama anatiliab ushauri maanani.

Yeye anchagua na kutengua jinsi anavyojisikia na inategemea anaamkaje, au madhara yakishakuwa makubwa sana kama issue ya umeme, wizara ya nishati au issue ya DP world ndio anafanya maamuzi.
Kile kijitabu kiitachwo katiba kinampa rais ruhusa ya kufuata ushauri au kutupilia mbali. Je unajua hao wafanya vetting wanapatikana vipi? Tatizo ni kubwa kuliko unavyofikiri.
 
Back
Top Bottom