Malecela, Chitalilo Vs Dr Slaa

Mwanakijiji kasema wapi hiyo kauli?
Hapa kuna wanao pigania maslahi ya chama.
Yeye anadai ccm ndio wapewe mustakabali wa nchi!
Nasema NO NO NO!


Once again you don't read what somebody actually said.. unadhania amesema hivi au vile...

Narudia tena na uangalie maneno ninayotumia na usiogope kufikiri:

Technically.... - unaelewa maana ya kutanguliza hiyo?

JM yuko sahihi, CCM ni waanzilishi wa hoja ya ufisadi.. think about it

BabaH.. you on the right track kwani nilichosema hapo is deeper kuliko watu wanaoharakisha kufikiri nimesema nini kwa vile hawataki kufikiri nilichosema.
 
Realist!!! And who is an idealist in this context?? I thought most of us here are idealists trying to shape the Tanganyika we want!! Just thinking aloud!

There are people caught up in this Opposition vs CCM race for brownie points.

To some the opposition can do no wrong, to some CCM can do no wrong.This is exactly the sort of thinking that start a nonsensical and precious time consuming debate on "who started the EPA saga", pointlessly partisan puckering.

I abhorr such idealism, the priority should be solving problems, not politicking for brownie points.
 
MKJJ huu si muda wa codes tena jamani!
Mimi nimeshasoma ripoti zote!
Najua huu ni wakati wa SHERIA ILI HAKI IPEWE NAFASI!
SASA HAYA MAMBO YA KUSEMA HOJA NI YA ccm SI NI KAMA KUANZA KUGOMBANIA MADARAKA KABLA YA HAKI KUTENDEKA?
NANI ASIYEJUA ccm WAKIACHIWA HAWATAPINDISHA KAMA AMBAVYO WAMEKUWA WAKIFANYA?
SI JUZI TU WAMEPITISHA BAJETI YA KIFISADI HUKU BADO MKIWA STAUNCH SUPPORTERS?
Mi ngoja nijirudie zangu kule kwenye issue za kagoda!
Sasa si ni wewe ulikuwa uking'ng'ana na ZIMBAWE na sasa una lipi jipya?
 
Koba.. "think about it"... hivi ni vigumu sana kufikiri nilichosema! ?
MKJJ,

Oh yeah, come to think of it; the whole lot began with CCM, when they diverted from their core business to being a gang of looters, a syndicate: from CCM to Chama Cha Majambazi and now Chama Cha Mafisadi.

Haiwezekani kwa mtuhumiwa kujifanya yeye ndiye mpelelezi mkuu... kutakuwa na haki hapo? Let others prosecute. Such a common law our lawmakers are failing to comprehend. Our parliament is such a cheap place where only the dumberer can inhabit... A sane person person can never dare to stand up for the dirt in there...

This topical appeasement by JM is meant to confuse and disorient, so that the focus is diverted, and with others (Serukamba, Chitalilo) contributing to the chaos, the scene becomes muddled, and that's what they want.

Unfortunately Ufisadi has become such a sticky issue and has refused to follow the 7-day rule for news in the media:

Mpaka Kieleweke!
 
HOJA KUWA YA ccm AMA LA,IJADILIWE BAADA YA HAKI YA KISHERIA KUCHUKUA MKONDO WAKE!
Msituchanganye kabisaa!
USHAHIDI KUWA ccm ILICHOTA PESA ZA EPA KWA KUMTUMIA MWENYEKITI WAO IDDI SIMBA KWA KUSHIRIKIANA NA MALEGESI NA LUKAZA...!
SASA BADALA YA KUWAKAMATA KWASABABU USHAHIDI UKO NJE...MMEAMUA KUWAKUMBATIA NA KUWASAFISHA KWA STYLE AMBAYO WENGI WETU HAPA JF HATUJAIPENDA!
Neno ccm liwekwe kando kwa sasa...Na siyo ccm tu!
Hata CHADEMA NA VYAMA VINGINE VYOTE!
SASA NI EPA,RICHMOND,KAGODA,KIWIRA ETC ETC!
 
MKJJ huu si muda wa codes tena jamani!
Mimi nimeshasoma ripoti zote!
Najua huu ni wakati wa SHERIA ILI HAKI IPEWE NAFASI!
SASA HAYA MAMBO YA KUSEMA HOJA NI YA ccm SI NI KAMA KUANZA KUGOMBANIA MADARAKA KABLA YA HAKI KUTENDEKA?
NANI ASIYEJUA ccm WAKIACHIWA HAWATAPINDISHA KAMA AMBAVYO WAMEKUWA WAKIFANYA?
SI JUZI TU WAMEPITISHA BAJETI YA KIFISADI HUKU BADO MKIWA STAUNCH SUPPORTERS?
Mi ngoja nijirudie zangu kule kwenye issue za kagoda!
Sasa si ni wewe ulikuwa uking'ng'ana na ZIMBAWE na sasa una lipi jipya?

Jmushi.. ninapokushawishi usome mtu alichoandika na ufikiri kabla hujatamka ninataka kukusaidia upolish ujengaji hoja wako. Kudai kuwa mimi "nimedai" CCM ipewe nchi ni uzushi wa wazi kwa sababu kama ungefuatilia maandishi yangu hutaona mahali hapa pamoja nimewahi kusema kitu kama hicho au hata kukiashiria! Lakini well, huwezi kukanusha na kusema "niwie radhi". Unaamini unachoamini hata kama hakina msingi na uko tayari kukisukumiza kooni alimradi usikubali kuzusha.

Ushauri wangu, kama huelewi mtu kasema nini au una wasiwasi unaweza ukamnukuu vibaya muulize akueleweshe ili utakapoamua kumpinga basi uwe umeelewa alichokuwa anasimamia. Ni ushauri wa bure tu.
 
MKJJ,

Oh yeah, come to think of it; the whole lot began with CCM, when they diverted from their core business to being a gang of looters, a syndicate: from CCM to Chama Cha Majambazi and now Chama Cha Mafisadi.

Haiwezekani kwa mtuhumiwa kujifanya yeye ndiye mpelelezi mkuu... kutakuwa na haki hapo? Let others prosecute. Such a common law our lawmakers are failing to comprehend. Our parliament is such a cheap place where only the dumberer can inhabit... A sane person person can never dare to stand up for the dirt in there...

This topical appeasement by JM is meant to confuse and disorient, so that the focus is diverted, and with others (Serukamba, Chitalilo) contributing to the chaos, the scene becomes muddled, and that's what they want.

Unfortunately Ufisadi has become such a sticky issue and has refused to follow the 7-day rule for news in the media:

Mpaka Kieleweke!

very good...! at least umefikiria!
 
There are people caught up in this Opposition vs CCM race for brownie points.

To some the opposition can do no wrong, to some CCM can do no wrong.This is exactly the sort of thinking that start a nonsensical and precious time consuming debate on "who started the EPA saga", pointlessly partisan puckering.

I abhorr such idealism, the priority should be solving problems, not politicking for brownie points.

I agree! The main challenge here is how to solve the problem with the kinds of Malecela pulling the shots. I would welcome the idea of a drastic shift/change of the mindset of Tanzanians but that is an idealistic wish coz the opium of CCM is stuck with them!
 
kumbe wewe hapa unapachukulia kama kijiwe ndio maana unatoa kauli unazotaka mwenyewe eee!

kumwita mtu "mnafik" unaona kauli safi wakati mtu hajakukera pahali. acha hizo dogo. haipendezi.
Msimamo wangu kuwa mafisadi wakamatwe ndio msimamo wa wananchi!
sasa nyie mnaotaka kuni attack personally mtaumbuka!
Nakufahamu gaijin!
Najua una ushabiki wa watu flani flani!
Mimi sina!
Niko hapa kwa wakati wa Mungu!
Nakata issues!
Ningekuwa na haja ningekuwa nawapigia simu hao vigogo kama wengine wafanyavyo!
Sina haja hiyo kwasababu nimezisoma RIPOTI ZOTE NA SASA UKWELI UMWENIWEKA HURU!
MAFISADI WAKAMATWE MARA MOJA!
 
Tunze kukata issue sasa...Nani ni nani,anataka nini na kwanini!
Pia tunajua yote sasa!
Tuachane na mambo ya vyama vya kisiasa enyi VIJAKAZI!
Nasikia huruma lakini NAWAONEA HURUMA WANANCHI ZAIDI KWASABABU NINA EMPATHY!
 
