Mambosasa: Kilichopelekea mwanafunzi wa UDSM akamatwe ni kusambaza uzushi mtandaoni

Ukiweka chuki binafsi pembeni, Mambosasa yupo sahihi kwa kiasi fulani, nini lengo la yule kijana kupost picha Facebook wakati kama kiongozi wa DARUSO alikuwa na nafasi ya kufikisha suala kwenye uongozi wa wanafunzi na kisha uongozi wa chuo? kimsingi lengo lake lilikuwa kuzua hofu na taharuki.

Ushari wangu ni kuwa afutiwe na mkopo kabisa. Zama hizi ni zama za JPM, watoto wa facebook lazima wadhibitiwe ili heshima irudi.
 
Sasa ni uzushi gani uliosambazwa hapo? Manake uzushi ni uongo.

Kilicho cha uongo kwenye hizo nyufa za hayo majengo ni nini au ni kipi?

Yaani hawa watu bana! Hivi huwa hata hawajistukii juu ya hizo pumba wazitoazo?

Foolish....
Mkuu leo umeandika kwa kupanic sana
 
hostel-jpg.643165

Unafaidika nini mkuu kuzoom picha ili ionekane kama kuna crack kuubwa? hili ni suala la kitaalamu waacheni mainjinia watupe majibu ya kitaalam.
 
Polisi wa Tanzania wanaajiriwa kwa kuzingatia urefu sifa za kitaluma huja badae. Polisi hata asome vipi lakini sifa ile ya msingi iliyomuingiza humo/urefu inatamalaki katika mambo mengi sana.. yani badala ya kumpongeza mtoa taarifa wao wanamkamata kisha badae wanataka polisi jamii. Ndo maana mnafanya maamuzi ya kukurupuka kwakuwa mna frastration.
 
Masikini Mambosasa.....

Pole sana katika jukumu la kutetea ugali wako!
 
TOYOTA kuna magari yao waligunduwa yana hitilafu kwenye exceleletor waliagiza magari hayo yote yarudishwe kiwandani, kwa sababu wenzetu wanaijuwa thamani ya uhai.

Ila hapa kwetu hata ya Shauritanga tumeshayasahau tumekalia vitisho tu shubaaamiti.
 
Kwa hiyo kakamatwa kwa kuonyesha watu uozo wa jengo ambalo lilitakiwa liwe ni siri !!?
 
TBA wakikamilisha matengeezo ya kasoro zilizojitokeza inapaswa hayo majengo tuyabadili jina na kuyaita jina la uyo kijana, uyu kijana ni shujaa na kumuita tu shujaa haitoshi , kuhamasisha na wengine kufichua mambo kama aya uyu kijana tumtunuku zile hostel kwa kuziita jina lake KUMBUSHO HOSTEL.
nakumbuka miaka ya nyuma pale mlimani kulikuwa na huozo na vibaraka kwenye huongozi wa wanafunzi(serikali ya wanafunzi walijaa vibaraka wa utawala wa chuo ) lakini kunamwanafunzi wa sheria aliyeitwa Twaha Ulimwengu aliongoza mapinduzi kwenye serikali ya wanafunzi (hii ni story ndefu inaitaji muda) kwa kifupi alipindua serikali ya vibaraka hapo chuoni na toka siku iyo hakatunukiwa jina la jenerali, na sehemu ambayo mapinduzi yalifanyika panaitwa Revolution Square.
modality nayojaribu kujenga hapa ni kuwa , ushujaa aliouonyesha uyu kijana usipite bure bila kumtunuku.
 
Kamanda wa polisi mkoa wa Dar Lazaro Mambosasa amesema walimkamata mwanafunzi Kumbusho Dawson baada ya kusambaza uzushi kwenye mtandao,

Kamanda ameelezea kama mwanafunzi huyo angekuwa na taarifa yoyote basi angeipeleka kwa mkandarsi wa majengo au mmiliki wa majengo hayo

Mtu aliyekuwa alalamike ni mmiliki wa majengo hayo na sio yeye

Pia amesema ameshangaa watu kulalamika na kupokea usumbufu mkubwa kwa jambo hilo wakati kuna maghorofa makubwa hapa Dar yalishaanguka na kuumiza watu lakini hakuna watu hawakuonyesha kuvutika kama ilivyokuwa kwa jambo hili


CLASS OF 2017 A country should and must be run as a country and not as a school.
 
Hivi kabla ya kumkamata si ingefaa kwenda kwanza kwenye tukio? Maana aliripoti na kuweka kielelezo kwa hivi ni vema kuprove Hilo kwanza. Tatizo naona ni kumtaja mtu. Ila no vizuri kuacha kutaja taja watu kwa matukio Kama haya
 
I think it is a public owned building. The owners are all the Tanzanians who are the tax payers. In my opinion.
 
Back
Top Bottom