Malima kulala chumba cha 400,000/= hii ni nini CCM jitafakarini

monitor wa darasa na mwalimu wa nidhamu hadi mwalimu mkuu wako kimya darasani wanafunzi wanacheza kidali poa,kelele hadi wengine wanakojolea madawati
 
Kwa asiyejuwa Kiswahili kusema vijipesa au vijisenti inakuwa ni mwao, kwa Waswahili ni neno la kawaida kabisa na hata ukitembea na mabillioni inatakiwa usijikwaze kwa kusema natembea na "mapesa" au "mabillioni". Hata bwana "mapesa" aliomba msamaha wakati fulani kwa kauli yake hiyo.

Nna uhakika kuwa wote ambao mnashangazwa na hilo neno, Kiswahili si lugha mama kwenu. "Nimejidundulizia vijisenti vyangu nikajijengea kibanda changu mtaa wa Mahiwa", Kumbuka hiyo ni prime area Kariakoo Dar. Na hilo ni jumba la vyumba sita ambalo kiwanja tu kwa sasa ni millioni 800. Ni utamu wa Kiswahili.
 
Jeshi la polisi mkoani morogoro limetaja vitu alivyoibiwa mh Adam Malima ni pamoja na pete mbili zenye thamani ya sh mil 2.5!. Hivi haya mapete makubwa kubwa ambayo mheshimiwa huonekana akiyavaa tena ya gharama kubwa, yana tija gani kweli?. Je ni kutaka kuonekana mtanashati au kuna ushirikina ndani yake?. Nimepata kuona viongozi mbalimbali nchini akiwemo mkuu wa kaya pamoja na yule waziri wa fedha Mustaafa Mkulo wakiwa wameyavaa pia, lakini haya ya Adam Malima ni bab kubwa. Cha kushangaza huwa sioni pete za ndoa mikononi mwao. Kwangu mimi binafsi huwa nachukulia kama ni ulimbukeni...haina tofauti na wanaume wanaovaa hereni au shanga! tumezoea vijana mitaani wanaitwa masharabaro wakiwa wamelipuka kila aina ya madudu yakiwemo hayo ya mh Malima. Gharama ya mil 2 ya pete hizo angeenda hata pale kituo cha watoto yatima Dogodogo centre akawanunulia chakula.
 
Kama hela inaruhusu kwanini asilale? Umasikini wenu usifanye na wengine waishi kwa tabu.
Pesa inayotumika pale ni kodi yetu. Hii inaamana kuwa malipo usiku wake mmoja anawalaza njaa watz 400 wanaoishi chini ya dola moja... hii ni sawa kweli????? bora karudisha alichotuibia
 
Jamaa Chapombe Sana akiitwa fataki sitashangaa!!!!Anasema eti saa zote yupo stand by mkuu wake waziri akimtuma safari ya nje iwe ni rahisi kwake.Swali>Angeweza kwenda nje na silaha zote alizokuwa nazo?
 
Hajaibiwa kupitia dirishani wewe,
Changu alieingia nae ndio kamkomba.
Kwa nchi za wenzetu hii ni kashfa kubwa sana, pengine hata Anaweza kushtakiwa kwa uzembe.
Maana hata hiyo laptop itakua Na Nyaraka mbalimbali za siri za serikali.


Hawakawii kusingizia chadema hawa!
 
sidhani kama kuna hotel ya lk 4 Tanzania hii umesikia vibaya!

mkuu level nyingine zipo ktk nchi hii hujawahi na huenda mpaka unakufa hutafika!zipo zaidi tena kwa mbali!uliza watu wanaojua watakuambia!ask Bilila Lodge!

shida hapa sio bei ya hotel,shida ni je kiongozi wa umma,anayetumia fedha za umma anastahili kulala hapo?vinginevyo atuthibitishie ilikuwa safari binafsi na alikuwa anajigharamia mwenyewe kwa pesa yake!
 
Yaani kuna watanzania wenginw ni janga kabisa "Hivi wewe ni mtanzania au mrundi?, unaishi au ni marehemu?, Yaaani hawa wendawazimu wa rangiza njano na kijani kutumia ovyo kodi na resources za nchi hii vibaya wewe unaona sawa tu".


Kama hela inaruhusu kwanini asilale? Umasikini wenu usifanye na wengine waishi kwa tabu.
 
Back
Top Bottom