Mambo ya diamond platnumz

Fruit

Senior Member
Jan 1, 2013
193
54
Ustadhi Yahya Michael, mkazi wa Dar, hivi karibuni amejitokeza na kudai kuwa yeye ndiye mganga aliyempaisha mwanamuziki Nasibu Abdu ‘Diamond Platnumz’ ambaye kwa sasa ni kinara wa Bongo Fleva, Risasi Jumamosi lina mkanda kamili.

MH! SIKU HIZI ANAJIFANYA SUPASTAA

Akizungumza na gazeti hili katika mahojiano maalum maeneo ya Magomeni, Dar, mganga huyo alidai kuwa pamoja na jitihada kubwa alizofanya kumpaisha Diamond lakini anamshangaa kwa kuwa amesahau alikotoka na anajifanya supastaa.

Alidai kuwa siku hizi akimpigia simu, Diamond huwa hapokei, tofauti na zamani… Stori: Hamida Hassan na Gladness Mallya
Ustadhi Yahya Michael, mkazi wa Dar, hivi karibuni amejitokeza na kudai kuwa yeye ndiye mganga aliyempaisha mwanamuziki Nasibu Abdu ‘Diamond Platnumz’ ambaye kwa sasa ni kinara wa Bongo Fleva, Risasi Jumamosi lina mkanda kamili.
MH! SIKU HIZI ANAJIFANYA SUPASTAA
Akizungumza na gazeti hili katika mahojiano maalum maeneo ya Magomeni, Dar, mganga huyo alidai kuwa pamoja na jitihada kubwa alizofanya kumpaisha Diamond lakini anamshangaa kwa kuwa amesahau alikotoka na anajifanya supastaa.
Alidai kuwa siku hizi akimpigia simu, Diamond huwa hapokei, tofauti na zamani alipokuwa akihangaika kuchomoka kisanii.
Mganga huyo alifunguka kuwa sababu ya kufanya hivyo ni baada ya kuchukuliwa na watu waliompeleka kwa waganga wa Kigoma ambako anajidanganya kuwa ndiyo wanampaisha kumbe walimchukua akiwa ameshampandisha kwa kumpa dawa kali za mvuto.

ALIMPA DAWA GANI?
Alizitaja dawa alizompatia Diamond kuwa ni mitishamba aina ya Dubi, Ntajamasala (hii humfanya watu wamuogope na kumheshimu), Italigula, Nkangacharo na Kalila Lila (ambayo huichoma na kuoga kwa ajili ya kuwavutia watu).

ANGUKO LA DIAMOND
Alidai kuwa Diamond amejisahau na hajui kama anguko lake linakuja kufuatia ahadi aliyoiweka wakati anaanza kuimba baada ya kumpatia dawa hivyo atapotea kwenye muziki.
Akielezea historia ya kukutana kwao, Ustadhi Yahya alisema yeye na staa huyo walikutana miaka ya 2000 nyumbani kwa Papaa Misifa ambaye alikuwa meneja wa Diamond.
Alidai kuwa kubadilika kwa Diamond kulikuja baada ya kutwaa tuzo tatu za Kili mwaka 2010 ndipo akawa anahusudu wanawake tofauti na masharti ya dawa japokuwa alimkanya lakini hakumsikia.

DIAMOND ANASEMAJE?
Kama ilivyo desturi ya gazeti hili, lilimgeukia Diamond ili kupata mzani wa habari hiyo ambapo alipopatikana kwa njia ya simu alisomewa maelezo yake yote.

AMKANA
Katika maelezo yake, Diamond alikataa kata kata kuwa hamfahamu mtu huyo kisha akakata simu.
“Sina msikiti nitakuwaje na Ustadhi? Huyo mganga nasema simfahamu,” alisema kisha akakata simu.
 
mods.huu uzi uhamishewe jukwaa la burudanh na michezo.magazeti ya udaku ya shigongo na jf wapina wapi.tunapoteza hadhi ya janvi hili.
 
Hivi huyo mganga yeye mwenyewe hataki kupaa? Mbona anapaisha wengine tu na yeye bado yuko hapohapo?

Kweli mdau, pia watz hupenda wakim-support mtu abaki palepale ili waendelee kun-support na akichomoka inakuwa tena story kwamba amewasahau, unapomsaidia mtu lengo ni kumnyanyua ili na yeye awe katika maisha bora lakini engi wetu utasikia jamaa amejisahau hakuna kutukumbuka tena (ule msemo wa TENDA WEMA NENDA ZA........ huwa watu wanausema kinafiki tu huwa hawamaanishi).
 
Hiyo dawa ya DUBI na NTAJAMASALA aliyompa Diamond ni bora sasa mganga aitumie mwenyewe ili diamond aogope na atishike, lakini kama walipeana dawa za kienyeji WAKALIPANA basi kila mtu "KIVYAKE"
 
Wana sema almasi ni wa fm. Sasa lina ibuka ni ndumba za kiganga mmh. Watu hawakosi vya kusema bna mara freemasoon mara uchawii.
Tume wazooea na uzushi wamaneno so mtu asifanikiwe tu haya mna ongea. Vitu ambavyo havipo kabitha kah.
 
Hivi Diamond ana ugomvi na Shigongo? mbona ameamua kumchafua hivi? na huyo mgongo ethics zake za kazi zinasemaje?kwanini mambo yake na Diamond ayaweke hadharani? huyu mganga ni msanii na anajipigia promo tu hana lolote... Diamond kamua kaka....
 
Hiyo dawa ya DUBI na NTAJAMASALA aliyompa Diamond ni bora sasa mganga aitumie mwenyewe ili diamond aogope na atishike, lakini kama walipeana dawa za kienyeji WAKALIPANA basi kila mtu "KIVYAKE"

Hata mimi nashangaa! Kama ilikua business akakulipa pesa yako, sasa unampigia simu ili iwaje? Kwa taarifa yako Shigongo, huo udaku wako unazidi kumpa chart Diamond. Kama mimi nilikua simjui, nikaja mjua baada ya kuanza kuandikwa anatenbea na Wema. Mwaya kaza buti, ongeza ubunifu. Ukipata plan na kwa maisha ya baadae yasije yakakukuta ta Mr. Nice
 
Hawa wanao mpa air time huyi mganga ndio washirikina!
 
Back
Top Bottom