Mamlaka ya Ngorongoro kuna tatizo kubwa sana

Upekuzi101

Senior Member
Aug 28, 2020
134
348
Huwezi amini hili eneo linapokea na kulaza wageni zaidi ya 100 kila siku. Ngorongoro Simba camping site huu mlango una zaidi ya miezi mitatu bila kufanyiwa matengenezo baada ya kuharibiwa na tembo ila tangu uharibike haujawai kutengenezwa na wala hakuna kiongozi anayeona hili ni tatizo.

Pia Kuna suala hili la Choo. choo kimoja kinafanyiwa ukarabati Toka waanze huo ukarabati hadi sasa ni miezi miwili na bado kimefungwa kwa madai bado ukarabati unaendelea. Kiukweli kila mgeni analalamika kwani vyumba vya choo vinavyotumika ni viwili tu kwa wanaume na wanawake na Leo hapa Kuna wageni zaidi ya 120 hili ni tatizo kubwa mno kiukweli.

Mheshimiwa Mchengerwa angalia sana mamlaka ya Ngorongoro, watu wameshazoea kazi na madaraka kwaiyo hawana tena msukumo wa kazi so tafuta vijana wanaojitambua uwape kazi hapo Ngorongoro, hii ni aibu kubwa kwa wizara ya Mali Asili na utalii Tanzania.

IMG-20230216-WA0021.jpg
 
Ngorongoro ni chaka la ubadhilifu!
Tangu serikali ilipowahamishia hazina kuu!
Wamekuwa na tabia ya kuacha ili uharibifu uwe mkubwa,kisha waweze kuomba fungu toka serikali kuu.
 
Hizo Ni strategy za kuwavutia wazungu,maana kwao wameacha milango ya kutumia lift,ku-swap card milango ifunguke,vyoo vya kukalia.

Sasa wanaonyeshwa culture halisi ya kiafrica, wana-enjoy Sana mkuu.Tena ningeshauri hata chooni maji/toilet paper zisiwepo Ila yawepo Yale majani ya kujifutia baada ya kumaliza kunyer,watu wa bush wanayajua vzr majani hayo.
 
Huwezi amini hili eneo linapokea na kulaza wageni zaidi ya 100 kila siku. Ngoro ngoro Simba camping site huu mlango una zaidi ya miezi mitatu bila kufanyiwa matengenezo baada ya kuharibiwa na tembo ila tangu uharibike haujawai kutengenezwa na wala hakuna kiongozi anayeona hili ni tatizo.

Pia Kuna swala hili la Choo. choo kimoja kinafanyiwa ukarabati Toka waanze huo ukarabati hadi sasa ni miezi miwili na bado kimefungwa kwa madai bado ukarabati unaendelea kiukweli kila mgeni analalamika kwani vyumba vya choo vinavyotumika ni viwili tu kwa wanaume na wanawake na Leo hapa Kuna wageni zaidi ya 120 hili ni tatizo kubwa mno kiukweli.

Mheshimiwa Mchengerwa angalia sana mamlaka ya Ngorongoro, watu wameshazoea kazi na madaraka kwaiyo hawana tena msukumo wa kazi so tafuta vijana wanaojitambua uwape kazi hapo Ngorongoro, hii ni aibu kubwa kwa wizara ya Mali Asili na utalii Tanzania.

View attachment 2519998
Tembo hakuwaelewa kwanini wao wanaowaletea hela walale nje kwenye mbu na baridi huku nyie mnalala ndani huku mkinywa whisky na wine.
 
Watu wasio wabunifu na makini ndio wamepewa kazi nyeti ya kulinda na kuboresha maliasili zetu.
 
Mnawaweka hao wageni kwenye hatari kubwa ya kuvamiwa na wanyama wakali........tusishangae huko mbeleni ukaanzishwa uzi mpya baada ya huu.
 
Back
Top Bottom