Mama Kikwete Uso Kwa Uso Na People's Power

MtamaMchungu

JF-Expert Member
Apr 10, 2011
8,345
11,227
Mke wa Rais, Mama Salma Kikwete, juzi alipigwa na butwaa baada ya baadhi ya wanafunzi wa Shule ya Msingi Ushashi iliyopo wilayani Bunda mkoani Mara, kumsalimia kwa kumuonyeshea ishara ya vidole viwili. Mama Kikwete alikuwa mgeni rasmi katika hafla ya kukabidhi vyumba vitatu vya madarasa na ofisi mbili za walimu na
jengo moja vilivyojengwa na kukarabatiwa kwa
msaada wa Kampuni ya Saruji ya Twiga kwa kushirikiana na Mwanza Huduma Limited.

Baada ya kukata utepe
kama ishara ya kuzindua majengo hayo, Mama Kikwete, alikagua madarasa hayo mapya pamoja na ofisi za walimu kabla ya kukutana na
wanafunzi 30
waliotengwa rasmi
kukabidhiwa mabegi ya shule na mgeni rasmi huyo.
Na alipofika mbele ya
wanafunzi hao, Mama
Kikwete, alinyoosha
mkono juu kuwasalimia wanafunzi hao, lakini
wengi wao walimjibu kwa kumuonyesha ishara ya vidole viwili, kitu ambacho
kilimshangaza na kusema: “Huu sio utaratibu.” Na kisha akawauliza: Je; walimu wenu wanawafundisha hivyo?. Hata hivyo, wanafunzi karibu wote walikaa kimya, lakini mmoja wao bila woga alijibu“Ndiyo” na kumfanya Mama
Kikwete kumgeukia Mkuu wa Wilaya ya Bunda, Francis Isack na viongozi wengine na kuwaambia:
“Inaelekea watoto hao ndivyo mnavyowafudisha.”
Baada ya kukemea
kitendo hicho, Mama
Kikwete aliendelea na
zoezi lake la kuwagawia wanafunzi hao mabegi ya shule kabla ya kwenda katika jukwaa la wageni
lililoandaliwa maalum
kwa ajili yake na msafara wake. Salamu ya kuonyesha vidole viwili mara nyingi hutumiwa na Chama upinzani cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema).
Kampuni ya Twiga Simenti ilijenga madarasa matatu
na ofisi za walimu na
kulifanyia ukarabati jengo moja, ambapo walitumia jumla ya Sh. milioni 90.
Sherehe hizo za kukabidhi vyumba hivyo vya madarasa, zilionekana kama ni za Chama cha Mapinduzi (CCM), baada ya nyimbo zilizokuwa zikipigwa ni zile za chama hicho, huku akina mama wengi wakiwa wamevalia fulana na khanga za CCM pia.

CHANZO: NIPASHE
 
Na yule mama uwezo wake wa kuelewa mambo ni mdogo .Maana anaota mchana anadhani CCM wana own Watanzania na hatta hajui kwamba watu wana uhuru .Najua aliumia sana kama alivyo umia kule Tunduma last time .Ndipo akome kuzurura
 
kama kweli akwenda ki siasa mbona alipatwa mshangao na salam za vidole viwili, kila mtu anahaki ya kufanya anachokitaka ila asivunje sheria. kwani kunasheria ya salam? Mama iyo ndiyo Tanzania ya leo.
 
Kwa hiyo ni sahihi kuimba nyimbo za ccm lakini ni haramu kuonesha alama ya chadema. Well, a taste a things to come Madam so you better get used to it....
 
Ningekuwa mimi ndio mkuu wa wilaya naulizwa swali la kijinga hivyo kuwa inaelekea ndio mnavyowafundisha ningesema NDIO, yaani huyu mama ana cheo gani kwani? si alikua mwalimu huyu jamani? kwa hio mwanafunzi aki-misbehave ndio mwalimu amemfundisha? Pumbafu kabisa, hivi na yeye wakati ni mwalimu, wanafunzi waki-misbehave ndivyo alivyowafundisha? ina maana nae aliwafundisha watoto wetu hivyo????
 
Nitampeleka Diploma ya Ualimu japo alishafeli mara kibao
 
Na yule mama uwezo wake wa kuelewa mambo ni mdogo .Maana anaota mchana anadhani CCM wana own Watanzania na hatta hajui kwamba watu wana uhuru .Najua aliumia sana kama alivyo umia kule Tunduma last time .Ndipo akome kuzurura


Uelewa wake waweza kua mdogo but hio ni kusoma kuzingatia alama za nyakati...
 
Back
Top Bottom