Mamba wawili ‘watoa roho za watu’ wageuzwa kitoweo

Donnie Charlie

JF-Expert Member
Sep 16, 2009
15,159
16,241
Wananchi wa wamegawana nyama ya mamba baada hao kuvunwa huku ikisadikaka kuwa nimiongoni mwa mamba waliowashambulia wananchi wa Kijiji cha Izindabo na kupoteza maisha.

Buchosa: Mamba wawili walioshambulia watu Kijiji cha Izindabo, Kata Lugata Kisiwa cha Kome wilayani Sengerema Mkoa wa Mwanza wamegeuzwa kitoweo na wananchi wa kijiji hicho.

Baadhi ya wananchi wana kijiji hicho wameipongeza serikali kwa kuwagawia kitoweo hicho ambacho kitawa pia afya njema.

Bagoke Richard ni moja wa wananchi waliochuna mamba hao, amesema nyama ya mamba ni lishe tosha na ni tiba moja wapo kwa magonjwa ya binadamu hasa wanaosumbuliwa na magonjwa ya miguu na vidonda vya tumbo.

"Nyama mamba ina faida kubwa ndiyo maana wananchi wanaitamani kuitumia ni tiba pia inarutubisha mwili wa binadamu kiafya,” amesema Magoke.

Wanyama aina ya mamba wamekuwa nitishio kwa wananchi wanaoishi kandokando wa Ziwa Victoria kutokana na kuwashambulia wakati wanapokwenda kuonga na kuteka maji na kufanya shughuri zingine za kibinadamu.

Ofisa Mtendaji Kata ya Lugata ameongoza zoezi la wananchi wa Kijiji cha Izindabo kupata kitoweo hicho Kwa kuzingatia ratibu walizojipangia kila mtu apate anayehitaji.

Mamba hao wamevunwa na maofisa wa Taasisi wa Utafiti Wanyamapori Tanzania (Tawiri) kwa lengo kuokoa maisha ya watu wanaokaa kandokando mwa ziwa Victoria.
 
14c985e9-8d2a-4b31-a3fb-5fbca3730c27.jpg
 
Back
Top Bottom