William J. Malecela
R I P
- Apr 27, 2006
- 26,588
- 10,375
Yes;we're Great thinkers lkn sasa tunapoanza kujadili watu na kuacha kujadili kwa nini wanagombea na kushinda tunatia mshaka hiyo thinking capabilities yetu imeegemea wapi!
Uzee hauna hata kipingamizi kimoja cha kumfanya Mzee Malecela au Jackson Makweta asigombee at the same times ukijana haumfanyi wana Sengerema au wana Nyamagana au wana Kigoma ndiyo wawarudishe wabunge wao akina Ngeleja,Masha,Serukamba hata Zitto Kabwe bungeni!Kinachopimwa ni kama wametimiza kile walichowahaidi wapiga kura wao!
Kwa sababu katiba inamruhusu bila kipingamizi mtu yeyote afikiae umri wa miaka 18 kugombea Ubunge na atleast uwe na miaka 40 kugombea Urais basi tuiheshimu katiba;na kama unahisi mtu fulani hafai kuwa Mbunge kwa sababu ya umri wake aondolewe kwa sanduku la kura kwenye uchaguzi na wala si zaidi ya hapo!
West Virginia wanaye Seneta mwenye umri wa miaka 92 sasa,na kule Connectcut walikuwa nae Seneta Biden kwa miaka karibu 40;na wote walipigiwa kura na wananchi na wale hawakuteuliwa!Sasa kama Mzee Malecela anachaguliwa kwa kutumia sanduku la kura kwa nini apigiwe kelele hivi hapa JF?
Nasisitiza tena,kama wana Mtera wataona mzee Malecela anawafaa sisi JF hatuna la kufanya,kama wanaona hawafai watamuangusha kwenye uchaguzi kama walivyomuadhibu mwaka 1980's alipoangushwa na Mazengo kwenye uchaguzi wa Ubunge!
- Marekebisho hapo Great Thinker, Biden amekuwa Senator wa Delaware for the last 36 years na sasa he is about kumrithisha mtoto wake ambaye ni Attorney General huko.
Respect.
FMEs!