Mama Maria: Kuilipa Dowans tatizo kubwa

Dowans italipwa bilioni94,umeme wa mgao utaendelea mpaka july 2011,matumizi ya msingi yatapunguzwa serikalini e.g dawa za maleria ,vitabu mashuleni ,huduma kwa wazee,walemavu kukosa pesa kabisa
Mashangingi i.e landcruisers V8 yatazidi kununuliwa,Safari za nje kutafuta wafadhili-wanunuzi wa rasilimali ,AKA wawekezaji kuongezeka
Kiwango cha elimu kitazidi kushuka kwa kuwa mishahara ya walimu haitopanda na walimu kundelea kusoma ili kubadili career ,tayari walimu wengi wakishapata degree zao hawarudi kufundisha ktk shule walizotoka,hivyo tutakuwa na walimu wa short courses ,temporary without anycomitment to teaching as a career
Bei ya mafuta itazidi kupanda,Gas yetu itauzwa soko la nje -kuibiwa juu kwa juu.
Mh.J.K kazi yake itazidi kuwa ngumu,kwani mpaka sasa hajaweza kuteua wakuu wa mikoa,wilaya,wakurugenzi.
Katiba haitojadiliwa Tena,itaundwa tume na hiyo tume itasimamiwa na watu wale wale.....
Ahadi za CCM zitakuwa ngumu kutekeleza kwani watumishi wengi wa umma hawana moyo wala imani na viongozi walioteuliwa.

Tutalikumbuka Azimio La Arusha,hasa kuhusu maadili ya uongozi,viongozi na familia zao.
2015 CCM Kushika hatamu tena Raisi akiwa na Asilia ya Somalia-Iran

2rg2owh.gif
 
Duuu mzee, umejitolea kazi ya shekhe yahaya!! Lakini nahisi hali itakuwa mbaya zaidi ya ulivyoeleza. Tuombe Mungu.
 
Du Mzee utabiri wako komesha hata Raisi ajae umeshamjua huu upepo wa Misri utakuwa haujafika kwetu kweli.
Ahadi za CCM zitakuwa ngumu kutekeleza kwani watumishi wengi wa umma hawana moyo wala imani na viongozi walioteuliwa.
Tutalikumbuka Azimio La Arusha,hasa kuhusu maadili ya uongozi,viongozi na familia zao.
2015 CCM Kushika hatamu tena Raisi akiwa na Asilia ya Somalia-Iran
 
Hakuna chochote kitafanyika kuhusu Dowans na kama CCM wanataka kuvunja na kuleta visu mitaani, waache walipe....Yes Watanzania Tumetoa Tamko Rasmi.
 
Dowans italipwa bilioni94,umeme wa mgao utaendelea mpaka july 2011,matumizi ya msingi yatapunguzwa serikalini e.g dawa za maleria ,vitabu mashuleni ,huduma kwa wazee,walemavu kukosa pesa kabisa
Mashangingi i.e landcruisers V8 yatazidi kununuliwa,Safari za nje kutafuta wafadhili-wanunuzi wa rasilimali ,AKA wawekezaji kuongezeka
Kiwango cha elimu kitazidi kushuka kwa kuwa mishahara ya walimu haitopanda na walimu kundelea kusoma ili kubadili career ,tayari walimu wengi wakishapata degree zao hawarudi kufundisha ktk shule walizotoka,hivyo tutakuwa na walimu wa short courses ,temporary without anycomitment to teaching as a career
Bei ya mafuta itazidi kupanda,Gas yetu itauzwa soko la nje -kuibiwa juu kwa juu.
Mh.J.K kazi yake itazidi kuwa ngumu,kwani mpaka sasa hajaweza kuteua wakuu wa mikoa,wilaya,wakurugenzi.
Katiba haitojadiliwa Tena,itaundwa tume na hiyo tume itasimamiwa na watu wale wale.....
Ahadi za CCM zitakuwa ngumu kutekeleza kwani watumishi wengi wa umma hawana moyo wala imani na viongozi walioteuliwa.

Tutalikumbuka Azimio La Arusha,hasa kuhusu maadili ya uongozi,viongozi na familia zao.
2015 CCM Kushika hatamu tena Raisi akiwa na Asilia ya Somalia-Iran

Hata kule Tunisia na Egypt Viongozi wa serikali walidhani ni Business as Usual matokeo yake wote tunayaona.
So la kuiondoa CCM itaanza kaa utani kabisa katikati ya kundi la watu waliodharauliwa.
 
Wassira: Msimshinikize JK azungumzie Dowans

Imeandikwa na Christopher Maregesi, Bunda; Tarehe: 1st February 2011 @ 08:48

WATANZANIA wametakiwa kuacha kumshinikiza Rais Jakaya Kikwete atoe kauli ya Serikali juu ya sakata la Kampuni ya kufua umeme ya Dowans na badala yake ashughulikie masuala mengine ya maendeleo.

Mwito huo umetolewa na Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais – Uhusiano na Uratibu, Stephen Wasira ambaye amesema suala hilo hivi sasa liko mahakamani hivyo haitakuwa vyema kama shinikizo hilo litaendelea.

Akijibu moja ya maswali aliyoulizwa kwenye mkutano wa hadhara juzi kwenye eneo la stendi ya zamani mjini hapa, Wasira ambaye pia ni Mbunge wa Bunda, alisema maadam sakata hilo limeshahukumiwa kisheria, basi ni vyema kuliacha mikononi mwa vyombo vya sheria kuliko kung’ang’ania kauli ya Rais.

“Tumwache Rais ashughulike na mambo mengine makubwa ya kitaifa kuliko kumng’ang’ania atoe kauli juu ya sakata la Dowans, ambalo limeshahukumiwa na Mahakama,” alisema Wasira.

Kwa mujibu wa Wasira, Rais Kikwete hawezi kutoa tamko lolote kuhusu uamuzi wa Mahakama wa kuitaka Serikali iilipe fidia kampuni hiyo Sh bilioni 94 kwa kuwa Tanzania inaheshimu na kutekeleza utawala wa sheria, hali inayoifanya kuheshimiwa kote duniani na kwamba kama ni kupinga hukumu hiyo, Serikali itakata rufaa.

Kuhusu kutoilipa au kuilipa kampuni hiyo fidia, Wasira alisema japo inamwumiza kila Mtanzania akiwamo Rais mwenyewe, lakini haina budi kutekelezwa kama ilivyoamuliwa na Mahakama ingawa alisema mchakato wa kupinga hukumu hiyo umeshaanzishwa na jopo la wanasheria ingawa hakusema ulipofikia.

Awali katika swali lake mkazi wa hapa, Asetic Malagira alimtaka Wasira kuwambia wapiga kura wake sababu zinazomzuia Rais kutoa tamko kuhusu Dowans kwa kipindi chote cha mjadala huo na kama ni halali kwa Serikali kuilipa fidia kampuni hiyo.

Wakati huo huo, Wasira amewataka vijana nchini kujiunga katika vikundi vya kuzalisha mali, ili wasaidiwe mitaji.

Amesema vikundi hivyo vitawasaidia waondokane na umasikini na kuacha kutumiwa na wanasiasa kwenye maandamano yasiyo na maana kwa kulipwa ujira mdogo.

Alisema ni azma ya Serikali kuwawezesha vijana kuinuka kiuchumi kwa kupewa mitaji ili wajiajiri, jambo alilosema halitatekelezwa kirahisi kama vijana hao hawatajiunga katika vikundi vya uzalishaji mali.

PHP:
WATANZANIA wametakiwa kuacha kumshinikiza Rais Jakaya Kikwete atoe kauli ya Serikali juu ya sakata la Kampuni ya kufua umeme ya Dowans na badala yake ashughulikie masuala mengine ya maendeleo. 
 
Mwito huo umetolewa na Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais – Uhusiano na Uratibu, Stephen Wasira ambaye amesema suala hilo hivi sasa liko mahakamani hivyo haitakuwa vyema kama shinikizo hilo litaendelea. 
 
Akijibu moja ya maswali aliyoulizwa kwenye mkutano wa hadhara juzi kwenye eneo la stendi ya zamani mjini hapa, Wasira ambaye pia ni Mbunge wa Bunda, alisema maadam sakata hilo limeshahukumiwa kisheria, basi ni vyema kuliacha mikononi mwa vyombo vya sheria kuliko kung'ang'ania kauli ya Rais. 
 
"Tumwache Rais ashughulike na mambo mengine makubwa ya kitaifa kuliko kumng'ang'ania atoe kauli juu ya sakata la Dowans, ambalo limeshahukumiwa na Mahakama," alisema Wasira.

Utata kwa unakuja hiyo hukumu imeenda kusajiliwa tu siyo kuchunguzwa sasa huu utetezi wa JK unatoka wapi? Baada ya hukumu JK atasema hana la kufanya ila kutekeleza maamuzi ya kimahakama..........................hizo chenga hawajui ya kuwa hata sisi tunazifahamu?

Kuhusu tumwache JK ashughulikie mambo makubwa hivi kuna ubadhilifu wa zaidi ya Tshs 94 bilioni siyo jambo kubwa?
 
Lukuvi naye alisema hii ni ''petty issue''
 
mbona richmond aliiongelea,EPA aliiongelea pia..,,DOWANS anaogopa kuiongelea sababu na yeye ana mgao wake
 
Kama yeye hataki kuzungumza, basi wanaotaka kuzungumza kama akina Sitta wasitishwe, waachwe waseme
 
kuhusu swala la vijana sijaona uhusiano kati ya ajira na kushiriki maandamano. naona jamaa anamtumikia kafiri.
 
Kutoa rushwa ya sh bilioni 94 kwa mafisadi wachache walioko sisiem ni kitu kidogo sana, tumwache rais aongelee mambo makubwa kama vyandarua vya bush, kuzindua visima vya maji, kusafiri nje ya nchi etc etc, huo ndiyo uongozi wa Tz!! lol!!:msela:
 
mbona richmond aliiongelea,EPA aliiongelea pia..,,DOWANS anaogopa kuiongelea sababu na yeye ana mgao wake

Tusipoangalia tutaendelea kuongea mambo ambayo hatuna ushahidi nayo na watu wa aina hii mara nyingi kwa wale wanaojua makundi mbalimbali ya watu tutajua tunawekwa kundi gani! Nani ana ushahidi kuwa Przd ana share DOWANS? jamani tukumbuke kuwa deep thinker anachukua muda kuhukumu pia.
 
...kama ni kupinga hukumu hiyo, Serikali itakata rufaa. Hivi huyu Wassira anayaongea haya wakati werema alishasema kwamba serikali haitakata rufaa, sasa hiyo rufaa itakatwa kupitia kwa nani!
 
Ungemwangalia kwenye TV jana ni kama vile alikuwa anagombana na anaowahutubia. Walimpa maneno makali sana baba wa watu na sura yake ile!
 
Tusipoangalia tutaendelea kuongea mambo ambayo hatuna ushahidi nayo na watu wa aina hii mara nyingi kwa wale wanaojua makundi mbalimbali ya watu tutajua tunawekwa kundi gani! Nani ana ushahidi kuwa Przd ana share DOWANS? jamani tukumbuke kuwa deep thinker anachukua muda kuhukumu pia.

Kwa hili naomba kupingana na wewe.

Taifa liko njia panda juu ya Dowans, hakuna siku inapita hujasikia Dowans.
Hiyo ni kusema swala hili linagusa masilahi ya wananchi wengi. Ni kiongozi asiyemahiri tu ndio atatumia miezi miwili (Nov 15, 2010 - Ja 2011) kwa kisingizio cha deep thinking. Mbona minofu ya sangara alizungumzia tena kwa ukali kule mwanza??

Nitajie mwanasiasa asiyependa ku-seize opportunity ianyoweza kumpandisha chart, kwa nini anaogopa kutumia opportunity hii??

The machinery under him allows the president to be abreast of every key issue happening nchini. Sasa kimya chake kinatuambia kwamba ana hofu ya kuzungumzia swala lililo ndani ya ikulu yake.

Hata asipoongea tena we have drawn our conclusion kwamba anahusika ama kimasilahi au vile serikali yake ilivyoileta Dowans
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom