Mambo 5 ambayo Watanzania waliokuwa 'gwandalized' wanayakataa kuhusu CCM na serikali yake

Mzee Mwanakijiji

Platinum Member
Mar 10, 2006
33,476
39,995



[h=2]Mambo 5 ambayo Watanzania wanayakataa na hawatovulimia tena chini ya CCM[/h] Na. M. M. Mwanakijiji
3848880_orig.jpg

Nimejaribu kutafakari kwanini kuna wimbi la watu kuikataa CCM na serikali yake kwa nguvu zaidi wakati huu kama ilivyokuwa mwaka 1995. Miaka mingi imepita lakini wakati mwaka 1995 ilikuwa kwa kiasi kikubwa ni kutumia uhuru wa kujiunga na chama kingine zaidi ya CCM safari hii kuna kitu tofauti kinajionesha wazi. Watanzania kwa maelefu – mijini na vijijini, wazee kwa vijana, wake kwa waume – wameamua kuiambia CCM “Bye Bye” na kujiunga kwa mbwembwe kwenye CHAMA CHA DEMOKRASIA NA MAENDELEO. Nilipotafakari zaidi mang’amuzi haya mapya yanayoendelea nimejikuta nikirudi nyuma zaidi karibu miaka hamsini iliyopita.


Vitu vile vile vilivyowafanya Watanganyika na Waafrika kwa ujumla kuukataa ukoloni na serikali yake vimeanza kukataliwa tena na safari hii si dhidi ya ukoloni bali dhidi ya utawala ambao umegeuka na wenyewe na mwelekeo wa ukoloni usiopingika. Mambo haya matano manne kati yake yanajulikana sana kwani yamekuwepo katika tangazo la Azimio la Arusha la mwaka 1967 na ambalo ukweli wake bado unasimama.


Katika Azimio la Arusha tulitangaza hivi: Tumeonewa kiasi cha kutosha, tumenyonywa kiasi cha kututosha, tumenyanyaswa kiasi cha kutosha na tumepuuzwa kiasi cha kutosha… Ni unyonge wetu ndio uliotufanya tuonewe, tunyonywe, tunyanyaswe na tupuuzwe. Sasa tunataka mapinduzi ili tusionewe, tusinyanyaswe na tusipuuzwe tena!” Hivyo mambo manne ya kwanza ambayo Watanzania wanayakataa ni kuonewa, kunyonywa, kunyanyaswa na kupuuzwa. Tuyaangalie haya kidogo:

SOMA HAPA NA MWAMBIE MWINGINE
 
mwanakijiji yaani naona leo umeamua kutupia vitu nondo kwa elimu uraia na mkutano wetu kesho. Bravo to u MMM. Ukombozi uko mikononi mwetu.
 
As much as i don't like CCM....

bado naamini bado ni chama imara hata kama kinapungua nguvu as siku zinavyokwenda

sasa tusiamini sana kuwa CCM 'imekwisha'

safari bado ndefu mno kwa wapinzani....

tusiamini 'this hype'.....ya kuwa CHADEMA sasa mlango uko wazi...
 
As much as i don't like CCM....

bado naamini bado ni chama imara hata kama kinapungua nguvu as siku zinavyokwenda

Kauli yako ni kilele cha kujipinga.. unamuona mtu anatumbukia shimoni halafu unasema 'inawezekana kweli anatumbukia shimoni lakini nina imani hatotumbukia'..
 
Kauli yako ni kilele cha kujipinga.. unamuona mtu anatumbukia shimoni halafu unasema 'inawezekana kweli anatumbukia shimoni lakini nina imani hatotumbukia'..

Mzee Mwanakijiji,

Wasalaam.

Najipambanua kuwa shabiki na mpenzi Wa makala zako. Swali; je ninaruhusiwa kuzitumia, namaanisha kuzibandua na kuzibandika mahali pengine kwa faida ya watanzania?

Namini itawasaidia wengine wote na ndio maana sija Pm.

Alamsiki!
 
CCK vipi hawapati wanachama?

Chadema ni nguvu ya soda kama ilivyokuwa CUF na NCCR kabla. Viko wapi? na maskini CCJ ndiyo ilikufa kabla ya kuzaliwa. CCK sijui imefia wapi.

CHADEMA tumesha anza kuona mivutano isiyo na mfano, Mbowe anasema ni demokrasia, Slaa anasema si chochote, Heche anasema kakosea, Naibu wake anasema Heche ndio kakosea.

Ukija upande mwingine, ushawahi kumuona Slaa na Zitto wakiwa pamoja? Mawee.

Sakata la kugombea Urais, kugombea vyeo ndani ya CHADEMA ndio litazuwa mvurugano usio na mfano.

Kuna vijana ambao wamo ndani jikoni (Kina TUNTEMEKE), wanaona jinsi chama kinavyopelekwa kubaya, kuna wakuu ndani humo wanalazimishwa na wachumba zao wawafukuze wengine ndani ya chama. Kuna salama hapo? Kuna ukabila unaoongelewa waziwazi na wana CHADEMA, kama unabisha muuilize Shibuda. Kuna usalama hapo.

CCM bado tupo juu sana, mnayoona yanayopukutika ni magamba kama ilivyo dhanna. Mlifikiri kujivuwa gamba ni kitu hafifu? ni highly scientific.

Tunangoja kuona watu wanavyochaniana magwanda, maana fukuto la huko (Kama unabisha muulize TUNTEMEKE) halisemeki.
 
bado naamini bado ni chama imara hata kama kinapungua nguvu as siku zinavyokwenda
...


Umesahau jambo moja muhimu sana. Tofauti na huko nyuma, sasa hivi hatuna CCM. Hakuna! Tuna vijikundi vidogo vidogo vinavyofanya siasa chini ya brand name CCM, wenye CCM walishakufa miaka mingi. Na kila kijikundi kinamvinzia mwingine, magamba saga ni trailer, sinema yenyewe bado.
 
Mzee Mwanakijiji,

Wasalaam.

Najipambanua kuwa shabiki na mpenzi Wa makala zako. Swali; je ninaruhusiwa kuzitumia, namaanisha kuzibandua na kuzibandika mahali pengine kwa faida ya watanzania?

Namini itawasaidia wengine wote na ndio maana sija Pm.

Alamsiki!

unaruhusiwa chini ya conditions mbili: usibadilishe maneno (isipokuwa kusahihisha makosa ya kiuandishi) na usibadilishe jina la mtunzi. Enjoy!
 
CCK vipi hawapati wanachama?

Chadema ni nguvu ya soda kama ilivyokuwa CUF na NCCR kabla. Viko wapi? na maskini CCJ ndiyo ilikufa kabla ya kuzaliwa. CCK sijui imefia wapi.

CHADEMA tumesha anza kuona mivutano isiyo na mfano, Mbowe anasema ni demokrasia, Slaa anasema si chochote, Heche anasema kakosea, Naibu wake anasema Heche ndio kakosea.

Ukija upande mwingine, ushawahi kumuona Slaa na Zitto wakiwa pamoja? Mawee.

Sakata la kugombea Urais, kugombea vyeo ndani ya CHADEMA ndio litazuwa mvurugano usio na mfano.

Kuna vijana ambao wamo ndani jikoni (Kina TUNTEMEKE), wanaona jinsi chama kinavyopelekwa kubaya, kuna wakuu ndani humo wanalazimishwa na wachumba zao wawafukuze wengine ndani ya chama. Kuna salama hapo? Kuna ukabila unaoongelewa waziwazi na wana CHADEMA, kama unabisha muuilize Shibuda. Kuna usalama hapo.

CCM bado tupo juu sana, mnayoona yanayopukutika ni magamba kama ilivyo dhanna. Mlifikiri kujivuwa gamba ni kitu hafifu? ni highly scientific.

Tunangoja kuona watu wanavyochaniana magwanda, maana fukuto la huko (Kama unabisha muulize TUNTEMEKE) halisemeki.

Mtawanga sana Mwaka huu
 
Safi..........hakika tumechoka Kuonewa, Kunyonywa, Kunyanyaswa, Kupuuzwa na Kudanganywa. Kwakuwa tushatambua ni vitu gani hatuvitaki, there is no turning back.
 
1. Tumeonewa
Watanzania wameamua kukataa kuonewa na watawala wao. Kuonewa huku kunakuja kwa aina nyingi sana lakini kubwa ni ile hisia ya tofauti kati ya watawala na watawaliwa ambapo watawala ambao kutokana na nafasi zao wanajiaminisha kuwa wanaweza kufanya lolote, kwa yeyote aliye chini yao. Mifano miwili iko wazi sana kuwakilisha hili. Wengi mnakumbuka yule DC aliyemzaba kibao baba wa watu mbele za watu na hakukemewa na Rais Kikwete wala viongozi wengine. Wapo watu wengi sana ambao wamejikuta wakionewa na watawala iwe katika ajira, biashara au hata nafasi tu. Matokeo yake Watanzania hawa wamejikuta wakilazimika (sijui kama ni sawa kuita kulazimika au kulazimishwa) wanatafuta kujipendekeza kwa watawala hao ili ‘mambo yao yawanyokee'.
Ni uonevu wa kiutawala ambao unalazimisha wananchi wa kawaida kuwa kama vijakazi mbele ya watawala. Ni uonevu unaowafanya watawala waweze kutoa maagizo yoyote kwa sababu ya utawala wao. Tumeona watu wetu walivyohamishwa kwa nguvu sehemu mbalimbali ili kupisha ‘wawekezaji' tumeona mahali ambapo watu wamenyang'anywa maeneo waliyokuwa wanalima mazao ya chakula ili waje watu kulima mazao ya ‘mafuta'! Sasa Watanzania hawa wameamua kukataa kuonewa tena!
2. Tumenyonywa
Sasa mojawapo ya mambo ambayo Azimio la Arusha lilipambana nalo ni kile Mwalimu alikiita "exploitation of man by man'. Kwa wanaokumbuka vizuri tatizo kubwa la ubepari mahali pote duniani ni kuwa unatengeneza tabaka la wanaofanya kazi na kuhenyeka na wanaokunja nne na kubweteka wakila matunda ya jasho la wengine. Unyonyaji huu ambao umesifiwa kuwa ni ‘ubepari" au mfumo wa mtaji (capitalism) umesifiwa sana kwa kuinua maisha ya watu hasa kwa kuongeza ushindani. Lakini utabiri wa Nyerere juu ya mfumo huu umekuwa wa kweli na matokeo yake miaka hamsini tangu aandike yale yanatimia. Nashauri watu wasome "A Rational Choice" ambapo Mwalimu anaelezea kwanini kwa taifa changa kama la kwetu uchaguzi sahihi ulikuwa ni ujamaa na si ubepari.
Sasa ubepari una matokeo mazuri vile vile hasa kwenye level ya ushindani. Lakini ni ushindani wa nani hasa? Nyerere anaelezea kwa kweli siyo ushindani wa mtu mwenye biashara ndogondogo na kampuni kubwa ya kimataifa! Huwezi kumshindanisha mchimba madini wa Chunya na Barrick au Ango-Ashanti Gold. Huyu mchimba madini hana ubavu! Huwezi kushindanisha kwa mfano kiwanda kidogo cha kutengeneza baskeli na kiwanda kikubwa cha kutengeneza baskeli cha huko Marekani. Matokeo ya ushindani huu mara zote ni kuwa makampuni makubwa ndio yatanufaika na wafanyabiashara ndogo wataendelea kufanya biashara ndogo au – kama Nyerere alivyoonesha kwenye maandishi hayo – yule mkubwa anapoamua kumnunua yule mdogo!Dunia imetambua hili na miaka kama kumi iliopita mwamko wa kuupinga huu ubepari wa kimataifa umeibuka katika kampeni ya kupinga utandawazi ambapo ubepari ulivuka mipaka ya nchi na kuanza kuingia kwa nguvu kwenye nchi maskini ambapo kweli walileta viwanda vikubwa lakini wakati huo huo kuua kabisa viwanda vya ndani na ushindani mdogo wa ndani. Kumbe unyonyaji ambao umetokea sasa siyo wa mtu na mtu tena bali ni unyonyaji wa makampuni makubwa ya kimataifa dhidi ya vijimiradi vidogo vya baba, mama na vijana wetu!Hivyo, Watanzania wanakataa kunyonywa; wanakataa kugeuzwa vijakazi na watumishi wanaovaa suti za kupendeza za makampuni makubwa ya kimataifa ambayo kutokana na sera zilizopo yanaweza kuzalisha nchini nakuondoa faida yote kwa asilimia 100 kuipeleka kwao. Yaani, makampuni ambayo yamekuja na kugeuza Tanzania shamba lao. Na hili linatisha zaidi hasa pale ambapo serikali inakubali kampuni ya kigeni kukodi eneo la ardhi na kupanda mazao ya chakula ambayo soko lake kwa asilimia 100 ni kwenda kwenye nchi zao! Kuna uwezekano huko baadaye watu watu wakawa wanakufa njaa wakati mashamba ya wageni yanazalisha chakula na kupelekwa nje na watu wetu watakapoanza kulalamika wataambiwa "ndio mkataba unavyosema!"Hivyo, wanakataa kuonewa kwa namna yoyote ile kwani wameshaonewa kiasi cha ‘kutosha'!
3. Tumenyanyaswa
Sasa hili la kunyanyaswa linaendana na hilo la kunyonywa. Wakati hili la kunyonywa linahusiana na mahusiano ya kiuchumi hili la kunyanyaswa linahusiana na mahusiano ya mtu na mtu katika jamii na hasa kati ya wale walionacho na wale wasionacho. Wale walionacho wanaweza kujipatia lolote katika jamii wakati wale wenzangu na miye inabidi wajitahidi sana kupata kidogo wanachokipata. Ni unyanyasaji wa kimfumo. Fikiria kwamba hakuna kiongozi mkubwa wa kitaifa ambaye anata tatizo la umeme au maji! Yeye ameweza kujiwekea posho au utaratibu wa kununua genereta na mafuta yake (iwe nyumbani au ofisini) na ana uhakika wa usafiri wake (lipo gari la serikali kumpeleka kokote). Mtu wa kawaida hata hivyo anapata shida ya maji na umeme kwa sababu vitu hivyo ni anasa kwake na anapojaribu kuvitafuta ni manyanyaso ya kila namna.
Lakini unyanyasaji mwingine ambao uko wazi – na watu wenye madaraka hauwagusi – ni kutotendewa kwa heshima wanakofanyiwa wananchi wanapotaka huduma mbalimbali. Hivi majuzi nilikuwa na mjadala mnono kwenye FB yangu na mambo mengi yakawa dhahiri. Mtu anapoondoka nyumbani kwenda kutafuta huduma hasa kwenye taasisi ya serikali anatakiwa ajiandae kihisia na kiakili; kuna kuzungushwa, kuna kucheleweshwa, kunakusumbuliwa kiasi kwamba anaporudi nyumbani anakuwa hoi bin taaban si kwa sababu ya safari bali sababu ya watu aliokutana nao. Ni kunyanyaswa kunakofanyiwa mtu duni kulinganisha na heshima anayopewa mtu ‘anayejulikana'. Hili Watanzania wanalikataa.
4. Tumepuuzwa
Sasa hayo matatu ya kwanza yote yanahusiana moja kwa moja na jinsi mtu anavyotendewa. Lakini hakuna kitu kinachoudhi zaidi kama mtu kupuuzwa. Unapompuuza mtu kimsingi unamuondolea umuhimu wake alionao na unaondoa hisia yoyote ya kuonekana ana thamani. Kumpuuza mtu ni kumfanya mtu si kitu; anachosema hakina maana, matatizo yake hayana mpango, na malalamiko yake ni ya kijinga. Mfumo unapompuuza mtu unamfanya mtu au raia ajihisi ameondolewa thamani.Wakoloni walifanikiwa sana katika kumpuuza mtu mweusi; walimpuuza kiasi kwamba athari zake zilibakia kwa muda mrefu kwenye fikra za watu wetu. Hata leo hii utakutana na watu ambao wanatafuta kuonekana wana thamani mbele ya wazungu kuliko inavyoweza kuelezeka kiakili. Mkoloni alimfanya mtu wetu duni kwa mifumo aliyomtengenezea na kwa jinsi alivyomhudumia. Kupuuzwa basi ni jambo ambalo mwanadamu hajaumbwa kuishi nalo. Huwezi kumpuuza mwanadamu kwa muda mrefu kabla mwanadamu huyo hajaamua kuasi.Hata watumwa walipuuzwa kwa muda mrefu lakini hatimaye kizazi chao kilikuja kuasi. Sasa kupuuzwa huku katika nchi yetu kunaonekana sana katika mambo mawili makubwa (nitaacha wengine wayaongeze). Kwanza ni katika ubora huduma ambazo serikali inatoa kwa wananchi wake. Ukiangalia vizuri sana utaona kuwa utawala uliopo haujaweka msisitizo katika ubora wa huduma bali wingi wa huduma. Shule, hospitali, barabara, nishati, n.k vyote vipo na vingi vimeongezwa lakini suala la ubora linaudhi. Mkaguzi na Mdhibiti Mkuu katika ripoti zake mbalimbali amekuwa akigusia hili kwa namna moja au nyingine anapolinganisha fedha iliyotumika na ubora wa kitu kilichonunuliwa au kupatikana (value for money comparison). Hili la ubora linaonekana sana kwa kukosekana kwa mifumo mizuri ya Quality Assurance (QA) na hivyo taasisi na ofisi nyingi za serikali kukosa usimamizi mzuri wa huduma wanazotoa.Sasa Watanzania hawataki kuendelea kupuuzwa. Kwani kupuuzwa kunakoudhi zaidi ni kule kwa wao wananchi kuonekana wasumbufu; maswali yao kutupwa pembeni na wanapouliza kujihisi kama wanamuuliza mfalme wa mbinguni. Habari zilizoripotiwa kuhusu Wassira hivi karibuni kwenye jimbo lake kunatudokeza. Siyo mara moja kiongozi wa umma anaposimama kuulizwa maswali anaanza kuonesha kumpuuza mwananchi aliyeuliza swali hilo. Ni nani amesahau jinsi yule mtoto wa shule alivyomuuliza swali Lowassa na kujiletea matatizo? Ni mara ngapi watu wanaogopa kuuliza maswali kwa sababu watu wa ‘usalama' watawaita pembeni na kuwabana? Hadi waandishi wa habari wanaogopa kuuliza maswali wanapokuwa mbele ya watawala na badala yake wanakuja kama kasuku kutuambia alichoongea mkubwa na kuacha maswali yaendelee kuning'inia au wanakimbilia kuandika maswali kwenye tahariri zao badala ya kumuuliza muusika na kumbana atoe majibu. Wanaogopa kupuuzwa!Lakini maelfu wameamua kukataa kuendelea kupuuzwa! Hakuna utawala ulioweza kudumu huku ukipuuza wananachi wake au kundi kubwa la wananchi wake.Sasa hayo manne yote yanapatikana ndani ya azimio la Arusha. La tano hata hivyo naweza kusema ndio linakataliwa zaidi na kizazi cha sasa nalo ni kudanganywa.
5. Tumedanganywa
Watanzania wamechoka kudanganywa na kuahidiwa mambo yasiyoweza kufanyika. Lakini ni kudanganywa kunakofanyika kiutalamu sana na sasa wananchi wamegundua. Sasa kudanganywa kunakofanywa mara nyingi ni kule kunakotelewa na wenye vyao kwa namna ya ahadi. Watawala wanaposhindwa kutoa majibu ya kueleweka wao hutoa ahadi.
Sasa ahadi zinaficha ukweli wa uzembe na kushindwa kwa watawala. Fikiria pembezoni ya makazi ya polisi pale Msimbazi ambapo kwa miaka nenda palikuwa pamerundikana vinyesi na uchafu. Sasa mahali kama hapo unaweza kuuliza nani au kumuuliza mtu nini akakupa jibu la ukweli zaidi ya kutoa ahadi? Kwa mfano ukiendea na kukutana na S/M Selous Namtumbo utashangaa nini ukiona watoto wa darasa la tano wanasoma chini ya paa la majani, hakuna ukuta wala hifadhi nyingine yoyote? mtu akiuliza ‘kwanini' jibu la kiongozi au mtawala litakuwa nini kama siyo ahadi? Sasa wananchi wameshaanza kugundua kuwa ahadi = uongo wa kinamna.
 
watanzania wangapi? mm simo ila nakushauri kuanzia hapa, anza Kampeni zako na 2015 kapige kura kwani kura yako ni moja
 
As much as i don't like CCM....

bado naamini bado ni chama imara hata kama kinapungua nguvu as siku zinavyokwenda

sasa tusiamini sana kuwa CCM 'imekwisha'

safari bado ndefu mno kwa wapinzani....

tusiamini 'this hype'.....ya kuwa CHADEMA sasa mlango uko wazi...
CCM "inanguvu" iliyothibitika kwa vitendo ya "kuchakachua kura". Nakubaliana na wewe kwamba safari ya kelekea Ikulu kwa Chadema katika mazingira tuliopo na kwa katiba hii ndio imeanza
 
Back
Top Bottom