Mwanakijiji kasema wapi hiyo kauli?
Hapa kuna wanao pigania maslahi ya chama.
Yeye anadai ccm ndio wapewe mustakabali wa nchi!Nasema NO NO NO!


Hebu onesha huo muda wa Mungu ulionao kwa kunionesha ni wapi na lini nilipodai kuwa "CCM ndio wapewe mustakabali wa nchi"? Ukinionesha nitasema kweli mwenzetu umetumwa na Mungu wa Ibrahim, Isaki na Yakobo!
 
Ni ufukara wa mawazo kuyafanya maslahi ya taifa mtaji wa siasa za ccm. Ukweli kama wao ndio waliokuwa waanzisha mwendo leo tusingekuwa tunajadili suala hili, kwani wao wana majeshi, mahakam, polisi na magereza. Ila kwa kuwa wao sio waanzisha mwendo ndio maana imekuwa vigumu kuwashughulikia wenzao waliofikisha nchi hapa ilipo kwa kutumia vyombo nilivyovitaja hapo juu. Ni ukweli usiopingika kuwa Mugabe na ZANUPF hakuwa kama walivyo leo; walianza taratibu kuwadanganya wananchi na kuwashinikiza pale walipoona imeshindikana, wamenza kutumia vyombo nilivyovitaja hapo juu dhidi ya wananchi na wenye kudai mustakabali wa nchi yao. Ni ukweli usiopingika kuwa Mafisaidi hawana tofauti na Mugabe! Nadhani ingekuwa busara kwa Kina Malecela na wengine waliochoka wakae kando, wasidhani hii nchi ni yao!!!!
 
Wadau, hoja ya ufisadi kila mmoja anajua ilianzishwa na nani, wana jambo nadhani tulikuwa wa kwanza kabisa kuiona orodha ya mafisadi kama ilivyowasilishwa na mdau FMES.

Malecela aka Tingatinga ni mjanja sana na baada ya kuwa amejeruhiwa na wanamtandao anachofanya ni kuuma na kupuliza. Na kama mnavyojua CCM wako macho sana na yeye, kitendo cha kumshambulia Dr Slaa kina maana yake na kisichuliwe kama kweli amekitoa akiwa anajua nini na nani ni waanzilishi wa hoja ya mafisadi.

Mhe Chitalilo nadhani naye anapaswa ajitazame kwanza kama anataka kuwaambia wengine wanaonekanaje. Tunamjua na nikiwa mtu ninayetoka jirani kabisa na jimbo lake najua wapigakura wanamsema namna gani, kifupi mbinu alizotumia (ambazo zilitumiwa na namba nzuri ya wabunge wa CCM) zilikuwa za kifisadi hata kama zililazimishwa zionekane ni Ukarimu wa Kiafrika.

Kwa sasa umma uko makini na TBC walidhani kwa kutorushwa hewani hoja za dr Slaa jioni walijua watanzania aka umma hautajua nini kinaendelea, wanajua na sasa wanapima na wanatambua kabisa kuwa wabunge wengi wa ccm ni wawakilishi wa 'wapigakura' na wala si wawakilishi wa umma, kifupi namba kubwa miongoni mwao ni mafisadi kwa namna moja ama nyingine, wengi wameshiriki na kwa kukaa kimya wanaonesha kukubaliana na ufisadi.

Japo hoja zimeanzishwa na wapinzani ambao Mkullo amewaita wabunge makini lakini umma tunafurahi kwamba kina Kilango, Nyalandu, Sendeka, Kimaro na wengine toka ccm wameweka uchama pembeni na kufanya kile kinachomaanisha BUNGE yaani Kuhoji, Kuwakilisha umma na kuisimamia serikali



Ufisadi hautokani na mtu bali mfumo ambao watu hao wamo, itikadi isipofuatwa basi jua linakuchwa
 
Jmushi.. ninapokushawishi usome mtu alichoandika na ufikiri kabla hujatamka ninataka kukusaidia upolish ujengaji hoja wako. Kudai kuwa mimi "nimedai" CCM ipewe nchi ni uzushi wa wazi kwa sababu kama ungefuatilia maandishi yangu hutaona mahali hapa pamoja nimewahi kusema kitu kama hicho au hata kukiashiria! Lakini well, huwezi kukanusha na kusema "niwie radhi". Unaamini unachoamini hata kama hakina msingi na uko tayari kukisukumiza kooni alimradi usikubali kuzusha.

Ushauri wangu, kama huelewi mtu kasema nini au una wasiwasi unaweza ukamnukuu vibaya muulize akueleweshe ili utakapoamua kumpinga basi uwe umeelewa alichokuwa anasimamia. Ni ushauri wa bure tu.

Nilifungiwa kwa kusema Kikwete ni MAFIA!
Tena ulikiri wewe ndiye uliyechukia mimi kusema hivyo!
Niliomba msamaha nikarudishwa!
Kesho yake...Swahiba wako mkuu MWAFRIKA WA KIKE..
Akaniibulia tuhuma kuwa nimesema tumwage damu!
Nikasema tena sikuambiwa hivyo na wala hakuna mahali niliwahi kusema hivyo!
Akaingia mitini!
Msimamo wangu umeshajulikana na wengi na hakuna atayeweza tena kuwapotosha wale wana jf wanaoelewa nia yangu halisi kuwa...
HAKI NI SHERIA!
 
Hebu onesha huo muda wa Mungu ulionao kwa kunionesha ni wapi na lini nilipodai kuwa "CCM ndio wapewe mustakabali wa nchi"? Ukinionesha nitasema kweli mwenzetu umetumwa na Mungu wa Ibrahim, Isaki na Yakobo!

Kwa kumsapoti KIKWETE AMBAYE NI MWENYEKITI WA ccm!
Na kumsapoti Mama Killango aliyeteuliwa na baadhi ya wana ccm wenye nia zao!
Mama Killango aliyeshirikiana na MAFISADI KUPITISHA BAJETI YA KIFISADI!
Halafu kwa kuipa kipaumbele issue ya ZIMBABWE WAKATI HUU MUHIMU KWA TAIFA LETU!
Hivi wewe MKJJ hujui wakati tulionao?
HUJUI NCHI IMEUZWA NA WANANCHI WAKE WAKIWAMO?
UNAPIGANIA UHURU WA ZIMBABWE...SISI TUKO HURU?
 
NA KAMA TUKO HURU...NANI ALIMPA SINCLAIR RIPOTI YA MADINI KABLA YA WAZALENDO!?
Kwa tafsiri kamili hapo juu...UHURU TULIO NAO NI UPI HUO?
 
This is what Malecela said yesterday.

MHE. JOHN S. MALECELA: Mheshimiwa Naibu Spika, napenda kukushukuru sana kwa kunipa nafsi hii ya kuwa msemaji wa kwanza katika mjadala huu wa Ofisi ya Waziri Mkuu, kama alivyoiwasilisha leo asubuhi.

Mheshimiwa Naibu Spika, kwanza nataka kuchukua nafasi hii kumpongeza Mheshimiwa Waziri Mkuu, na kumuhakikishia kwamba Chama Cha Mapinduzi, na watanzania wote watakuwa naye bega kwa bega katika kuona kwamba sera za Chama Cha Mapinduzi, zinatekelezwa kwa ukamilifu kama tulivyozipanga na kwamba sisi Wabunge, tutampa kila ushirikiano. Na lazima niseme hili kweli, kwamba Waziri Mkuu, umeanza vizuri na endelea hivyo. Waheshimiwa Wabunge, ningependa niwarudishe kwenye ajenda ya sasahivi nayo ni hotuba ya Waziri Mkuu, akiwasilisha mapato na matumizi ya Ofisi yake. Kwasababu haya mengine yote yaliyosemwa tunaweza tukayachukua kama ajenda ya siku nyingine, lakini kwa leo tuna ajenda ya hotuba ya Waziri Mkuu. Narudia tena hotuba ya Waziri Mkuu (Makofi).

Mheshimiwa Naibu Spika, baada ya kumpongeza Mheshimiwa Waziri Mkuu, ningependa na mimi niseme moja au mawili. Ninataka kulihakikishia Bunge hili na watanzania wote kwamba Chama Cha Mapinduzi, kamwe hakitaficha maovu. Ya kwamba Chama Cha Mapinduzi, kila mara kitakuwa katika mstari wa mbele wa kuona kwamba uovu unaondolewa katika nchi yetu. Twende kwenye hatua za kweli, nani aliyeyaleta haya mambo ya EPA mara ya kwanza? Alikuwa ni Dokta Chegeni, wa Chama Cha Mapinduzi, kutoka Jimbo la Busega. Halafu jambo la pili nitoe mfano tu juzi hapa nyinyi wenyewe mliona Chama cha Mapinduzi, Mheshimiwa Mbunge wa Same Mashariki amesema kwa nguvu zake zote tunaye Mheshimiwa Mpendazoe Fred Mpendazoe Tungu, Mbunge wa Kishapu amesema kwa nguvu. Kwa hiyo ninataka niwahakikishie hata mimi ninarudia tena, hela za EPA zitarudi, lakini nataka nisem

Mheshimi Naibu Spika, ndiye aliyeyaona maovi haya na yeye ndiye aliyeunda hiyo tume ambayo tunasomewa hapa vipande na akaahidi kwamba itakapokuwa tayari ataileta kwenye Bunge hili tuje tuizungumze kihakika. Sasa mimi nashangaa kwamba kitu ambacho Rais alikiunda na tunamshukuru sana na tunampongeza kwamba alichukua hatua ya Chama cha Mapinduzi kupambana na ufisadi na akasema kwamba hela zote lazima zirudishwe chini ya EPA na ripoti italetwa Bungeni tutaizungumza, sasa wenzetu kama wanataka wangoje naona wanafanya haraka mno ..................................

KUHUSU UTARATIBU

MHE. CHACHA Z. WANGWE: Mheshimiwa Naibu Spika, kuhusu utaratibu.

NAIBU SPIKA: Kuhusu utaratibu, naomba nataka kusikiliza kuhusu utaratibu.

MHE. CHACHA Z. WANGWE: Mheshimiwa Naibu Spika, Kanuni ya 68.

NAIBU SPIKA: Soma, naomba uisome Kanuni.

MHE. CHACHA Z. WANGWE: Kama huna kanuni wewe shauri yako. (Kicheko/Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, ningependa kujua kama ni utaratibu kuzungumzia ................................... (Kicheko/Makofi)

NAIBU SPIKA: Waheshimiwa Wabunge, tafadhali soma.

MHE. CHACHA Z. WANGWE: Mheshimiwa Naibu Spika, nitaisoma wengine hapa hawasomi, Kanuni ya 68 inasema, Mbunge anaweza kusimama wakati wowote na kusema maneno kuhusu utaratibu ambapo Mbunge yeyote ambaye wakati huo atakuwa anasema atanyamaza na kukaa chini, na Spika atamtaka Mbunge aliyedai utaratibu ataje Kanuni au sehemu ya Kanuni iliyokiuka. (Kicheko/Makofi)

NAIBU SPIKA: Sasa ndiyo hiyo taja sasa. (Makofi)

MHE. CHACHA Z. WANGWE: Kanuni ambayo imekiukwa ni Kanuni ya 68 (7) inasema, hali kadhalika Mbunge anaweza kusimama wakati wowote ambapo hakuna Mbunge mwingine anayesema. (Kicheko/Makofi)

NAIBU SPIKA: Mheshimiwa Mbunge naomba usipoteze muda, Mheshimiwa Mbunge .............................. (Kicheko/Makofi)

MHE. CHACHA Z. WANGWE: Mheshimiwa Spika, ngoja ............................... (Kicheko/Makofi)

NAIBU SPIKA: Mheshimiwa kaa chini. (Kicheko/Makofi)

MHE. CHACHA Z. WANGWE: Mheshimiwa Spika, naomba unilinde nimalize. Kama ni sahihi kuzungumzia mwenendo wa Rais ………………… (Kicheko/Makofi)

NAIBU SPIKA: Mheshimiwa Mbunge nimesimama naomba ukae chini. Mheshimiwa Chacha Wangwe Spika akisimama unatakiwa Mbunge ukae chini na Kuhusu Utaratibu ni vizuri ukajiandaa halafu unaenda kwenye ……..……..……, tumeshapoteza dakika tano, kwa hiyo naomba aliyekuwa anazungumza aendelee. (Makofi)

MHE. JOHN S. MALECELA: Mheshimiwa Naibu Spika, nakushukuru sana na ninapenda niendelee. Kama nilivyokuwa nikisema CCM kamwe haitalinda ufisadi na tutapambana na ufisadi kwa nguvu zetu zote na mimi nina hakika sisi wote tutamuunga mkono kama Rais wetu alivyosema kwamba hela za EPA zirudi na zitarudi na zisiporudi ni kweli kwamba tutakuwa na haki ya kuuliza kwa nini hazikurudi. Lakini mimi nina imani na Rais wetu na kwamba akishasema yale aliyosema nina hakika yatatekelezwa. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, nashukuru kwamba viti vya Bunge letu vimesimikwa kwa bolt, otherwise kwa hali ya namna hii kusimama tu mtu hata hana pointi na wala hajui ile order ni namba ngapi, katika Mabunge mengine watu huinua viti halafu kuanza kutupiana. (Kicheko/Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, ………………….

KUHUSU UTARATIBU

MHE. CHACHA Z. WANGWE: Kuhusu utaratibu.

NAIBU SPIKA: Kuhusu utaratibu, kifungu namba gani?

MHE. CHACHA Z. WANGWE: Mheshimiwa Naibu Spika, kifungu namba 64 katika e inasema, hatazungumzia mwenendo wa Rais, Spika, Mbunge, Jaji, Hakimu au mtu mwingine yeyote anayeshughulikia utoaji wa haki isipokuwa tu kama kumtolea hoja mahususi kuhusu jambo fulani. Sasa msemaji alikuwa anamzungumzia Rais na mwenendo wake kuhusiana na suala la EPA.

Je, hajavunja hiyo? (Kicheko/Makofi)

NAIBU SPIKA: Waheshimiwa Wabunge naomba mnisikilize, nadhani tunayo kazi kubwa ya kuweza kusoma kanuni. (Makofi)

Kwa hiyo swali la kumzungumzia Rais, anasema Rais ameahidi kwamba anameunda tume ambayo ina miezi sita na alichosema msemaji mimi nimesikia kwamba atakapotoa Rais kama hatujaridhika ndio tutauliza, sasa hapa hajamsema Rais, naomba tuendelee mzee. (Makofi)

MHE. JOHN S. MALECELA: Mheshimiwa Naibu Spika, nina matumaini yangu kwamba muda nitaongezwa.

NAIBU SPIKA: Unaongezwa.

MHE. JOHN S. MALECELA: Mheshimiwa Naibu Spika, lakini huyo ni Makamu wa Mwenyekiti wa Chama cha CHADEMA sishangai, ninaendelea. (Kicheko/Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, sasa ningependa kwenda kwenye suala la Serikali la Mitaa, ..................................

KUHUSU UTARATIBU

MHE. CHACHA Z. WANGWE: Kuhusu utaratibu. (Kicheko/Makofi)

NAIBU SPIKA: Mheshimiwa Mbunge naona sasa tunaanza kutumia nyumba vibaya, tunaanza kutumia nyumba vibaya kwa sababu hakuna alichokisema Mzee Malecela toka wakati ule.

MHE. CHACHA Z. WANGWE: Mheshimiwa Naibu Spika, kipo hapa.

NAIBU SPIKA: Wewe siyo Makamu Mwenyekiti.

MHE. CHACHA Z. WANGWE: Mheshimiwa Naibu Spika, maana unamlinda sana, usimlinde zaidi ya mahitaji. (Kicheko/Makofi)

NAIBU SPIKA: Haya tunaendelea, mzee Malecela unaendelea, kwa sababu sasa tunafanya utani ndani ya Bunge hili, naomba tuendelee naona sasa tunafanya utani. (Makofi/Kicheko)






MHE. JOHN S. MALECELA: Mheshimiwa Naibu Spika, ninaendelea kama nilivyokuwa nasema sasa nataka nije kwenye suala la Serikali za Mitaa. Watanzania na Waheshimiwa Wabunge wenzangu mtakumbuka kwamba tangu mwaka 1974 tulishughulika sana kuunda vijiji na haja yetu ilikuwa kwamba kuwaleta wananchi wetu pamoja ili tuweze kuwapa maendelea, sasa mimi kwanza pendekezo langu la kwanza ningependa nimuombe Waziri Mkuu kwamba aunde katume ka watendaji siyo ka Wabunge hapana, ka watendaji waende wakaangalie hivi vile vijiji tulivyoviunda tukaambiwa viwe na Serikali na Serikali za vijiji zipo lakini je, zinaendesha mambo kama inavyotakiwa? Nia ya marehemu Baba wa Taifa ilikuwa ni kupeleka madaraka kwanza mikoani, wilayani na baadaye vijijini, je, tangu wakati huo ni madaraka gani tumepeleka huko vijijini na hayo madaraka yanatumiwaje?

Mheshimiwa Naibu Spika, kwa mfano mimi niseme Mheshimiwa Waziri Mkuu ni hakika kabisa kwamba sasa hivi vijiji vyetu vimekosa watu wa fani ya fedha, wamekosa fani ya fedha kwa hiyo hakuna mtu anayeshughulika na ukusanyaji wa mapato ya kijiji, matumizi yake na kuwaambia wanavijiji kama inavyotakiwa na sheria fedha zilivyotumika. Sasa mimi ningeomba jambo hilo liangaliwe sana, tuliwaahidi wananchi wetu tukiwapeleka vijijini vitu vikubwa vitatu maji, elimu na afya sasa je, tumefika kiasi gani? (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, mimi ningependa nianze kutoa dokezo Mheshimiwa Waziri Mkuu, wanavijiji wamejenga Shule za Msingi katika kila kijiji Tanzania na kwa kweli jambo hilo ni la kujivunia sana na hata tunapotaja takwimu za watoto walioenda darasa la kwanza, waliomaliza kidato cha nne ni kutokana na hiyo kwamba baadhi yao walianza kusoma chini ya mti lakini kwenye kijiji.

Mheshimiwa Naibu Spika, sasa mimi nadhani ni wakati umefika Serikali iangalie namna ya kuboresha Elimu ya Msingi, Serikali iangalie namna ya kuboresha Elimu ya Sekondari wananchi wamejitolea wamejenga shule, wamejenga nyumba za walimu sasa linapokuja suala hakuna madawati, walimu hawatoshi mimi nafikiri hilo linakuwa ni la kwetu. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, niende upande wa afya, ni kweli kwamba tamko lililotokea hivi karibuni kutoka Serikalini ni kwamba tunataka tuwe na zahanati kila kijiji, mimi nina hakika jambo hilo litawezekana kwa sababu tuliposema tuwe na Shule ya Sekondari kila kata sasa hivi ni kata chache ambazo hazina Shule za Sekondari lakini ningeomba safari hii maadam tumepanga hivyo, basi Wizara inayohusika iwe na vitu vifuatavyo. Kwanza, wananchi watakapoanza kujenga vile vitu ambavyo viko juu ya uwezo wao vitu kama mabati, vitu kama mbao hivi tuweze kuwasaidia na pili, tuhakikishe kwamba watumishi watakaoenda kwenye zahanati hizo waanze kutayarishwa sasa kwa sababu tuna vijiji zaidi ya 10,000 sasa kupata watumishi kwa vijiji vyote hivyo itakuwa ni vigumu kama hatukujitayarisha bado mapema.

Mheshimiwa Naibu Spika, mimi ningeomba kwamba kwa upande wa vijiji miundombinu, ni kweli sasa hivi mambo haya ya simu za mkononi yanaenea vizuri sana lakini mimi ningeomba hii miundombinu ya simu za mkononi angalau ziende katika kila kijiji kama itawezekana. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, tuje kwenye suala la barabara, nataka kwenda haraka kwa sababu muda wangu mwingi umechukuliwa, mimi nina hakika kama tukiunganisha vijiji vyetu na mabarabara ya kudumu hata suala la usafiri litakuwa jepesi, leo Dar es Salaam wamesema kwamba wao hawataki hivi vi-haice wanasema hivi vinaleta matatizo kwenye mji, sisi vijijini tutavihitaji kwa usafiri kutoka kijiji hadi kijiji lakini kwa sasa hawawezi kuja vijiji kwa sababu mabarabara hayapitiki vizuri.

Mheshimiwa Naibu Spika, lingine ningekuja kwenye upande wa kilimo, mara nyingi sana tunasema wakulima wetu kilimo chao bado ni kilimo duni, sasa kitaachaje kuwa duni ikiwa leo Mkoa wa Iringa, Mkoa wa Ruvuma, Mkoa wa Mbeya, Mkoa wa Rukwa kila siku kilio chao ni mbolea, kwanza haifiki kwa muda na mbolea haitoshi na nisisitize hasa lile kwamba mbolea haitoshi halafu tunamwambia mkulima ana kilimo duni, sasa hapa sijui ni vipi?

Mheshimiwa Naibu Spika, nikitoka hapo nije kwenye suala la mifugo, Mheshimiwa Waziri Mkuu kama kuna watu ambao kwa kweli wamesahaulika katika bajeti zetu mara kwa mara ni upande wa mifugo. Ningependa nisisitize kwamba wakati umefika wafugaji waangaliwe, wengi tunasema wenzetu Botswana wana mfugo mizuri na wanapata bei nzuri, ndiyo lakini ukienda utakuta miundombinu yote maji na kadhalika wanatengenezewa na Serikali, sasa sisi bahati mbaya katika Tanzania mifugo wanastawi katika sehemu zilizo na ukame Dodoma, Singida, Arusha, Shinyanga na kadhalika. Sasa kote humu mimi nilitazamia kama kweli tunataka kuwahudumia wafugaji basi suala la maji lingekuwa ni suala la msingi sana kwa binadamu na mifugo yao. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, upande wa madawa, kweli Serikali kama inaweza kutoa ruzuku kwa mbolea basi kwa nini isitoe ruzuku kwa madawa ya mifugo? (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, baada ya hapo ningependa tu kusema ninamshukuru sana Waziri Mkuu kwa hotuba yake tunamtakia kila jema na awe na hakika kwamba tutakuwa naye na tutamsaidia kuweza kufaulu na hasa katika kuleta maendeleo ya wananchi vijiji mwetu. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, naunga mkono hoja mia kwa mia. (Makofi)
 
Nilifungiwa kwa kusema Kikwete ni MAFIA!
Tena ulikiri wewe ndiye uliyechukia mimi kusema hivyo!
Niliomba msamaha nikarudishwa!
Kesho yake...Swahiba wako mkuu MWAFRIKA WA KIKE..
Akaniibulia tuhuma kuwa nimesema tumwage damu!
Nikasema tena sikuambiwa hivyo na wala hakuna mahali niliwahi kusema hivyo!
Akaingia mitini!
Msimamo wangu umeshajulikana na wengi na hakuna atayeweza tena kuwapotosha wale wana jf wanaoelewa nia yangu halisi kuwa...
HAKI NI SHERIA!

Mambo ya Isaiah Washington wa Grey's Anatomy hayo.

I did not call him a faggot!
 
Malecela nyie mwacheni alikuwa anatafuta jinsi ya kuktetea wife.Isitoshe inabidi tujiulize beef la mke wa MAlecela Mke wa Mwenyekiti Mstaafu wa CCM na Mke wa Msekwa Mwenyekiti wa Sasa Wa CCM.Hapo kuna kitu......LADBA KWA MSISITIZO NAWEZA KUWAKUMBUSHA KUWA WAKATI SWALA LA EPA LINALETWA BUNGENI NA LA ZITO KABWEPIA KUHUSU KARAMAGI CCM WALIKAA KIKAO NA KUWEKA MIPANGO KAMAMBE YA KUWAMALIZA WAPINZANI,NDO AKAANZA YULE ALIYEKATWA MKONO(MUDHIHIRI) AKAJA MAMA MANYANYA STELLA HUYU ALIKUWA HAJAPANGWA ILA WALIJUA KAMA KAWAIDA YAO WANAWAKE KUWATETEA WAKUBWA ZAO AKAWAGEUKA.NDIPO WAKMSIMAMISHA MKUBWA WAO MALECELA AKAMALIZA KWA KUSEMA WAKINA ZITO NA WENZAKE NI WAHONGO NA WAFUKUZWE BUNGENI,Kwa ufupi isingekuwa kauli ya MAlecela Zito asingefukuzwa Bungeni.Pengine labda Uzee unamsumbua anasahau...Lakini Uzee waliaema Ni DAwa....
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom