Mamlaka husika hebu lioneni hili

NI MTAZAMO TU

JF-Expert Member
Feb 20, 2014
1,203
999
Nimejaribu kuchunguza kwa haraka nimegundua maduka mengi haswa ya uswazi wanauza vitu vya matumizi ya Binadamu, kama vile dawa ya panya, dawa ya mende, unga, mchele, mafuta ya taa, sabuni za unga na hata baadhi ya dawa kama vile panadol..

Ujumbe wangu kwenu hiii ni kitu hatarishi kwa maisha ya Binadamu, inaweza kuja tokea kuua mtaa au hata, familia pale unga wa dona kwa bahati mbaya ukaingia dawa ya PANYA AU MENDE,

najua maisha ni magumu ya mtaani watu hujaribu hiki na kile ili mladi kumnasa mteja,ila tujaribu kutenga hizi bidhaa jamani, tahadhari ni njema kabla ya hatari wakubwa..

Na kama hamuamini hili hebu pita kwenye maduka ya Manzese, Kimara, Tegeta, Mbagala, Kiko na mwananyamala kisha ulizia dawa ya panya kwenye duka lilijaa vitu vya kula utashangaa..

Nawasilisha wazo langu la J2 hii...
 
Observation nzuri, lakini hatuna utekelezaji wa karibu kwa mamlaka husika kwani hata ukienda ofisini kwa wenye mamlaka ya kisheria kushughulikia jambo kama hili utaishia kupokea majibu ya kuudhi.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom