Mama Mkwe Avuruga Bajeti!!!

Losambo

JF-Expert Member
Nov 8, 2011
2,612
864
JAMAA mmoja baada ya kuwa na hali ngumu aliamua kufunga safari kutoka kwake Mbagala hadi Kinondoni jijini Dar kwa swahiba ili akapate msaada wa fedha apunguze ukali wa maisha.

Katika kutafuta nauli ya kumfikisha Kinondoni alipata elfu moja ikiwa ni nauli ya kwenda na kurudi huku akipiga hesabu mia mbili ya kununulia hata karanga kama anapokwenda atamkosa mwenyeji wake.
Akiwa ndani ya daladala alishtuliwa na sauti ya mama mkwe wake ikimsabahi akiwa na mdogo wa mkewe. Jamaa hakuwa na jinsi ilibidi awalipie nauli ya shilingi mia sita ya kuishia Karume na ya kwake ya kuishia Kinondoni buku likakatika na kumfanya abakiwe mtupu.

Jamaa alipofika Kinondoni alipata pigo lingine baada ya kukuta jamaa yake kasafiri.
Hakuwa na jinsi ilibidi aunge azimio kurudi Mbagala kwa miguu, huku akimlaumu mama mkwe kumharibu bajeti yake.

Kwa habari na vichekesho mix vingine bofya http://www.globalpublishers.info/profiles/blogs/vituko-mix-1
 
Kwani ilikua ni lazima awalipie?au ndo kujikomba ukweni teh teh
 
Kwani wakati wanapanda gari walitengemea watamkuta humo. Hayo ni maamuzi yasiyokuwa na mtazamo wa mbele
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom