Elections 2010 Malecela ahofia CCM kuwa katika hali ngumu 2010

CCM ni Chama cha Mafisadi, na ambaye anaupinga ufisadi basi huyo si Mwana CCM halisi.Huu ndiyo ukweli wenyewe na wala haupingiki. Wapo baadhi ya wana CCM wachache ambao wanaokerwa sana na tabia hii mbaya ya ufisadi wa mali za umma, lakini wanakosa platform ya kuzungumzia kero zao kwa kuhofia kufanyiwa yale waliyo fanyiwa marehem Hores Kolimba na Prof Kighoma Malima. Baada ya ukweli kudhihiri na uwongo kujitenga, Malima alijitoa ndani ya CCM na kuanzisha kambi yake ya upinzani dhidi ya CCM. Alipokwenda nchini Uingreza kwa ziara binafi(inasemekana alikwenda tafuta misaada ya kisiasa), makachero wa CCM nawo wakapanda ndege na kufuatilia nyendo zake na walipowasili huko walijifanya ni waandishi wa habari na hivyo kumfuata mojakwamoja hotelini alikofikia na kumuhoji mahojiano bandia huku wakijua walichokuwa wamedhamilia kukifanya zidi ya uhai wake. Baada ya masaa machache tu kupita Prof Mlima aliripotiwa kuwa amefariki kwa ugonjwa wa pressure ya moyo. Kwa upande wake Kolimba, mambo ni karibu sawa na yaleyale aliofanyiwa mwenzake. Akiwa ndani ya ukumbi wa Bunge huko Dodoma, alianguka chini na kufariki dunia baada ya nukta chache tu za kukamata kipaza sauti kinachodawi kuwa kilikuwqa kimeandaliwa rasmi kwa yeye Kolimba kukitumia wakati wa kujitetea kwake pale aliposhutumiwa kwa kusema CCM ilikuwa imepoteza muelekeo wa kisiasa. Kwahivyo, kwa mifano hiyo michache, yatosha kuwa ni vikwazo halisi kwa wana CCM wapenda haki kueleza bayana dukuduku zao dhidi ya wenziwao wasiopenda haki na usawa katika nchi hii ya Tanzania. Kila mtu anazingatia ule msemo maarufu wa kiswahili usemao YARAABI NAFSI!!!!!!!!!!! nahivyo kuifanya agenda nzima ya ufisadi kuwa ni swala nyeti na la siri ndani ya CCM. MPO HAPO WA BONGO!!!!!!!!!!!!!!? HUU NDIO UKWELI HALISI NA SABABU HASWA YA USIRI WA UFISADI NDANI YA CCM.
 
Last edited:
Mwalimu aliwahi kuita wapinzani wa CCM mbwa ama kuwalinganisha na Mbwa kuchukua Nchi ila sasa nadhani huko aliko anaona kwamba alitete mbwa na CCM yake iko mikononi mwa mbwa .
 
*ASEMA NCHI INA UFISADI WA KUTISHA, ATABIRI UGUMU KWA WABUNGE 2010
Na Ramadhan Semtawa

SPIKA wa Bunge, Samuel Sitta amejitosa katika mjadala ulioanzishwa na makamu mwenyekiti wa zamani wa CCM, John Malecela, akisema ufisadi nchini umefikia kiwango cha kutisha kutokana na baadhi ya watu, wakiwemo wanasiasa kuwa na utajiri ambao vyanzo vyake havina maelezo.

Wiki iliyopita Malecela alikaririwa na vyombo vya habari akisema kuwa suala la ufisadi litawaweka pabaya wabunge wengi wa CCM kwenye uchaguzi mkuu ujao wa mwaka 2010, huku akisema baadhi ya wabunge wanaweza kupoteza viti vyao kutokana na kutoenda majimboni na kutofuata ilani ya CCM.

Kauli hiyo iliibua mjadala baada ya katibu mkuu wa chama hicho tawala, Yusuf Makamba kumjibu mkongwe huyo akisema haoni mafisadi wala ugumu kwa chama kushinda mwakani, huku Naibu Waziri wa Kazi Ajira na Maendeleo ya Vijana, Dk Makongoro Mahanga akiibuka na kusema mafisadi ndani ya CCM ni wanne tu.

Jana Spika Sitta, akizungumza na Mwananchi kwa simu akiwa Entebe, Uganda, alisema ufisadi uliopo sasa nchini unatisha na akatabiri ugumu kwa baadhi ya wabunge kurejea kwenye chombo hicho cha kutunga sheria.

"Ahaa... mimi ninachofahamu suala si kusema kuna mafisadi wanne ndani ya chama au wangapi, tunazungumzia suala zima la kuporomoka kwa maadili ya uongozi," alisema Spika Sitta ambaye zaidi ya wiki moja iliyopita aliomba kuongezewa ulinzi akidai kuwa wapinzani wake wa kisiasa wanamuandama, akiwatuhumu kuwa ni mafisadi.

"Unaponiambia sijui kuna mafisadi wanne sikuelewi. Hivi sasa kuna ufisadi mkubwa, watu wana utajiri wa kutisha ambao maelezo yake hayaeleweki.

"Kwa mwanasiasa wa kawaida kuwa na utajiri wa kutisha, inatia mashaka sana."

Sitta, ambaye alijinadi kuwa bunge lake litakuwa la "kasi na viwango" mara baada ya kuvishwa joho la uspika, alisema kuporomoka kwa maadili ndiko kunakofanya kuwepo mafisadi kuanzia ndani ya chama.

"Hivi sasa hakuna miiko ya uongozi ndiyo maana kuna ufisadi wa kutisha, zamani kulikuwa na miiko ya uongozi," alisisitiza.

Aliongeza: "Kwa mfano, mimi nilikuwa mtumishi wa umma kwa miaka 40, lakini nisingeweza kuwa na utajiri kama baadhi ya watu walivyo, sasa iweje mwanasiasa tu wa kawaida uwe na utajiri wa ajabu?" alihoji.

Alisema hata kama wapo wanasiasa wafanyabiashara, bado kuna mashaka na utajiri wao.

"Unaweza kukuta mtu ana magari ambayo idadi yake inatisha; ana majumba mikoani na fedha za ajabu. Utajiri huu unatoka wapi kwa mtu mwanasiasa tu,"alihoji.

Alisema watu siku hizi wanaangalia haki binafsi badala ya maslahi ya umma, ndiyo maana hata baadhi yao hushiriki katika mikabata mibovu ya kifisadi.

"Mtu anachungulia atapata nini katika mkataba fulani, anasahau kabisa maslahi ya jamii,"alisema Spika Sitta.

Kuhusu kauli nyingine ya Malecela kwamba wabunge wa CCM wanaoishi mijini watakabiliwa na wakati mgumu mwakani, alijibu: "Hilo liko wazi.'

Spika alisema siku zote mbunge awe wa CCM au wa chama cha upinzani ambaye haendi jimboni kwa wapigakura wake, ana wakati mgumu kutetea kiti chake.

"Sijui kama wabunge wa CCM ambao watakabiliwa na ugumu jimboni ni wengi au wachache, lakini mbunge yoyote ambaye hayuko karibu na wapigakura wake mwakani atakuwa katika wakati mgumu," alisisitiza.

Alisema kwa kawaida mbunge anapaswa kuwa karibu na wapigakura wake ili kushiriki katika mambo mbalimbali, yakiwemo ya kijamii.

Alisema kuna mambo ya ndani ambayo wananchi wanaamini mtu pekee wa kumweleza ni mbunge, sasa asipokuwa karibu na wapigakura lazima utapata wakati mgumu tu mwakani.

Kuhusu utekelezaji wa ilani ya chama, alisema: "Hilo kwa sehemu kubwa linapaswa kutekelezwa na serikali na imekuwa ikifanyika hivyo, lakini mbunge lazima ufike jimboni."

Pamoja na mambo mengine, Malecela alisema: "Vita dhidi ya mafisadi ni ngumu kwa sababu ndani ya CCM kuna baadhi ya watu wanaokichafua chama kwa tabia zao za kuungana na mafisadi."

Mzee Malecela aliwasha moto huo wakati tayari kukiwa na mvutano mkubwa ndani ya CCM baina ya kambi inayopambana na ufisadi, ambayo imekuwa ikijionyesha waziwazi na ile inayotuhumiwa kuwa ya ufisadi ambayo vita vyake vinaonekana kuwa vya chinichini.

Malecela, mjumbe wa kudumu wa Kamati Kuu ya CCM, alienda mbali zaidi alipoonya baadhi ya wabunge kwa tabia zao za kutokwenda kwenye majimbo yao na kwamba, hawafuati ilani ya uchaguzi ya chama hicho.
source......Mwananchi Date::8/10/2009
 
Last edited:
* watu wana utajiri wa kutisha ambao maelezo yake hayaeleweki.

"Kwa mwanasiasa wa kawaida kuwa na utajiri wa kutisha, inatia mashaka sana."



"Unaweza kukuta mtu ana magari ambayo idadi yake inatisha; ana majumba mikoani na fedha za ajabu. Utajiri huu unatoka wapi kwa mtu mwanasiasa tu,"

Wakuu serikalini kuna mambo makubwa ambayo watu wa kawaida kama mimi hatuyajui na hatutayajua mpaka wenyewe kwa wenyewe wayaseme..........huyu jamaa kusema hivi sio kwamba ana uchizi anajua na aliona na anayaona, kama kweli anayoyasema sio kwamba anajaribi kujiosha i mean kujipendekeza kwa wananchi basi ...THINGS WILL FALL A PART one day.....lets see..
 
Alichosema Sitta ni ukweli mtupu, ila tu kwenye hiyo list inabidi aweke na jina lake. Hizo mali alizo nazo amezipata wapi kwenye siasa?
 
Geofrey Nyang'oro

MJUMBE wa baraza kuu la taifa la CCM, Hussein Bashe amesema amesikitishwa na kitendo cha wajumbe wa halmashauri kuu ya chama hicho kuzungumzia masuala ya chama nje ya mkutano mkuu, akisema huo ni udhaifu.

Akizungumza wakati wa ufunguzi wa semina ya siku moja iliyowakutanisha wajumbe wa Jumuiya ya Umoja wa Vijana wa CCM (UV-CCM) kutoka Jimbo la Kinondoni jijini Dar es Salaam na jimbo la Kikwajuni Zanzibar, Bashe alisema kuzungumzia suala la chama nje ya vikao ni udhaifu ambao usipokemewa utakifikisha chama hicho pabaya.

"Hawa wanaokitabiria chama mabaya kwenye chaguzi zijazo ni wajumbe wa NEC, wao wana nafasi ya kuingia kwenye vikao na kuyazungumza haya. Inakuwaje leo wazungumzie uchochoroni,"alihoji na kusisitiza: "Sisi vijana wa CCM tunao wajibu wa kukipinga kitendo hiki kwa nguvu zoeti."

Alisema kama suala hilo litaachwa liendelee, watakaoteseka ni vijana ambao wana muda mrefu wa kuendelea kukitumikia chama hicho.

"Ndugu zangu hili ni jambo la kusikitisha sana kuona watu wenye nafasi ndani ya vikao vya halimashauri kuu wakilizungumzia suala hilo uchochoroni kama tutaacha liendelea sisi ndio tutakaotaabika,"alisema Bashe.

Kauli hiyo imekuja wakati makamu mwenyekiti wa zamani wa CCM, John Samuel Malecela akiwa aimekitabiria chama hicho kukumbana na wakati ugumu kwenye uchaguzi mkuu ujao kutokana na kukithiri kwa tuhuma za rushwa dhidi ya wabunge wa chama hicho, huku Katibu Mkuu Yusuf Makamba akipingana na kauli hiyo kwa madai hakuna mafisadi ndani ya CCM.

Lakini Bashe alisema jana kuwa vigogo hao wanaozungumzia masuala ya chama uchochoroni wakati wao ni wajumbe wa halmashauri kuu ya CCM na wana mahali pa kuzungumzia, ni dhaifu na wanataka kuuingiza udhaifu huo ndani ya chama

Aliwataka vijana ambao alisema kuwa ndio nguvu kazi ya taifa, kusimama kidete na kupinga vitendo hivyo.

"Kitendo hiki kinasikitisha sana uliona wapi baba na mama wanatoka na kwenda kugombania barabarani sisi vijana ndio wengi ndani ya chama na tunapaswa kupinga vitendo hivi kwa nguvu zote," alisisitiza.

Kuhusu Muungano, Bashe aliwataka watu wanaojadili kuwa utavunjika, kuacha fikra hizo na badala yake wazungumzie namna ya kuuboreshe.

Alisema kasoro zilizopo ndani ya Muungano zinazungumzika na kwamba kama kunamtu anayefikiri kuuvunja muungano nibema akachana na fikra hizo na badala yake aachie wahusika wanaozungumzia suala hilo kufanya kazi yao.

"Kuhusu Muungano, kumekuwa na maneno mengi nawaomba vijana wenzangu tushiriki katika kuulinda Muungano wetu, watu wanaozungumzia kuhusu kuvunjika tuwaombe waache kauli hizo na badala yake wazungumzie namna ya kuuboresha," alisema Bashe.

Alisema kila kilichoundwa na binadamu kina kasoro zake lakini akabainisha kuwa kasoro hizo zinazungumzika na mwafaka wake unaweza kupatikana kupitia meza ya mazungumzo.

Semina hiyo iliyoandaliwa na vijana wa umoja huo wilayani Kinondoni na kuwashirikisha wajumbe kutoka Zanziba ilihudhuriwa na vijana 100, kati yao 60 wakitokea Kinondoni na waliosalia Kikwajuni.
source mwananchi Date::8/10/2009
 
Yeye hawezi kukurupuka tu ..anajua kuna watu wana mali nyingi kumzidi manake haya maneno ni makali sana tusimdharau.........
 
Wee mvutakamba,
Walishatuonya kuhusu kumsema mzee wetu kwa nini umethubutu?
Sasa unaona mashambulizi?
Masanilo asante kwa kutupa tahadhali. Hata hivyo message sent.

- Mkuu ni kweli message sent on both sides, tofauti ya hapa na zeutamu ni kwamba kule ukibandika matusi unashangiliwa sana na kuheshimika, lakini hapa JF unashnagiliwa kwa hoja muhimu kwa masilahi ya taifa.

- Mkuu Mchukia Ufisadi samahani sana kwa kukukwaza, ila the lesson ni kwamba ukiwa na hoja huhitaji ngonjera kama hizi zako na wenzako, wewe ni kuweka hoja tu.

Ila thanks for the debate na see yah! na I promise sitarudia tena.

Respect.

FMEs!
 
Binafsi namshukuru sana Mama Anna Kilango kwa kumpa au kumuambukiza Mzee JSM mtizamo MPYA kabisa juu ya UFISADI. JSM yule aliyekuwa WM na Makamu wa Rais sio huyu wa sasa. Nakumbuka vizuri alivyomshambulia Jenerali Ulimwengu alipoongelea RUSHWA ilivyokuwa imetamalika na kushika kasi wakati wa awamu ya pili. FMES, anayekuteua huwa hajui kila kitu kuhusu wewe na kuna nafasi nyingine ukiteuliwa unapwaya, unashindwa, zinakuzidi uwezo wako,....
 
Wakuu, inaonekana nyie (Mchukia Fisadi na Field Marshall), mnajadili Malacela na kuteuliwa kwake na Nyerere, bila kutia maanani Katiba na Sheria zinazohusu kuteuliwa au kuchaguliwa kwa viongozi.

Katiba ya Tanzania inampa powers Rais kuteuwa Watanzania kadhaa kuingia Bungeni. Sasa nadhani idadi ya Wabunge wa kuteuliwa ni 10. Wakati wa Nyerere idadi hiyo ilikuwa kubwa zaidi. Katiba hiyo hiyo inampa Rais uwezo wa kumteua Mbunge yeyote kuwa Waziri isipokuwa Waziri Mkuu ni lazima atokane na Wabunge wa kuchaguliwa na aidhinishwe na Bunge lenyewe kabla ya kuapishwa Waziri Mkuu.

Malacela kama mawaziri wengi wakati wa enzi ya Nyerere, alikuwa Mbunge wa kuteuliwa hapo mwanzo. Cleopa Msuya na Joseph Warioba pia walianzia kama wabunge wa kuteuliwa. Baadaye waliingia Bungeni kwa kuchaguliwa ktk majimbo yao na wakapata sifa ya kuteuliwa Waziri Mkuu.

Kwa hiyo kama kuna utata kwamba mawaziri wengine hawakustahili, jambo la kwanza la kufanya ni kutazama upya Katiba na Sheria zetu. Pia ni lazima kuhakikisha Rais anakuwa ni mtu anayeweza kutumia powers zake kushitisha uteuzi wa Waziri Mkuu au Waziri yeyote pale anaporidhika mhusika hatekelezi wajibu wake au siyo mwadilifu. The reason for the current crisis of leadership in our country is indecision and ineptitude on the part of those on top.They turn a blind eye to immoral behavior.

Ndio sababu tunaweza kuwa na kiongozi anayekiri hadharani kwamba mtu ambaye imedhihirika ni mhalifu, hakuwa na kosa! Ndio sababu tunaweza kuendelea na uongozi wa watu ambao hata jumuiya ya kimataifa imethibitisha kwamba ni mafisadi; na wao wenyewe wamekiri kuwa na marundo ya fedha yasiyolingana na mapato yao halali, wakiyaita eti ni "vijisenti". Wanatutambia sisi wananchi wanyonge kwamba Serikali yetu sii chochote ama lolote.

Wakati wa enzi za Nyerere, mteule wake yeyote aliyemtilia shaka juu ya uadilifu wake, aliondolewa ktk wadhifa wake kwa kufukuzwa au kwa kupewa nafasi nyingine ambapo hangeweza kuathiri sana maendeleo. Mtindo wa kusema eti mhalifu ni lazima apelekwe mbele ya mahakama kwanza na akipatikana na hatia, ndipo aachishwe kazi, utaangamiza taifa.

Chama tawala kimekumbatia wazee waliochoka na waliofilisika kimawazo na ni wang'ang'anizi wa madaraka kiasi cha kudhani wananchi hawaoni madudu yao ya ufisadi ktk parking meters au Ubungo Bus Terminal; na wengine wanadhani kwamba wanachama wa ccm hawawezi kuona mvurugano na ukwapuaji wa fedha za umma unaofanywa na viongozi wa ccm bila kuchukuliwa hatua.

Waendelee tu na kutowachukulia hatua hadi hapo wananchi watakapotamka "enough is enough" Oktoba 2010.
 
Unazani makongoro mahanga anaposema kuna mafisadi 4 tu kwenye CCM, je ni kweli...ni nani?

unazani ni hawa:
1. RA
2. AC, andre Chenge
3..........
4..........

je unazani ni hawa tu? wengine ni kina nani?

5. Sita??
6. Kingunge??
7. ......
.
.
.
.
.
.
.

tuwaweke wazi...
 
1. RA
2. LoWaSa
3. Mkapa
4. Chenge
5. Makamba
6. Mramba
7. Yona
8. Idrisa
9. Ruta
10. .....etc.....nk....

Wapambe wa ufisadi
1. Mahanga
2. Serukamba
3. Bashe
4. ....etc....nk....
 
Jamani Mzee Makamba ana nini? Nadhani unamwonea mzee wa watu. Hebu toa data kama unazo.
 
Back
Top Bottom