Mama anamtetea mke wangu pamoja na kunisaliti

Ongea naye tena,fanya uchunguzi kuwa kipindi chote hicho mlichotengana naye hajawahi kuwa na mpenzi mwingine tena...pimeni afya then mjenge familia.Samehe kama yupo tayari kuwa muaminifu,hakika naamini hatarudia tena ila ukioa mwingine anaweza akakutenda vivyo hivyo ukaona labda mama fulani asingerudia haya.Jipe moyo na mrudie mke wako
 
Hata hao watoto hawatakupenda tu subiri utajaona kitendo cha wewe kuleta mwanamke hapo ndani huku mama yao yupo uliharibu.hebu roho mtakatifu akupe Neema ili uweze msamehe mkeo inatosha kwahayo mliyoyafanya ili mtunze familia yenu vyema.Hebu nikuulize toka umemwoa huyo mkeo ulikua hujawahi kumcheat hata siku moja kabla la hilo songombingo? Kama ulishawahi mcheat haijarishi ni mazingira gani Samehe mkuu,kama hujawahi kabisa kabisa na Mungu wako ndo anajua waweza kufanya walichoshauri baadhi uondoke hapo kajianzie maisha mapya Ila usifikiri ukioa huyo mke mpya ndo atakua perfect ni vile hujui tu anaweza nae akakucheat tu vilevile ili hali mnaishi wote je naye utamwacha? Je utaacha wangapi?
 
Yaaani wee mwanaume ndio bongee ya mpumbavu na ukumbuki andiko la enyi wazazi watiini watoto wenu na wanaume aishi na mke wake kwa akili. Ukihama hiyo nyumba roho inakuuma kumuacha wkt ni haki ya wanawe kuwalea na kuwarithishia hapo. Embu amka usingzini... na unamoyo kbsaaa mbwle ya wanao unaleta malaya na kumfanyia fujo walipo wanao! how deeea uua?
 
Hapo ndio tatizo la wanawake linapokuja anapigwa miti akitaka kuachwa anaaanza kulialia afu huwa wanasahau mchepuko sio muuoaji so kote anaachwa akiangalia umri umeenda na anawatoto inabidi arudi kwa aliyemsaliti ili akomae maana yeye ndio security yake aliyebaki, hapo usitegemee kuwaataondoka hata siku moja ataanzaje maisha na hasa kama ni mama wa nyumbani keshazoea vya kunyonga vya kuchinja kazi. We chapa lapa ila nawaonea huruma sana hao watoto mistake ya mama yao itabidi waishi nayo maana hakuna namna tena.
 
Nitaheshimu mawazo yenu as my last resort

I like the promise of respect toward our comments. Believe me I understand the pain you feel. Hata ungelala na wanawake 1000 mbele yake, it still happened (Your wife slept with your friend). Truth is, it hurts her as well that you sleep with other women. Kaumia same as you and even more. Please stop digging the hole? (If u ever find urself in a hole stop digging is the first solution).
Time will pass and this will go away. Mkeo hatakufanyia hivyo tena for the fear of what happened. Utakuwa na mke anayekuheshimu. Mtalea watoto vizuri nao tena kwa experience madhara ya kuchepuka, I hope watajifufunza huko ukubwani.

Brother ni wanawake wachache sana hawatachepuka kwenye mazingira kama hayo ya safari (and if u try to be honest, maybe na wewe kule ulichepuka). Utaoa mwingine na mambo hayo yatatokea. Nikwambie kitu? It will be hard kumfukuza huyu mwingine, coz utahisi jamii itakujudge una tatizo, kwanini we uwe wa kufukuza wanawake tu?
Hizi mambo ni aibu brother. Just make it with your wife, nothing else will be better for you, your wife na watoto. Umeumia ndio ila huko mwenyewe asilimia kubwa ya wanandoa wameumia. We msamehe tu, usione wazazi hawana uchungu na wewe mtoto wao kwa kukuambia umrudie. Its because they've lived long, they have seen these things, they know better....
 
msamehe Kwa sababu umemnyoosha vya kutosha sanaa hata hivi n mvumilivu sana hyo mke, Hata ukisema Uoe mwngine yatakuwa n Yale Yale tena kama ni mkristo hutaoa mwingine maana dini hairuhusu

Kumbuka usiposamehe Hata Mungu hawezi kukusamehe dhambi zako pia
 
Umeomba ushauri na ndio huu: SAMEHE 7X70. Kwani hao wasichana unaotembea nao ni wewe ndio wa kwanza kwao kuwa nao? Ok, labda kama wewe ndio ulikuwa wa kwanza kwa mkeo lakini kumbuka wanaume wengi duniani tunaoa wake waliokuwa wa watu. Sasa hicho kinyaa kinatoka wapi wewe. Cha msingi mkacheki afya na mtubu dhambi ili Mungu awasamehe kwa uzinzi wenu. Huyo ashajuta kilichobaki ni ww kufungua tena moyo.
Kumbuka mtaachia hiyo laana watoto zenu. Halafu eti unadai ulimwaachia kadi ya benki kwa ajili ya matumizi sijui nini nini...! Really..! Are you serious, come on! Hii kitu ni tofauti jamaa angu.
 
Mungu aliye juu akupe Neema yakumsamehe mkeo ili mjenge familia yatosha mliyoyafanya maana nawe umelipa kisasi ili hali kisasi ni juu ya Mungu tu.
Watoto wameshuhudia mengi si kwa mama hata wewe baba ambapo wewe ndo ungesimama imara kuilinda heshima ya nyumba badala Yake ikawa kinyume kabisa baba kuleta wanawake Nyumbani nakusababisha ugomvi hii lazima itajenga chuki kati ya watoto na wewe baadae utajaona.
Kama katika maisha yako hujawahi kumcheat mkeo waweza kumwacha Ila kama ilishatokea kumcheat msamehe. huwezi jua pengine hata mama yako Labda alipitia situation hii Ila kwa busara ya baba yako akasamehe pengine ndo maana wanaomba umsamahe.
Palipo na migogoro na magomvi hata maendeleo hudumaa baraka Mungu huzifunga hebu jaribuni mmalize uone atakavyokua mke mwema hutoamini.usifikiri kuoa mwingine ndo atakua umeoa malaika nae ni Binadamu anaweza kukucheat ili hali mnaishi wote je naye utamwacha? Utaacha wangapi?
Mama ni mama tu ukioa huyo hatakua na Upendo kwa wanao kama alionao huyo mkeo haijarishi alivyoanguka dhambini haiondoi thamani Yake kwa wanao.Roho mtakatifu aponye jeraha moyoni mwako na mmrudie mkeo.
 
Msamehe Bwana ,hakuna akiyekamilika.....kosa si kosa bali kurudia kosa ila hata kama umeshamsamehe mara ngpi usiache kumsamehe tena mbona Mungu anatusamehe na kusahau,na bdo anaendelea kuwa mwema kwetu?!



Ni kwasababu Upendo husamehe,give her another chance plz,alfu anayeumia hapo ni wewe mwenyewe ni kama umeshikilia kaa la moto kumwunguza mtu,anayeumia zaidi ni yule aliyeshika kaa who is you now,msamehe maisha yaendelee


Tena Mungu amewarehemu kawaacha hai hadi Leo ni ili mmalize tofauti zenu,forgive her plz,Mungu akutie nguvu,na kama itatokea ukakumbuka mabaya yake u just pray for her and love her even more.
 
kwa sisi waislamu MWENYEZIMUNGU ameahalalisha talaka lkn huchukia kuona wanandoa wawili wameachana kwa 7bu za kidunia lkn linapokuja swala la uasherati ameridhia

adhabu ya mwinzi ni kukatwa kiganja cha mkono lkn mwenyezimungu ametuhusia tusamehe wanaotukosea
hii inamaana ukimkamata mwinzi aliyekuibia ukamkata kiganja cha mkono utakuwa umetekeleza kauri ALLAH mfano utapata thawabu kumi lkn km utamsamehe huyo mwinzi utapata thawabu maradufu na utakuwa umemjengea mwinzi tabia mpya ya kuwa mtu mwema kwa maana ataamini nafsn mwake

tukirudi kwa mkewako wazazi hawana daraja mbele ya kauri ya ALLAH isipokuwa tunatakiwa tuwakatilie kwa kauri njema na si kuwalidhisha araf tukawa tunamkosea mungu hapo ulipo umemkosea sana mungu wako 7bu unazini ndani ya nyumba yako iliyopo familia yako

nini cha kufanya adhabu uliyompa imemtosha sasa amejifunza km humpendi una mapenzi nae usimuonee haya mkimbie mwache peke yake ndani ya nyumba umuandikie talaka kuwa umemuacha mbele ya mashaidi

ila km unahisi unampenda na unamuonea huruma tengeneza kitu moyoni kuwa umemsamehe then shilikiana naye kitandani na nendeni mkaanze maisha eneo jingine mbali na hapo kisha warudisheni watoto wenu na waone kuwa mmebadilika nuru mpya itaibuka nyumbani kwenu fulaha italejea shetani kutibua fulaha ndani ya nyumba na kuleta huzuni

nb. nilichogundua mpk mkeo akakusaliti ni kitendo cha wewe kumuamini na kumpenda kupita kiasi akahisi huwezi fanya lolote na hili ndio tatizo la wanawake wengi pindi unapoonyesha kumjali kupita maelezo


MSAMEHE
 
Temporary separation is a medicine.
15 years can change everything.
Mwache na tengana naye angalau miaka 15 hivi. Akiweza kutubu baada ya miaka 15 basi atakuwa amemaanisha kuwa yeye ni mkeo, vinginevyo ni maigizo.
 
Msamehe Bwana ,hakuna akiyekamilika.....kosa si kosa bali kurudia kosa ila hata kama umeshamsamehe mara ngpi usiache kumsamehe tena mbona Mungu anatusamehe na kusahau,na bdo anaendelea kuwa mwema kwetu?!

FORGIVNESS ....hiyo ni POWER pekee ndo itakayo kupa Amani ya maisha ktk uhai wako !!
msalala kwetu tumia mbinu hii.... Ya kusamehe !! Vinginevyo utaishi kwa majuto na misongo !!

Ni kwasababu Upendo husamehe,give her another chance plz,alfu anayeumia hapo ni wewe mwenyewe ni kama umeshikilia kaa la moto kumwunguza mtu,anayeumia zaidi ni yule aliyeshika kaa who is you now,msamehe maisha yaendelee


Tena Mungu amewarehemu kawaacha hai hadi Leo ni ili mmalize tofauti zenu,forgive her plz,Mungu akutie nguvu,na kama itatokea ukakumbuka mabaya yake u just pray for her and love her even more.
 
Yaaani wee mwanaume ndio bongee ya mpumbavu na ukumbuki andiko la enyi wazazi watiini watoto wenu na wanaume aishi na mke wake kwa akili. Ukihama hiyo nyumba roho inakuuma kumuacha wkt ni haki ya wanawe kuwalea na kuwarithishia hapo. Embu amka usingzini... na unamoyo kbsaaa mbwle ya wanao unaleta malaya na kumfanyia fujo walipo wanao! how deeea uua?
kuwa uyaone sio maghorofa
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom