Mambo Muhimu katika sheria ya ndoa!

Umeona na wewe kaka,

Yaani kwanza ni jukumu lako kumtunza mtoto wa watu...na halafu sheria inampa mamlaka ya kuuza phoenix yako ili eti akalipie matumizi yake na mtoto.

Hii sheria inahitaji marekebisho ya haraka sana.

Ndio maana mimi napendekeza kwamba ndoa ziwe katika mfumo wa corporate union. Kila mtu awe na shea zake ili mambo yakienda mrama ajue anachoambulia!!

Corporate union??? Dah umefika mbali! Kimsingi sheria hii iliandikwa wakati wanawake wamekandamizwa sana. Ila kwa sasa Law Reform

commission imependekeza mabadiliko yake. Ikiwa wataileta hadharani tusikawie kutoa maoni yetu!
 
Seriously, inabidi tuanze kuziangalia ndoa kiuchumi pia.

Niliwahi kutoa mawazo yangu kuhusu hili suala hapa JF na bado naamini ndoa za kisasa zinatakiwa kuangalia mchango wa mwanandoa ili kuamua nini anamiliki na anastahili kupata ndoa inapoparaganyika!!
 
Kuvunjika kwa uchumba!
Ikiwa kuna ahadi mlipeana halafu mkaingia some expenditures in that relationship, thereafter ahadi hiyo ya kuoana ikavunjwa ama ndani ya nchi au

nje ya nchi (umepigwa kibuti), unaweza kwenda mahakamani kudai fidia. Hii itawezekana pale ambapo ulimpa mchumba wako mali ukijua kabisa

mtakuja kuoana. Kwa mfano kama ulimjengea nyumba au ulimpa gari ukijua kabisa kwamba unampa mkeo mtarajiwa basi unaweza kwenda

mahakamani. Ila huwezi kwenda mahakamani kutaka specific performance 'Kulazimisha kufunga ndoa' maana ndoa ni hiari ya mtu.
 
Seriously, inabidi tuanze kuziangalia ndoa kiuchumi pia.

Niliwahi kutoa mawazo yangu kuhusu hili suala hapa JF na bado naamini ndoa za kisasa zinatakiwa kuangalia mchango wa mwanandoa ili kuamua nini anamiliki na anastahili kupata ndoa inapoparaganyika!!

Kuna concept mpya inaitwa economic refugees. Hawa ni watu wenye shida za kiuchumi, wamepigika! Sasa wanatafuta mtu mwenye pesa

wamuoe au waolewe nae ili kuepukana na shida zake. Nadhani suggestion yako itafaa kuondokana na matatizo haya
 
Nadhani "opportunist(s)" linafaa zaidi ya "refugee".
 
Mpenzi wako akimengwa na bado unampenda unaweza ukadai fidia na ukasonga mbele kama kawa

S. 72. (1) A husband or wife may bring a suit for damages against

any person with whom his or her spouse has committed adultery:

Provided that no such proceeding shall lie-

(a) where the aggrieved party has consented to or connived at the

adultery;

(b) where damages in respect of the alleged adultery have been

claimed in a petition for divorce.

(2) A suit brought under this section shall be dismissed if the

defendant satisfies the court that he or she did not know and could

not, by the exercise of reasonable diligence, have known that the

person with whom he or she committed the act of adultery was

married.
 
Ieleweke tuu kwamba mali mnazopata nkiwa ndani ya ndoa zinakuwa ni za wote labda pale ambapo itathibitika bila shaka kuwa ilikusudiwa mali iwe ni

ya mmoja wao. Kitendo cha kuongeza thamani katika mali hiyo, mfano kurekebisha nyumba, kujenga fensi nk inatosha kumpa mwenzi wako haki

katika mali hiyo na itachukuliwa kuwa wote mna share sawa katika mali hiyo. Ieleweke kwamba kwa mujibu wa kesi ya Bihawa Mohammed v Ali Sefu (moja ya kesi chache ambazo court of appeal imeamua kwa haki) hata kitendo cha mkeo kuwa mama wa nyumbani kinachangia yeye

kupata haki katika mali zenu
 
Katika hii kesi sina ugomvi na mwanamke kupewa mali walizochuma na mume wake. Ugomvi wangu ni kutoa 50% kwa 50%. Binafsi naamini kwamba haiwezekani watu wawili wakazalisha kwa usawa wa kiasi hicho.

Katika mazingira ya sasa...Ni muhimu kuweka kanuni zinazoweza kukutoa mchango wa kila mwanandoa kwenye mali walizochuma pamoja (matrimonial property)
 
Kuna ugumu katika kupima hasa pale ambapo mwanamke anachangia 'invisibly' ! Labda concept hii intokana na philosphy kwamba mkioana

mnakuwa mwili mmoja na mnapotengana mnapata nusu mbili zilizo sawa
 
Hiyo imekaa ki-theory zaidi.....Hata hiyo habari ya mwili mmoja pia imekaa hivyo hivyo. Endapo sheria mpya itatoa ruhusa mtu ku-withdraw hiari yake ya kuendelea kuwemo kwenye ndoa, maana yake kila mtu anakuwa na mwili wake ama ndani au nje ya ndoa. Hapo ndipo tutakapoanza kuona uhalisia hata kwenye mali. Mchango wowote inabdia upewe thamani badala ya kuita invisible contribution.
 
Back
Top Bottom