Malipo ya Dowans yawekwe kwenye foleni -- hadi 2020

Zak Malang

JF-Expert Member
Dec 30, 2008
5,404
234
Nimesikia katika vichwa vya habari kwenye mojawapo ya magezeti yaliyosomwa leo redioni kwamba Hazina (Treasury -- i.e. Wizara ya Fedha) imesema haina hela sasa hivi kuilipa Dowans mabilioni hayo.

Na ni bora isiwe nazo kabisa hizo hela -- kwani itafanya ukatili mkubwa sana ikiwalipa hawa Dowans kwanza kabla ya mamia (bila shaka) ya wananchi wengine wanaodai malipo yao kutoka serikalini -- wengine kutokana na amri za mahakama halali za humu kwetu ndani -- siyo mahakama uchwara inayoketi katika sitting room ya RA.

Treasury iwasaidie wananchi, iweke madai hayo ya Dowans katika foleni, mwisho kabisa, yatangulie yale yaliyokuja mwanzi, hata ni kama ya miaka kumi iliyopita. Dowans ina haraka gani? Inataka ilipwe kabla Bunge kukutana, na ambalo RA na genge lake la wezi linahofu linaweza kupiga kura kusitisha malipo hayo?
 
Si nilisikia inatakima ilipwe A.S.A.P kila inapopita siku moja kuna faini ya mill 20.mpaka 2020 si itakuwa hata trillion,au inakuaje?
 
Hivi hakuna mtu wa kwenda mahakamani kuzuia malipo hayo? Hivi kweli hakuna njia nyingine kabisa? CJ Chande vipi, yuko upande gani. Twakuomba usikie kilio cha wananchi na usiisajili hukumu hiyo. Kwa kiasi fulani utakuwa umesaidia kuiokoa nchi iambayo dalili zote zaonyesha inaelekea kwenye machafuko huko mbeleni. Please CJ Chande, help us!! You are our only hope!
 
Tukiacha ku support ufisadi, 2015 tukachagua kiongozi mzuri.Watashangaa 2020 badala ya kwenda bank kuchukua jasho letu wanaelekea Ukonga.
 
Wakidhubutu kulipa bila kupata kwanza ridhaa ya mahakama kuu, kama yalivyo matakwa sha sheria wananchi tutakuwa tuna uhalali wa kuandamana nchi nzima.
 
Serikali kwanza iwalipe TANESCO malimbikizo ya deni lake. Nasikia ukijumulisha na Zanzibar ni mabilioni ya kutosha. Serikali inashupalia kuilipa Dowans ili iweje. Inasahau yenyewe ndo kati ya wadaiwa sugu.

Hivi tusipowalipa hawa dowans watatufanya nini?? Sisi si ni dola kamili. Kama ni lazima basi RA na Ngeleja wawalipe kutoka mifukoni mwao.
 
Si nilisikia inatakima ilipwe A.S.A.P kila inapopita siku moja kuna faini ya mill 20.mpaka 2020 si itakuwa hata trillion,au inakuaje?

mkuu.... pale tu hukumu ya ICC itakaposajiliwa mahakama kuu..., basi kuanzia kesho yake malipo hayo yatakua yana accrue interest kila kukicha... kwa hiyo bado tuna kamuda ka kujipanga
 
Hivi hakuna mtu wa kwenda mahakamani kuzuia malipo hayo? Hivi kweli hakuna njia nyingine kabisa? CJ Chande vipi, yuko upande gani. Twakuomba usikie kilio cha wananchi na usiisajili hukumu hiyo. Kwa kiasi fulani utakuwa umesaidia kuiokoa nchi iambayo dalili zote zaonyesha inaelekea kwenye machafuko huko mbeleni. Please CJ Chande, help us!! You are our only hope!

Chande yupo upande wa wala kuku kwa mrija. Ndo maana akaukwaa u-CJ kutoka kwenye msururu wa wapendekezwa!
 
Serikali kwanza iwalipe TANESCO malimbikizo ya deni lake. Nasikia ukijumulisha na Zanzibar ni mabilioni ya kutosha. Serikali inashupalia kuilipa Dowans ili iweje. Inasahau yenyewe ndo kati ya wadaiwa sugu.

Hivi tusipowalipa hawa dowans watatufanya nini?? Sisi si ni dola kamili. Kama ni lazima basi RA na Ngeleja wawalipe kutoka mifukoni mwao.

Yes! Tusipowalipa watafanya nini? Watatutia utumwani? Hakuna kulipa, wafanye chochote, narudia chochote wanachotaka. Na hicho "chochote" utakuta kwamba hawanacho, ni woga tu wa serikali ya JK.
 
Wakidhubutu kulipa bila kupata kwanza ridhaa ya mahakama kuu, kama yalivyo matakwa sha sheria wananchi tutakuwa tuna uhalali wa kuandamana nchi nzima.

Kwa nini tusubiri wajilipe kwanza kabla ya ridhaa ya high court ndio tuandamane?Kwa nini tusifanye hivyo sasa hivi?TUCTA mko wapi,ebu tuhamasisheni wafanyakazi nchi nzima tugome kupinga udhalimu huu.!wapi wafanyabiashara,wakulima,wanavyuo....natamani kweli .....
 
Nisikiavyo, viongozi wengi katika serikali, na Cabinet pia, hawapendi ikawalipa Dowans, isipokuwa wachache tu. Kuna kampeni kali za ndani kwa ndani kuzuia, kwani wanaona ikilipa, basi CCM itazidi kutengwa na wana-CCM wengi na wananchi kwa ujumla, hivyo kuthibitisha utabiri wa Shibuda kwamba CCM itafia mikononi mwa JK.
 
riba ni 7.5%

Riba ikafie mbali. Kwa nini katika hili la Dowans riba ndiyo izungumzwe sana kuitisha serikali ilipe haraka? Mbona hawazungumzii riba katika madeni mengine ya serikali inayodaiwa -- kama vile yale ya wazee wa EAC? Nakubaliana na mmoja hapo juu kwamba serikali isilipe -- tuone hao akina RA na maswahiba wao wa ICC watafanya nini? hakuna lolote watakalofanya, I tell you.
 
riba ni 7.5%

Kwani serikali inalipa hela ngapi kwa njia ya riba tu kutokana na madeni inayodaiwa na wafadhili wa nje, na ambayo huchelewsha kuyalipa? Mwaka 1979 Brazil walitupa mkopo dola milioni 5 kujenga barabara na hadi leo hatujalipa jumla ya dola milioni 150 pamoja na riba. Mbona Brazil haijatufanya chochote?

Kwa nini tumuogope huyu fisadi RA eti riba itakuwa kubwa! Na iwe kubwa tuone basi!
 
Back
Top Bottom