Mama anamtetea mke wangu pamoja na kunisaliti

dawa nyepesi sana ondoka wewe kaanze maisha kwingine mbona simple like that mkuu..... weka miakakati namana ya kullipia watoto ada na matunzo yote.. acheni ubinafsi vikojoleo vyenu vinawaumiza watoto embu wapeni watoto relief hata kidogo jamani.. baba analala na mwanamke mwingine mama analala na wanaume mwingine kweli? mnafundisha nini hawa malaika? embu we mwanume kuwa mwanaume ondoka hapo kama ni swala la hati ya nyumba transfer kwenye majina ya watoto that all .... usiwaze kwamaba unampa faida mama waza kuwa watoto wako wanahitaji malezi mema .. kama ni wasi wasi wa mkeo kuja kutiwa ndani kwako kashatiwa hata kwabla ujamwacha.......

kuwaacha watoto kwa dada yako eti kisa nyie mnashindana kugongana kwenye nyumba yeni ni upuuzi tena upuuzi mkubwa
Chukua huu ushauri aisee
 
Duh mwanaume mfanyie yote ila uzinzi noma hata akikusamehe IPO siku tu mi nalielewa hilo na wanawake mlio kwenye ndoa jitahidi sana kama huwez kuishi bila yeye usidhubutu.......kaka Fanya kinachokupa Amani,ila kwenye maamzi yako kumbuka watoto
Wazo la kuwapeleka watoto boarding liko poa na kuhusu kuoa mwanamke mwingine MTU asikutishe unaweza pata mwanamke safi tu kuliko kuishi bila Amani.
 
Ulikosea approach tangu mwanzo. Alivyoletwa na wazazi, kesho yake tu ungebeba watoto na kuwapeleka kwenye usalama then ungeondoka ukawaachia nyumba na usionekane tena. Hizo za kumletea mwanamke umemshajiweka kwenye kundi lake maana kama kuzini ameshamuonyesha kuwa nawe umezini. Either ondoka umuachie nyumba au baki usamehe maisha yaendelee.
 
Urafiki na mahusiano yangu hapana. Kuja kwangu bila ridhaa yangu ni kosa kubwa ambalo halisameheki popote pale.
Urafiki mwisho kanisani, kazini kwangu marufuku
 
Kwanza ninakupa pole sana kwa yaliyokukuta. Ninajua maumivu yake. Ninashauri umsamehe na kumpa masharti maana unakoelekea siyo kuzuri. Looks like you are totally confused. For the sake of the children and yourself msamehe tu brother maana ukifikria kuoa tena utaweza kumpata ambaye ni mbaya kuliko huyo uliyenaye. Kama ninyi ni wakristo nendeni mkamwone mchungaji wenu f kwa ajili ya kupewa ushauri. Ninashauri tena ninaomba umsamehe na anaweza kuwa mke mzuri sana hapo baadaye.
 
Wakuu habari zenu

Mwaka 2012 nilienda kozi nje ya nchi kwa miezi 3 hapa hapa Africa, nyuma niliacha mke na watoto wawili walio primary school
Nikiwa kozi rafiki yangu akawa anakwenda kulala kwangu mara kwa mara especially weekends, akawa analala chumbani kwangu, haijajulikana hadi leo walianza lini uhusiano huo, alikua akienda kwangu kwa gia ya kuwaona wanaendeleaje

Niliporudi, nikakuta wife kamtimua kazi house girl wetu bila maelezo ya kueleweka, nikapuuzia, baadae rafiki kipenzi wa wife wa tangu shule na ambae wanasali jumuia moja maana amepanga mitaa yetu, akaniambia kwa urefu uhusiano wa wife na mshikaji wangu, ila kwa sharti la kutomtaja whatsoever the case, baadae nikaona niende kumtafuta yule hg aliefukuzwa kazi na wife nikampata, aka confirm habari zile na kunieleza kwa kirefu na ndio kisa cha yy kufukuzwa kazi pale kwangu baada ya kumuhoji kuwa "" kwa nn unamfanyia shemeji matendo haya

Baada ya kujiridhisha nikamuita wife mbele ya wazazi wake na kueleza kila kitu akabaki kimya akilia, nikamkabidhisha kwa wazee wake hapo hapo, akiwa kwao aliendelea kunibembeleza na kuniomba msamaha kwa kutuma watu mbali mbali wenye heshima, sikurudi nyuma, akasafiri kijijini kwetu kuwaona wazazi wangu na kuwaangukia, alikaa huko mwezi mzima

Baadae wakaja wote na wazazi wangu hadi kwangu, wakasema pamoja na yote yaliyotokea niishi nae hivyo ametubu, sio ombi ni amri ndio maana wamemleta wao, moyoni nikasema najua cha kufanya, nilishindwa kuwaelewa, wanamtetea mtu ambae ameniumiza despite kuwa nilimuachia kadi ya benki awe anachukua mshahara wangu kuendesha familia, mm kule kozi nikawa naishi kwa chakula cha kulipiwa na posho kidogo tu

Wazazi walipoondoka tu, nikaanza kumfanyia visa na matendo mabaya ili aondoke, nikatafuta msichana wangu nikawa najiachia nae pale mtaani bila woga, nakunywa nae bar za mtaani, nikaanza kuja nae home nalala nae chumba kingine, akawa anatufanyia fujo lakini namdhibiti kiume hadi tunajifungia chumbani, nilikua nafanya haya yote ili wife aondoke lakini wapi, yupo tu, anawapigia simu wazazi kushitaki wakinipigia nawaambia huyu ni mke wenu mm nilimtimua nyinyi mkamleta tena, ni mke wenu

Tumeishi kwa hali hii tangu 2012 hadi sasa, yule msichana wangu akachoka hizi vurugu akaamua kuniacha, sasa nina mwingine, sina uhakika kama yupo mwanamke huko nje angeweza kuvumilia matendo niliyomtendea huyu wife, lengo ni aondoke lakini hataki kuondoka hata baada ya kumu offer kugawana mali, watoto wameathirika sana na hizi vurugu huwa nikiwapeleka kwa dada yangu wanakataa kurudi

Lakini yote haya aliyasababisha yy kwa tamaa, nilishamueleza tangu siku ya ndoa kanisani kuwa nitakusamehe yote lakini uzinzi huwa sisamehi, sijamgusa tangu 2012,

Wadau naombeni ushauri nimtoe vipi huyu mwanamke?
Au mnadhani ipo siku naweza kusahau usaliti wake na kumpenda?

Na kama ni kumuacha ndani tutaishi hivi hadi lini?

Kuhusu watoto mnaonaje niwaache uko uko kwa dada yangu walelewe huko wasomee huko huko? Maana tangu likizo ya December wamekatalia huko hivyo school bus huwa linawafuata huko badala ya kwangu

Nitaheshimu mawazo yenu as my last resort
waonee huruma hao watoto wa shule ya msingi..,.kama wasingekua watoto ungemwachia nyumba then unafanya yako
 
Ondoka wewe tafuta nyumba hamisha watoto mkaishi kwingine huyo mwache abaki mwenyewe hapo!! akiwafuata mpaka makazi mapya kamshitaki
 
dawa nyepesi sana ondoka wewe kaanze maisha kwingine mbona simple like that mkuu..... weka miakakati namana ya kullipia watoto ada na matunzo yote.. acheni ubinafsi vikojoleo vyenu vinawaumiza watoto embu wapeni watoto relief hata kidogo jamani.. baba analala na mwanamke mwingine mama analala na wanaume mwingine kweli? mnafundisha nini hawa malaika? embu we mwanume kuwa mwanaume ondoka hapo kama ni swala la hati ya nyumba transfer kwenye majina ya watoto that all .... usiwaze kwamaba unampa faida mama waza kuwa watoto wako wanahitaji malezi mema .. kama ni wasi wasi wa mkeo kuja kutiwa ndani kwako kashatiwa hata kwabla ujamwacha.......

kuwaacha watoto kwa dada yako eti kisa nyie mnashindana kugongana kwenye nyumba yeni ni upuuzi tena upuuzi mkubwa

!
!
Yes mkuu. Yeye ndio wa kuondoka hapo aisee
 
Msalala Kwetu:

Kama Hukuwahi kucheat huko masomoni ni vizuri sana.

