Mambosasa: Mimi si msemaji wa Ikulu

pakaywatek

JF-Expert Member
Dec 28, 2014
4,636
6,261
Akijibu swali la mwandishi wa habari aliyetaka kusikia maoni ya jeshi la polisi, alisema yeye si msemaji wa Ikulu, mambo ya Ikulu kaulizwe mhusika wa Ikulu.

Pia amewaasa watu waache kusambaza mambo ambayo hawausiki nayo kusambaza wakitaka kujua jambo wakaulize wahusika kupata ufafanuzi.

=======

Kamanda wa Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam, SACP Lazaro Mambosasa, amewataka Watanzania kuacha kusambaza na kufuatilia taarifa za uzushi, badala yake wawafuate wahusika ili kujua undani wa taarifa hizo.

Kauli hiyo ameitoa hii leo Machi 17, 2021, jijini Dar es Salaam, mara baada ya kuulizwa swali la kwamba anauzungumziaje uzushi ambao umekuwa ukizushwa kwenye mitandao ya kijamii kuhusu Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Magufuli.

"Mimi sina cha kuzungumza kwa sababu mimi siyo Msemaji wa Ikulu, Msemaji wa Ikulu yupo, unaweza kumpelekea hilo swali atajibu, lakini ninachosema tu kwa Watanzania waache kuwa wazushi wa kupokea tarifa ambazo hawajazifuatilia na kujua ukweli wake, kuzisambaza na kuendelea kuvumisha uvumi ambao hauna maana viongozi wasemaje wapo anayetaka kulijua hilo awafuate viongozi wanaohusika," amesema Kamanda Mambosasa.

Chanzo: EATV
 
Attachments

  • Screenshot_20210317-213909.jpg
    Screenshot_20210317-213909.jpg
    51 KB · Views: 1
  • Screenshot_20210317-213857.jpg
    Screenshot_20210317-213857.jpg
    51.4 KB · Views: 1
Akijibu swali la mwandishi wa habari aliyetaka kusikia maoni ya jeshi la polisi, alisema yeye si msemaji wa ikulu mambo ya ikulu kaulizwe mhusika wa ikulu.

Pia amewaasa watu waache kusambaza mambo ambayo hawausiki nayo kusambaza wakitaka kujua jambo wakaulize wahusika kupata ufafanuzi.

=======

Kamanda wa Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam, SACP Lazaro Mambosasa, amewataka Watanzania kuacha kusambaza na kufuatilia taarifa za uzushi, badala yake wawafuate wahusika ili kujua undani wa taarifa hizo.

Kauli hiyo ameitoa hii leo Machi 17, 2021, jijini Dar es Salaam, mara baada ya kuulizwa swali la kwamba anauzungumziaje uzushi ambao umekuwa ukizushwa kwenye mitandao ya kijamii kuhusu Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Magufuli.

"Mimi sina cha kuzungumza kwa sababu mimi siyo Msemaji wa Ikulu, Msemaji wa Ikulu yupo, unaweza kumpelekea hilo swali atajibu, lakini ninachosema tu kwa Watanzania waache kuwa wazushi wa kupokea tarifa ambazo hawajazifuatilia na kujua ukweli wake, kuzisambaza na kuendelea kuvumisha uvumi ambao hauna maana viongozi wasemaje wapo anayetaka kulijua hilo awafuate viongozi wanaohusika," amesema Kamanda Mambosasa.

Chanzo: EATV
Sasa kama hausiki anayuzungumzia ya nini?
 
Back
Top Bottom