Malisa aandika historia saut

Alfu Lela Ulela

JF-Expert Member
Oct 29, 2010
1,255
77
Aliyekuwa Katibu Mwenezi wa CHADEMA tawi la Chuo Kikuu cha St.Augustine (CHASO-SAUT) Bw.Malisa Godlisten ameshinda kwa kishindo urais wa chuo hicho licha ya mizengwe mingi iliyokuwepo. Malisa ameshinda kwa 70.1% ya kura zote zilizopigwa dhidi ya 29.78% alizopata Bw.Anthony Nestory aliyekuwa mpinzani wake. 0.12% ya kura zilizopigwa ziliharibika.

Uchaguzi huo uligubikwa na sintofahamu maana ulipaswa kufanyika March 10, lakini ukaahirishwa baada ya tume ya uchaguzi ya awali kuvunjwa. Tume hiyo ilivunjwa baaa ya Rais anayemaliza muda wake Bw.Cosmas Mataba kuweka pingamizi kuwa haikuwa tume huru. Kufuatia madai hayo Mataba akaunda tume "huru" ya uchunguzi, ambayo ilitoa mapendekezo kuwa tume ya uchaguzi ivunjwe.

Tume ikavunjwa lakini cha ajabu Mwenyekiti wa hiyo "tume huru" ndio akachaguliwa kuwa Mwenyekiti wa Tume mpya ya uchaguzi. Baada ya tume mpya kuundwa wakapanga kumwekea pingamizi Malisa kwa kuwa alikuwa Katibu Mwenezi wa chadema. Hata hivyo pingamizi hilo likashindikana maana Malisa alistaafu Uenezi wa CHADEMA tangu mwezi March mwaka huu. Lakini hata hivyo Makamu Mwenyekiti wa Tume ya Uchaguzi Bw.Sylvester Yalerd ni Mwenyekiti wa CCM tawi la SAUT.


MIZENGWE SIKU YA UCHAGUZI
Siku ya uchaguzi, jumatano ya tar.25/04/2012 Ofisi za tume zilifunguliwa saa 03:30 asubuhi kinyume na utaratibu badala ya saa 08:00 asubuhi. Hadi siku ya uchaguzi idadi ya vituo vya kupiga kura ilikuwa haijulikani. mwenyekiti akatangaza ni vituo 7, tofauti na mwaka jana ambapo vilikuwa vituo 15.

Mwenyekiti akaagiza uchaguzi uanze na watu wapige kura bila kuchovya wino eti Tume haina bajeti ya wino. watu wakapaza sauti na kupiga kelele kwa watatoa hela za wino, ndipo mwenyekiti akaenda kuchukua wino kwa Dean of Students.

Mjumbe mmoja wa tume ajulikanae kwa jina la Susu alikamatwa akipenyeza masanduku ya kura kwa kupitia mlango wa nyuma ya ofisi lakini wananchi walimkamata na kumdhibiti kikamilifu, maana zilikuwepo tetesi kuwa kuna kura feki zimechapishwa Musoma na zimeshapigwa tayari, zikisubiri kuchomekwa kwenye mabox ili zikahesabiwe.

Wakati zoezi la kura likiendelea mzee mmoja anayesoma BAED 3, alikamatwa akipiga kura kwa kutumia kitambulisho cha mwanamke chenye namba 19686. Alipokamatwa na kuchunguzwa ilijulikana kuwa yeye alishapiga kura na alikuwa akimpigia mtu mwingine. mtu huyo aliwekwa chini ya ulinzi wa polisi na baadae kuripotiwa kwa mwanasheria wa chuo.

Mpinzani wa Malisa, Bw.Anthony Nestory alikamatwa akifanya kampeni kwenye foleni ya kupiga kura, ambapo alitolewa na kupelekwa mbele, akapiga kura na kuondoka. Yapo madai pia kuwa Bw.Anthony alikuwa akifadhiliwa na vigogo flani ndani ya CCM.

Mawakala wa Malisa waliokuwa vituoni walisimamia vema zoezi la kupiga na kuhesabu kura na kuhakikisha hakuna masanduku feki yanaingizwa katika kituo cha kuhesabu kura, huku mamia ya wapiga kura wakiwa wamekusanyika nje kituo hicho wakiimba nyimbo za ukombozi. Wakati zoezi la kuhesabu kura likiendelea Campaign Manager wa Anthony alitoweka na hakurudi tena.


MALISA AWEKA HISTORIA
1.Amekuwa Rais mdogo zaidi (maika 24) tofauti na waliomtangulia.

2.Rais wa kwanza kushangiliwa na idadi kubwa ya watu baada ya kutangazwa (gari iliyombeba ilizimwa na wananchi wakaisukuma takribani kilomita 6 kutoka eneo la chuo).

3.Rais wa pili kutoka Mass Communication baada ya Zawadi Machibya (mtangazaji wa BBC).

4.Rais wa kwanza kumshinda mpinzani wake kwenye darasa lake (kwenye course ya BAED anakosoma Anthony, Bw.Malisa alipata kura 574, dhidi ya 466 za Bw.Anthony).

5.Rais wa kwanza kuongoza kwa kura katika madarasa yote isipokuwa darasa la Sociology, alipokuwa anatoka mgombea mwenza wa Anthony aitwae Alice.

6.Rais wa kwanza ambaye amewahi kuwa kiongozi wa chama cha siasa cha upinzani, licha ya juhudi zilizofanywa na uongozi wa CCM Mwanza kumtoa kwenye mchakato.


 
Vyuoni ndio kipimo kizuri ccm kujiangalia upya dhahama ya 2015 itawaumiza wengi. Sie enzi yetu tulipata Mnyika na amekuwa mwanamageuzi mpaka leo yupo mjengoni.
 
lakini cha ajabu Mwenyekiti wa hiyo "tume huru" ndio akachaguliwa kuwa Mwenyekiti wa Tume mpya ya uchaguzi.


hapo sina mbavu...haya naendelea kusoma.

mwenyekiti wa tume huru iliyoundwa kwa ajili ya kuunda tume huru ya uchaguzi ndo akawa mwenyekiti wa tume huru ya uchaguzi.
 
hongera dogo,hiki ni kizazi cha mabadiko ya kweli sio kupendekeza au kuteu .kura ndio mpango mzima
 
Nilijua tu malisa ni motowa kuotea mbali tangu akiwa majengo sec moshi alivuna wanachama wengi sana,he is talented plus tym aliyokaa norway hakwenda kushangaa maghorofa bali alijipika ipasavyo
 
infact dogo amejitahidi ingawa kuna baadhi ya vitu umepost humu kama hazimo vizuri ,me nilifuatilia uchaguzi ule na ambacho saizi nasubiri ni kwamba kuna baadhi ya kashfa ambazo kijana malisa alikashifiwa na picha zake kuchanwa kitendo ambacho ni kinyume na sheria itabidi picha walizopigwa wahusika zifikishwe ofisini kwa ajili ya hatua mbadala na wale ambao picha zao zimepatika wakichafua kwa maandishi picha za antony nao pia inapaswa wawajibishwe kwa kufuata sheria za nchi kwa upande wa chuo ni kwamba kwa yeyote yule ambaye atakutwa na shitaka itabidi afukuzwe ndo kauli ya mlezi wa wanafunz hapo chuoni. . .dogo malisa nampongeza mwanzo mzuri.
 
Asante kwa kutujuza,
mwana chadema awa kiongozi St. augustine university.
mwenye macho aambiwi tazama!
 
Nafikiri atakuwa ni rais wa nne kutoka Mass Comm (si wa pili). Wa kwanza alikuwa Amani Millanga (2000-2003). Alifuatiwa na Peter Msofe (2001-2004) na Zawadi Machibya (2002-2005). Waliofuata hapo siwajui. Hongera Malisa
 
Kuna thread moja hapa jamvini ilisema kwamba katuka chaguzi nyingi za vyuo vikuu, wachadema hupendwa zaidi na wanashinda kwa kishindo chaguzi hizo!
M4C zikianzia vyuoni ni dalili nzuri ya mavuno makubwa msimu wa 2015.

Hongera Malisa, Hongereni marubani wa M4C!
 
Back
Top Bottom