Malecela: kuweka mihula kwa wabunge ni kukiuka Demokrasia

Unajua kuna vitu vingine Mwalimu Nyerere alivifanya utafikiri ni Nabii. Malecela angekwenda Ikulu tungekuwa na Museveni mwingine. Katiba ingebadilishwa kwa kisingizio kama anachotoa kuhusu ubunge. katika nchi changa kama yetu kuhodhi madaraka muda mrefu kuna kasoro kuliko kuachiana. Hivi Maelecela kama alivyo ana kitu cha kuongeza kwa wapiga kura wa Mtera?
 
Nakubaliana na haja ya kufanya hivyo kwa kuwa, Wabunge si watendaji, bali ni wawakilishi wa wananchi. Hivyo wananchi wanatakiwa waachiwe uhuru wa kuamua nani awawakilishe katika kutoa maoni, mahitaji na mapendekezo yao kwa serikali.

'Uwakilishi' na 'utendaji' ni dhana tu lakini kimsingi wote wanapaswa kutimiza majukumu fulani (kufanya kazi!). Kumbuka wabunge ndio hao wanaunda kamati mbalimbali za kibunge za kuisimamia serikali.
 
Unajua kuna vitu vingine Mwalimu Nyerere alivifanya utafikiri ni Nabii. Malecela angekwenda Ikulu tungekuwa na Museveni mwingine. Katiba ingebadilishwa kwa kisingizio kama anachotoa kuhusu ubunge. katika nchi changa kama yetu kuhodhi madaraka muda mrefu kuna kasoro kuliko kuachiana. Hivi Maelecela kama alivyo ana kitu cha kuongeza kwa wapiga kura wa Mtera?

Umri jamani msameheni bure! Nimecheka sana watu design ya Mugabe hawa!
 
Mzee JSM ameshavuka ule umri wa kuondoka madarakani kwa hiari. Hapo alipo ni kifo tu kitamwondoa. Ukishavuka miaka 70 kuondoka madarakani ni taabu. Ni KATIBA tu inawaondoa watu kama hawa au nguvu ya Mungu. Mwambieni JK amhakikishie nafasi kwenye jimbo la ikulu.
 
'Uwakilishi' na 'utendaji' ni dhana tu lakini kimsingi wote wanapaswa kutimiza majukumu fulani (kufanya kazi!). Kumbuka wabunge ndio hao wanaunda kamati mbalimbali za kibunge za kuisimamia serikali.

Ni kweli kabisa ndugu yangu. Ni majukumu hayo ndio yanayotofautisha kazi wanazofanya.

Kwa mtazamo wangu, hakuna kitu kitakachofanywa na binadamu kisiwe kazi. Hata kupumzika ni kazi binafsi.

Kamati za Bunge zinasimamia kwa kupata taarifa za utekelezaji wa taasisi za serikali. Baada ya hapo zinatoa mapendekezo. Na kama unavyojua, Kamati hizo hazitekelezi mapendekezo inayotoa.

Mkuu, Mbunge anakuwa mfanyakazi anapopewa majukumu ya ziada (kama uwaziri au unaibu waziri n.k). Vinginevyo kazi zao kubwa ni kushauri, kushawishi, ku-lobby, kuhakikisha serikali inatimiza malengo yaliyokubaliwa na Bunge.
 
Mambo haya ya kudai ukomo yanatokana na chaguzi zetu kutokuwa/kutoonekana kuwa HURU na HAKI. Mapesa ya ajabuajabu yanatumika kwenye kampeni, wakishachaguliwa wabunge wakapata nafasi za uwaziri wanaitafuna nchi kwelikweli, utawaondoaje hawa bila kuweka ukomo?

mimi nadhani irrespective of circumstances there should be a time limit. Hata kiongozi awe bora vipi lazima ufike muda atoke then wengine waje. Hiyo pia itasaidia hawa wanaobaki bungeni ili kujilinda kwa mabaya yao waliyofanya nyuma.
 
mzee wa zege naona zege linazidi kumwelemea hana mawazo mapya kabisa. Vision imepotea kabisa.
 
Vinginevyo kazi zao kubwa ni kushauri, kushawishi, ku-lobby, kuhakikisha serikali inatimiza malengo yaliyokubaliwa na Bunge.

Recta,
Nashukuru tunakubaliana katika hoja hiyo ya kazi. ubunge kama kazi inahitaji ubunifu katika kujenga hoja, kufanya utafiti, kukagua na kufanya tathmini na kubwa zaidi kutunga sheria. Mambo haya si kazi ya lelemama hata kidogo kwa mtu aliye serious na uzalendo kwa nchi yake. Ndipo hapa panapohitaji mawazo mapya na watu wapya.

Hivyo kama ilivyo kwa u-Rais, ubunge pia ni vema ungalikuwa na kikomo. Kwa mtu mchapa kazi term mbili (zikizidi sana tatu) zinatosha kuleta mabadiliko. Kwa 'domo'krasia yetu huku Afrika,na ushindi wa 'simple majority', ni wazi mtu anaweza kukaa milele bungeni hata kama 'hana jipya'! Ndio hao unaona wanaunga mkono hoja 'mia kwa mia' hata kama zina mapungufu ya wazi!
 
naona tungeweka umri wa kustaafu katika ubunge na kusema miaka 75 mwisho.

na pia tuweke mihula, na kusema mihula 4 mwisho. naimani kabisa kama ujafanya mabadiliko kwa kipindi cha miaka 20 basi huwezi kufanya mabadiliko tena.
 
Kwisha choika mbaya unategemea nini hapo kwa comment za mbunge wa aina hiyo jamani jamani hivi wote mkiwa ving'an'ganizi namna hiyo leo hii bunge letu lingekuwaje.hebu fikiria mpaka leo tuwe na wabunge wa aina ya huyo mzee.A quuen with eleven president! aah an MP celebrating a diamond Jubilee as an MP acheni hizo hii nchi ya wote.
 
Naona Mzee mzima Malecela ameoa ufisadi, ufisadi si katika fedha tu hata madaraka, kujikusanyia wewe ni ufisadi. Kwanza pia atambue kuwa dunia ya sasa inahitaji mawazo ya vijana zaidi, ye kwake hajui kuwa kesho ya ndiyo sasa, bado am,elala huyu!!
 
I would say kuwa na wabunge ni kukiuka demokrasia. Na bunge letu limetoka hata kwenye "rubber stamp" sasa limebaki "hollow shell".

Tunatakiwa kuwa na checks and balances kati ya bunge, serikali kuu na mahakama, lakini rais ambaye ni mkuu wa serikali pia ni sehemu nzima ya bunge na anaweza kuvunja bunge.

Wabunge wanaotakiwa ku represent interests za wananchi wana represent interests za chama na kuteteana, sasa hapo demokrasia iko wapi?

Kuwa na wabunge ni kukiuka demokrasia.Kama demokracy is the rule of the people, and the MPs do not represent the interests of the people, how can this setting be said to be democratic?

Kamati ya Uchaguzi yenyewe inachaguliwa na rais, ambaye ni mwenyekiti wa CCM. Sasa hata hatujui legitimacy ya matokeo ya wabunge na rais!
 
Kweli wananchi wanafhamu nani wa kumchagua baada ya kupewa kanga, kofia, na vikoi pamoja na biscut na keki. Wacha kusiwe na kikomo hadi vitukuu vitakaposhika madaraka.
 
Ningekuwa mimi Mzee Malecela, nadhani kuwa huu ndio ungekuwa wakati mzuri wa kujijengea historia imara ya kuwapiku Nyerere na Mwinyi kwa sababu ya uzoefu serikalini, bungeni na ukweli kuwa nimekuwapo madarakani katika kipindi ambacho nyakati zimebadilika. Ningesukuma mabadiliko ya katiba kuweka ukomo katika wabunge kusudi miaka ijayo jambo hili liwe unahusishwa na mimi; kwa sasa hivi ukomo wa urais unahusishwa na Nyerere.
 
Hi mifano siku zote huwa mizuri when they work for but when they work against hawa wakuu huwa hawakawii kuruka na kusema ooh! hapa sio Marekani au UK, we are still a young democracy, we have to do things on our way etc. etc.

Sasa on this hata kama hakuna sehemu nyingine zinafanya hivyo kwa nini sisi tusiwe wa kwanza????? Ili na wengine wajifunze kwetu????????


Nilikuwa naisubiri point hii !! Hawa jamaa wakizungumzia mambo yanayowanufaisha wao hutolea mifano nchi za wenzetu..Lakini inapotokea hali ya kuwapinga husisitiza kwamba hatuna uwezo wa kufanya mambo hayo kama wenzetu..!!

Let say the topic ya mishahara midogo kwa wafanyakazi wa Serikali wa Tanzania..!!Walipotolewa mifano ya mishahara ya wenzetu majuu kimbilio lao lilikuwa kwamba uchumi wetu ni mdogo hatuwezi kulipa mishahara sawa na wao..! Hawa jamaa ni balaa kabisa..!! Huyu mzee hana hata aibu..!! Anataka kufia Bungeni ndipo ajue kwamba wakati wake ume kwisha huyu mzee..!!

Maoni mengine yanawapunguzia heshima hawa watu..!!!Kwanini wasiwe kama Lennox Lewis ambaye aliamua kujitangaza kupumzika ili kutunza heshima yake ya Ubondi..!!
 
Unajua kuna vitu vingine Mwalimu Nyerere alivifanya utafikiri ni Nabii. Malecela angekwenda Ikulu tungekuwa na Museveni mwingine. Katiba ingebadilishwa kwa kisingizio kama anachotoa kuhusu ubunge. katika nchi changa kama yetu kuhodhi madaraka muda mrefu kuna kasoro kuliko kuachiana. Hivi Maelecela kama alivyo ana kitu cha kuongeza kwa wapiga kura wa Mtera?


Wakati mwingine inabidi tu kucheka ..!! Huyu mzee ni mlafi kabisa.. Nyerere aliyagundua yote hayo..Japo Baba wa Taifa alikuwa na udhaifu wake lakini aliweza kuitambua kebineti yake na kumkataa huyu mzee..Naunga mkono UNABII WAKE..!!

Na si siri hata udhaifu wa Rais wetu Baba wa Taifa alishauona mapema sana pia.Kama tutaweza kumkumbuka Baba Nyerere ni kwa hivi vioja tunavyo viona kwa sasa..!!!
 
Who is the oldest sitting US senator?



Robert Carlyle Byrd (born November 20, 1917) is the senior United States Senator from West Virginia, and a member and former Senate Leader of the Democratic Party. Byrd has been a Senator since January 3, 1959 and is the longest-serving member in the Senate's history. He is also the oldest current member of the United States Congress, and is the first politician in U.S. history to serve as a U.S. senator uninterrupted for half a century.

- Ukifuatilia huu mjadala ni vigumu sana kuelewa, kinachojadiliwa ni principle au ni jina na ndio hasa kilichotufikisha hapa tulipo hili taifa, hijawahi kua on principles siku zote ni fulani, fulani political action kufuatia fulani hakuna, ila ni maneno ya kelele za mlango tu!

- Kama umri wa viongozi wetu ni tatizo, basi tuonyeshe kwa utafiti tena academically kwamba wazee wameharibu one, two, and three na tizama vijana walivyorekebisha makosa ya hao wazee kwa one, two, and three, for that sasa ni vyema tukawa na sheria mpya ya kuanza na umri wa viongozi na pia ukomo wa kugombea na kuongoza, maana ukisoma kwa makini hoja nyingi kwenye hii thread unaweza kuamini kwamba Malecela anajipa tu ubunge, bila uchaguzi wala kura!

- Tumezoea maneno mengi matendo hakuna, Lowassa alipoharibu tumeiacha opportunity kubwa sana ya kupitisha sheria za kuwafunga mawaziri wakuu wote watakaorudia tena ujanja kama wake, lakini badala yake yakaishia kua maneno mengi hewa tupu, infact akaishia kutuachia a very foolish National debate kwamba alikosa kweli, alionewa, au hakupewa nafasi ya kujitetea and we loved it kujionyesha jinsi tulivyokwenda shule uchwara huku yeye anaondoka pole pole!

- Malecela na wazee wengine wote wanaofanya 15% ya bunge letu against vijana ambao ni 80% wana haki kisheria kuendelea kugombea ubunge, mpaka wananchi wao watakapoona wamechoka nao, watawabadilisha kwa kupitia uchaguzi na kura, na si vinginevyo unless tumepitisha sheria mpya za kuhusu umri. Ukomo wa uongozi ni hadithi za abunuwasi kwa wasio na uwezo wa kushinda uchaguzi, kila siku visingizio vipya, mata sikumoja ni independent candidates, mara siku nyingine zimeibiwa kura, mara siku moja ni wazee hawa, and then ni Mrema ndiye hafai, and then another day ni Lipumba na Seif, absolutely no clue what is our problem!

- Tizama jimbo la Serukamba, walimuondoa mzee wakampa huyu kijana, hawa kina Ngeleja ni vijana, kina Rostam hata anaweza kushirki American Idol kutokana na ujana wake, kina Ndulu wote hawa ni vijana aibu tupu! Sasa tumekaa hapa na kelele zisizo hata na masilahi kwa taifa utadhani sometimes ni watu wako vilabuni huko Saigon, badala ya kujadili facts, kwamba hatutaki wazee kwa sababu wamefanya ubaya one, two, and three no ni Malecela, Malecela and Malecela JF! and Malecela na Mama Kilango, Bwa! ha! ha! ha!

- Wakuu Great Thinkers tuambieni kwa academic facts tofauti ya results za viongozi wetu wazee na walio vijana, tuonyesheni mifanpo ya kisayansi hapa how kijana Serukamba is better kiuongozi kuliko Malecela, jinsi kijana Rostam alivyo bora kiuongozi kuliko Makweta, jinsi kijana Sophia simba alivyo bora kuliko Mrema, ishu kama hizi zinahitaji principles sio maneno maneno kama walevi wa Rubisi na kimpumu kama sio matapu tapu, hapa mjini kuna pombe moja inaitwa ugali kwa ugali ukiinywa hata kama una elimu ya ajabu waalahi utaishia kuchekesha tu maana utaweweseka tu hoja hakuna!

- Wananchi wa jimbo la Mtera wana haki zote za kutompigia kura mgombea yoyote wanayemuona hawafai, lakini hawawezi kuamuliwa na online political activism ambao hawawezi hata kujadili on accademic lines madhara ya viongozi vijana na wazee! Poleni sana wakuu demokrasia haikuanzishwa na vijana wala wazee, na wala haikuanzishwa kwa ajili ya ubaguzi wa wazee au vijana, ila demokrasia ni collective ideas za society bila kujali rangi, umri wala anything, humu forums vipi hatuna mizeee humu?

- Eti wakuu humu JF hatuna wazee? Sasa kwa mantiki hii ya wazee na vijana mnafanya nini humu? au ndiyo yale yale ya kunga'nga'nia humu mpaka mjifie tu kwenye keyboard? Bwa! ha! ha! ha! I mean najua kuna vijana hapa, lakini wengine mngenyamanza tu maana maneno yenu tu yanawasuta kuwa vingwengwe vya kutupwa, I mean vibabu mnatka kutufia humu Bwa! ha!

- Great Thinkers huongea kwa hoja wakuu sio kelele za mlango! Unless mmetuonyesha sheria iliyovunjwa na Malecela kwa kugombea ubunge at his age! Halafu mtuonyeshe utafiti wa kisayansi vijana na wazee kiumri wananzia wapi na kuishia wapi, umri gani ni kijana na umri upi ni mzee, au endeleeni na kelele za mlango! Sisi wengine tunajadili hizi ishu kwa kuangalia masilahi ya taifa!

Respect.


FMEs!
 
Tatizo wazee wakishafikia umri fulani wanasinzia sana.

New-Picture-29.bmp
 
Nilikuwa naisubiri point hii !! Hawa jamaa wakizungumzia mambo yanayowanufaisha wao hutolea mifano nchi za wenzetu..Lakini inapotokea hali ya kuwapinga husisitiza kwamba hatuna uwezo wa kufanya mambo hayo kama wenzetu..!!

Let say the topic ya mishahara midogo kwa wafanyakazi wa Serikali wa Tanzania..!!Walipotolewa mifano ya mishahara ya wenzetu majuu kimbilio lao lilikuwa kwamba uchumi wetu ni mdogo hatuwezi kulipa mishahara sawa na wao..! Hawa jamaa ni balaa kabisa..!! Huyu mzee hana hata aibu..!! Anataka kufia Bungeni ndipo ajue kwamba wakati wake ume kwisha huyu mzee..!!

Maoni mengine yanawapunguzia heshima hawa watu..!!!Kwanini wasiwe kama Lennox Lewis ambaye aliamua kujitangaza kupumzika ili kutunza heshima yake ya Ubondi..!!

- Sasa haya ni mawazo ya Great Thinker! ya kumtukuza shoga Lennox kwamba ndiye role model wako, sasa awe na kwetu wengine wote inatia hata kinyaaa, yaani ni kukurupuka tu mradi kusema tu!

Es!
 
Back
Top Bottom