Mambo Huangamia cha Chinua Achebe

Kanungila Karim

JF-Expert Member
Apr 29, 2016
20,744
25,447
Mambo Huangamia (kwa Kiingereza "Things Fall Apart") ni riwaya iliyoandikwa na Chinua Achebe. Ilitolewa mwaka wa 1958 . Hadithi ya riwaya hii imefuatiwa na Hakuna Starehe Tena (1960) na
Mshale wa Mungu (1964).


Mkondo wa hadithi
Mhusika mkuu anaitwa Okonkwo , tajiri katika kijiji cha Umuofia . Huyo Okonkwo hufuata mila na desturi za Kiigbo vizuri sana ili kumshinda babake ambaye ni mduni. Katika kufuata hizo mila alifika hatua ya kumuua mwana wake wa kambo na wanakijiji wakakubali. Siku moja lakini Okonkwo kwa bahati mbaya alimuua mwanakijiji mwingine na sasa akahukumiwa kuondoka kijijini kwake kwa miaka saba zinavyoamuru mila za kijiji. Huko uhamishoni Okonkwo alikutana na wamisionari Wazungu, akasikitika sana kugundua mwana wake mwenyewe aliacha mila za Kiigbo na kukubali dini ya Ukristo. Okonkwo akirudi kijijini baadaye akakuta hata maisha ya kijijini yameathiriwa na hiyo dini mpya. Akaanza kuupigia vita Ukristo, hatimaye lakini aliona kuwa haiwezekani kurudi kwa maisha ya kimila akajiua kwa kujinyonga.
 
Baba yake Okonkwo alikuwa mla madeni hodari pale kijijini kama unamdai hela ndogo halafu ukaenda kumdai anakuambia
"The sun rises first to the standing ones then to the sitting ones"
kwa hiyo lazima usubiri awalipe wanaomdai madeni makubwa halafu ndo na wewe utalipwa.
hadi anakufa alikuwa anadaiwa na umati wa wanakijiji.
 
Nakumvuka kwa mbali hii kitabu Luna sehemu nadhani ndo wamissionary walipofika na inteprter wao conversation yao ilikua hivi

Interpreter :and God send his son Jesus


Cjui ndo okonko :if he had son Jesus then what the name of his wife


Watu wakadata baada ya kuambiwa Mungu hana mke
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom