Mambo nayopenda kwa Waislamu japo ni Mkristo

OKW BOBAN SUNZU

Platinum Member
Aug 24, 2011
49,237
103,891
Pamoja na ukristo wangu yapo mambo kadhaa nayoyapenda kwa waislamu.

1. Kutoruhusu mtume wao adhalilishwe au kudhihakiwa. Huwezi kumkashfu mtume au kitabu chao cha Quran mbele yao halafu wakutazame tu. Lazima wakuletee noma

2. Mavazi ya staha kwa wanawake
Napenda sana dress code kwa wanawake. Wanavaa mavazi ya staha. Sehemu za ibada huwezi kuvaa kihuni-huni ukaingia

3. Kutengana wanawake na wanaume kwenye ibada zao

4. Kuruhusu ndoa ya mke zaidi ya mmoja kwa mtu mwenye uwezo wa kuwatunza.

5. Utoaji wa sadaka usiotia umasikini

6: Kuharakisha mazishi.

7. Kutomtenga muumini (Hapa uswali ama usiswali ilimradi wewe ni muislamu ukifa hamna longolongo utazikwa mahali popote! Njoo kwetu!

8: Kuharakisha ndoa! Hamna longolongo!
 
Hata mimi kuna vitu nimeona vimenivutia mno kama misiba hata kama siyo ndugu yao utaona wanajitolea mzika na kumsalia.

Siku kama hizi za mfungo wanalisha maskini ili wasishindwe funga, misikitini wanachanganyika maskini na tajiri, kiongozi na kapuka.
 
Back
Top Bottom