Kama tangu uoe hujawahi kucheat ni vizuri zaidi.

Lakini kama ulishawahi kulala na mwanamke mwingine kwenye ndoa ( ambapo tayari) ahh kaka msamehe. Kpimo hicho hicho unachompimia na wewe jipimie.

Unawapa watoto tabu bure, unampa dada yako tabu bure kukaa na wanao.

Tulizana. yaache maisha yaendelee. Wewe sio malaika.
 
kama ametubu na kujutia kosa lake, huna budi kumsamehe for the sake of your children. Akija mama mwingine anaweza akakuvuruga kuliko huyo.
hii isikie kwa mwingne lakn ikiwa yako ni ngumu kumesa.

Si jambo rahisi kumsamehe mzinzi
 
Namshangaa tu huyo mke..tangu 2012 hujamgusa na bado yupo? Kweli ana moyo wa ajabu..ningetamani aniazime huo moyo wake. Usiponigusa mwezi tena kitanda kimoja..bila sababu yoyote ya ugonjwa, kutakuwa hakuna ndoa kwasababu maana ya ndoa kwangu ni tendo la ndoa.
Kama alivyokushauri Miss chagga...ondoka wewe mwachie watoto hapo lakini hakikisha unawahudumia watoto wako kwa kila kitu ili wasiteseke. Siku moyo wako ukipenda kumsamehe rudi kwa mkeo. Maisha mnayoishi hapo ni maigizo, mnawaumiza sana watoto na pia mnajiumiza na nyie vile vile.
 
Kama vp mpishe uanzishe maisha mapya kimya kimya.
We uko kama mimi yani ukinisaliti nikiondoka huwa sigeuki nyuma, big up sana
 
Kwanza ninakupa pole sana kwa yaliyokukuta. Ninajua maumivu yake. Ninashauri umsamehe na kumpa masharti maana unakoelekea siyo kuzuri. Looks like you are totally confused. For the sake of the children and yourself msamehe tu brother maana ukifikria kuoa tena utaweza kumpata ambaye ni mbaya kuliko huyo uliyenaye. Kama ninyi ni wakristo nendeni mkamwone mchungaji wenu f kwa ajili ya kupewa ushauri. Ninashauri tena ninaomba umsamehe na anaweza kuwa mke mzuri sana hapo baadaye.
Chief nashukuru kwa mawazo yako

Nilipona maumivu siku nyingi, usaliti ulifanyika 2012, hivyo nilisha move on, tatizo ni mwanamke kukatalia kwangu, mengine nilishayasahau
Na suala la msamaha halipo, msamaha kama binadam nilishasamehe, ila mapenzi ndio haiwezekani, sina upendo nae tena

Siwezi kuishi bila furaha kwa maisha yangu yaliyobaki duniani kisa watoto, ndio fate hiyo, cha msingi ni wapate elimu na wakae sehemu salama wakipata huduma zote
Watabaki kwa dada yangu wakilelewa hapo na kupata huduma zote
 
Kweli nakuunga mkono ni kitu kakutia aibu huyo mwanamke.
Move on
 
Ondoka wewe tafuta nyumba hamisha watoto mkaishi kwingine huyo mwache abaki mwenyewe hapo!! akiwafuata mpaka makazi mapya kamshitaki
Mama, nimeupokea ushauri wako kwa mikono miwili, umeongeza kitu kikubwa sana,
Nipo tayari kumuachia nyymba ss tutaanza upya
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom