Mambo ya kuzingatia EAC kwa wanaogombea ubunge EAC

Oct 26, 2021
98
287
KWA WABUNGE WANAOMBA KURA KUWAKILISHA BUNGE LA EAC HAYA MAMBO MUHIMU SANA YA KUZINGATIA
"Asiyekubali kushindwa huyo sio mshindani"

Binafsi nianze kwakukipongeza chama cha mapinduzi (CCM) kwa namna nzuri iliyotumika katika kuwapata wagombea ubunge wa Afrika Mashariki kwa ngazi ya chama. Hakika mchakato ulikuwa mgumu sana ndani ya CCM, maana makada zaidi ya 452 waliomba ridhaa ya chama kuwateua wawe viongozi katika bunge la EAC.

Haki, usawa, uwazi, uzoefu, elimu na bila kusahau nidhamu na maadili ndio vitu pekee chama kilivizingatia katika uteuzi wa majina, nandio maana hutasikia mwanachama yoyote akilalamikia mchakato mzima maana kila mmoja alipewa fursa ya kujinadi kwa wabunge wa Jamhuri ya muungano wa Tanzania.
Ningependa baadhi ya mambo muhimu katika mtengamano huu wa EAC ambayo wateule wenzetu wa nafasi ya ubunge EAC wangeweza kuyasimamia na kuyatekeleza wakichaguliwa na waheshimiwa wabunge wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania tarehe 4/4/2017 mjini Dodoma.

Dondoo ni kama ifutavyooo:
1. Natural Resource.
a). Tanzania ni nchi mojawapo yenye rasilimali nyingi tulizo jaliwa na mwenyezi Mungu ukilinganisha na nchi nyingine wanachama ndani ya EAC. Kutokana na hili napendekeza rasilimali husika za nchi zibaki chini ya umiliki wa nchi husika (Resource ownership remains under the ownership of Tanzanians). Utajili kama ardhi(Land), mito, maziwa, madini n.k vibakie chini ya umiliki wa nchi husika.

b). Ulinzi wa Maliasili zetu pia ni muhimu sana kwa wabunge watakaochaguliwa kwenda kutuwakilisha katika bunge la Afrika Mashariki wafahamu umuhimu wa kutunza rasilimali zetu. kitu pekee hapa watumie fursa hiyo ndani ya EAC kuhakikisha

i) Joint efforts on combating Poaching incidents -Hapa naongelea masuala ya kuunganisha nguvu katika kupambana na majangili yanayo haribu maliasili zetu hasa kujihusisha na mauwaji wa tembo, faru, ukataji magogo, uchomaji misitu, n.k. Kuzuia ujangili ni gharama sana kwa nchi peke yake, maana baadhi ya majangili hutumia mipaka jirani kutorokea huko au kupitishia mizigo, lakini tukitumia juhudi hizi kwa pamoja itarahisisha sana kufanikisha hili tatizo la ujangili.

ii) Joint effort on promoting Tourism - Tanzania kama nchi wanachama ina viutio vingi sna na hifadhi 16, kwahiyo jitihada za pamoja zinahitajika sana katika kutanganza utalii wetu ili kupunguza gharama kwa nchi pekee kufanya utangazaji.

iii) Kulinda mazingira yetu kwakuhamasisha nchi wanachama umuhimu wa kutunza mazingira yetu. Njia pekee ni kuweka mkazo katika mambo yahusuyo mazingira kama kupanda miti, kusafisha kingo za mito, maziwa, kuzuia uvuvi haramu, kutupa taka ndani ya vyanzo vya maji n.k. hapa nipamoja na kulinda mipaka yetu vizuri, bila kuruhusu kufungua hovyo, mfano ni kuhakikisha tunaisimamia mpaka wa Borongoja kutofunguliwa japo wakenya wanaomba sana ufunguliwe katika mbuga ya Serengeti inayo pakana na Masai mara ya kwao.

2. Investment
Hapa hasa naongelea wabunge wetu watakaochaguliwa wahakikishe wanatengeneza mazingira rafiki na wezeshi ambayo yata wavutia wawekezaji kutoka nje ya EAC, ndani ya EAC kuja kuwekaza ndani ya jumuiya. Kama jumuiya tunahitaji sana Foreign Direct Investment ili waweze kukuza uchumi ndani ya nchi wananchama. Kwa sasa tupo kwenye soko la pamoja (Common Market) ambalo huongelea sana masuala ya mitaji, huduma, bidhaa na nguvu kazi. Hatuhitaji wawekezaji ndani ya EAC watoke ndani waende kuwekeza nje ya EAC.

Tuna karibu wananchi millioni 169 wanaotokana na nchi 6, kwahiyo tunalo soko tayari kilichobaki ni kuweka sera rafiki, (preferential treatment) kupunguza vikwazo vyovyote katika uwekezaji, uwazi wa mikataba, kuwalinda wawekezaji ilituweze kuwavutia waje kuwekeza nyumbani Tz ambao tunahubiri viwanda, na pia waje kuwekeza ndani ya jumuiya yetu EAC hasa kwa wekezaji wa ndani ya EAC. Tusiwaache waende na mitaji yao kuwekeza nje ya jumuiya.

3. Invite More Potential Members to join EAC
EAC bloc ni moja ya bloc ukilinganisha na ma bloc mengine lenye idadi ndogo ya nchi wanachama (has only 6 member countries) na wakati huo huo size ya Area ya ambayo 2.4 million sqkm ni ndogo ukilingnisha na bloc zingine kama SADC, COMESA, ECOWAS, IGAT, ACCA n.k. Pia lina watu wachache ambao ni kama millioni 169. Hii hujenga tafsiri kuwa EAc bloc haina soko la kutosha, nguvu kazi na ardhi kitu ambacho huwafanya wawekezaji kukimbilia kwenye ma bloc yenye idadi kubwa ya watu, nchi wanachama nyingi na Ardhi kubwa zaidi.

Napendekeza wabunge watakaochaguliwa tarehe 4/4/2017 watokao Tanzania wakahakikishe wanapambana sana kuhakikisha nchi jirani tunazo pakana nazo mipaka na zile za kimkakati tunazishawishi kujiunga na EAC. Mfano nchi kama Zambia, Malawi, Congo, Msumbiji n.k hizi nchi kwa sisi watanzania ni nchi rafiki tuna share mipaka, tumekuwa tukifanya nao biashara (wanatumia bandari ya Dar es Salaam maana wao ni LandLocked countries), tayari miundombinu ipo kama tazara, tunduma road, Lake nyasa, n.k. Hata hivyo migogoro inayoendelea kati ya Tanzania na Malawi inaweza ikaisha kama tutafanikiwa kuwashawishi Malawi wajiunga na EAC.

4. Language
Upande huu wa lugha, naomba nianze kwa kuwapongeza wabunge wa EAC wanaomaliza muda wao hasa hasa Mh. Shyrose Bhaji aliehakikisha lugha ya kiswahili inakuwa lugha maalumu katika bunge la EAC (Official Language). Kupitishwa tu hakutoshi tunahitaji mikakati zaidi ilikuhakikisha hii lugha inaongelewa na wananchi wa jumuiya ya EAC.

i). Kuhakikisha tunaweka sera itakayoruhusu kila nchi wanachama ndani ya EAC wanaweka Kiswahili kama somo katika shule za msingi au awali. Hii itasaidia kukifanya kizazi kijacho kiweze kuongea vizuri kiswahili. Pia itaongeza ajira kwa watanzania na wakenya maana wao huongea kiswahili vizuri.

ii). Kuhakikisha EAC inaunda TV na radio yake kama vyombo vitakavyotumika kukieneza kiswahili na kuifanya EAC wananchi kuijua zaidi.

iii). Kuhakikisha EAC inakuwa na kitengo cha masuala ya utafsiri (Interpreter institution)
iv). Kutumia Youth platformna na social media
v). Kuunda chombo ndani ya EAC kitakacho tumika kuwafundisha waheshimiwa wabunge lugha ya kiswahili kwa muda mfupi baada ya kuchaguliwa.
vi) kuruhusu nchi wananchama kuunda taasisi zitakazo tumika kuwafundisha wananchi wa nchi ambazo hawaongei kiswahili waweze kujifunza kiswahili cha kuongea kwa muda mfupi na kwa bei nafuu. Itaongeza ajira kwa watanzania na fursa.

5. Monetary and Fiscal Policies.
Kwenye eneo hili ya masuala ya fedha na uchumi, ni muhimu sana kwa jumuiya ya EAC kwa sasa kuanzisha Benki ya EAC, ambayo itatumika
i). Kama daraja la kuelekea sarafu moja (Monetary Union). Itasaidia sana kuweza kusimamia na kuendesha shughuli nyingi za kuhakikisha tunakuwa na sarafu moja.
ii). Kukopesha wajasiliamali wa nchi wananchama, mfano wale wanaotaka kuja kuwekeza ndani ya EAC lakini ni wawekezaji wa ndani itawasaidia kuwaongezea mtaji
iii). Kuwakopesha wakulima hasa katika eneo la umwagiliaji (Irrigaion schemes) maana kwa sasa karibu nchi zote ndani EAC zinatatizo la Ukame (Drought) kama janga, kwahiyo mikakati mingi ya kuwawezesha wakulima hasa cha umwagiliaji ili kuifanya bloc ya EAC yenye chakula wakati wote na ikiwezekana hata kuuza nje ya EAC bloc.
iv). Kuendelea kukopesha nchi wanachama katika miradi mikubwa hasa ya miuundombinu inayoounganisha nchi wanachama EAC kama barabara, reli n.k
6. Strengthening EAC Identity

Mpaka sasa vitu vinavyo tutambulisha sisi kama EAC ni wimbo wa EAC (Anthem), EAC flag, EAC Passport ambayo ipo valid tu ndani ya EAc members only. Wawakilishi wetu wanatakiwa wahakikishe EAC passport inatabulika na nchi wanachama pamoja nakuifanya itumike kimataifa (Internationalising EAC-Passport). Also making sure Kiswahili is used within EAC and allover the World. Feel proud when you speak swahili and don't feel inferior on using swahili laguage on international organization.

7. Advocate for jobs and opportunities for young Tanzanians and EAC people at large.
Wawakilishi wetu muhakikishe mnatengeneza ajira na fursa kwa vijana wenu huku Tanzania maana kwa kutumia fursa ya wewe kuwa mbunge fungueni macho ili muweze kuona fursa zaidi ambazo zitasaidia kukuza uchumi wa nchi yetu. Undeni Employment commission itakayo jielekeza katika kuwapatia equal treatment ya kupata ajira na fursa katika Afrika mashariki.

8. Promote Peace, security to the Partner states.
Wawakilishi wetu hakikisheni amani na utulivu ndani ya jumuiya unakuwa imara zaidi kwa kulinda na kusimamia sheria, kanuni na democrasia kuhakikisha hakuna mtu wa kuhatarisha amani yetu sisi watanzania pamoja na nchi wanachama. Kuwa mawakala wazuri wa amani hasa wakati wa chaguzi zetu, pia ubadilishaji wa madaraka ufanyike kwa amani, viongozi waheshimu democrasia za nchi zao.

Maana mkiweza kuisimamia amani iliyopo itasaidia hata wawekezaji (Foreign Direct Investment) kuja kuwekeza, watalii (Tourist) kuja kutalii, wananchi kufanya kazi na kusababisha uchumi kukua ndani ya jumuiya.

Naomba niishie hapa, chamsingi sisi ka watanzania tunategemea utumishi mwema kwa wote mtakaochaguliwa na wabunge tarehe 4/4/2017 kuwa wawakilishi wetu katika bunge la Afrika Mashariki (EAC). Baadhi ya mambo niliyojaribu kuyaeleza jitahidini muyasimamie maana tunahiaji kuona kama nchi tunafaidika na huu mtengamano wa EAC kichumi, kisiasa, kiutamaduni na kijamii. Nawatakia uchaguzi mwema wote mliosahiliwa na vyama vyote kushiriki usahili tarehe 4/4/2017, nimatumaini yangu wabunge watachagua watu makini sana watakao tuwakilisha katika bunge la Afrika Mashariki.

Sote tunawajibu wakujena nchi yetu.

TANZANIA KWANZA.
BY RRM.

17635409_1549926891717285_8648175381494145193_o.jpg
 
Back
Top Bottom