Elections 2010 Malecela ahofia CCM kuwa katika hali ngumu 2010

Kuna mtu anajua huyu mzee ataachi kiti cha Ubunge aka karithishwa huko kwao kama Zanzibar na ukoo wa Krume sasa ?
 
Kauli ambazo huwapa Ushindi CCM siku zote ni kama hizi hapa chini:-







Kauli kama hizi uweza kutolewa na Vichaa tu!

Hayo hapo juu niliyasema mapema:

Nawaoneeni huruma jamaa zangu subirini watu waamke waje wakute "MZEE" mmemsema vibaya. Hivi hamjui kuwa mzee huyu ni ifallible?
Bado kuna wengine watakuja baadaye nadhani bado wanambrief MUZEE response ya JF kuhusu kauli zake
 
Ni kweli inawezekana na namuomba sana Mungu iwe hivyo na naamini asilimia kubwa ya wabunge wa sasa hawatarudi kwenye nafasi hizo kwa kusindwa ila tuu kutakuwa na sura mpya ndani ya CHAMA CHA MAPINDUZI ambazo ndizo zitarejea

Itawezekana tu kukiwa na tume huru ya uchaguzi na vyombo vya dola kama polisi na UWT, JWTZ vilivyo neutral, yaani ni kwa ajili ya watanzania sio CCM. Vinginevyo huu ni mtego wa panya tinga tinga anauseti. Lower expectations ili oponents walale then siku ya mchezo waoneshe kilichomtoa kanga manyoya. Mchezo hauchezwi uwanjani (kwenye sanduku la kura) mchezo unachezwa mezani (kwenye kutangaza matokeo ya kura yaliyo kinyume na matakwa ya wapiga kura) na CCM ni wazuri kweli kwenye hili.

Hata siku moja siamini kama Tanzania kuna chama kitaishinda CCM iwe kwenye urais au wabunge kwa kuwa refa ni wao CCM na wachezaji ni wao CCM.
 
Mhuni tu huyu, hana jipya. Zee zima linasema kuwa wana mbinu mpya.

Hivi wizi ni kitu cha kujivunia mbele za watu na mbele ya wachungaji?


Nasema ni mhuni hana nyimbo mpya huyu.

Kambarage alikuwa sahihi kuhusu mhuni huyu!

- Mkulu wangu yaani a great thinker, hebu nijaribu kukuelewa na this post:-

1. Hivi kiongozi mhuni kama Malecela, anakuwa amechaguliwa na wananchi wa aina gani? Sio anaofanana nao? Sasa unafikiri in this case ya Mhuni Malecela, wananchi na viongozi waliomchagua Malecela kwenye uongozi wa taifa wanakuwa ni wa aina gani?

2. Kambarage hakuwa mhuni, sasa aliwezaje kufanya kazi kwa kumchagua mhuni Malecela, kuwa mpaka waziri wake wa nje? Na mpaka kuwa Makamu wa CCM, chama chake yeye mwenyewe Mwalimu? Eti si tumekubaliana kwamba Kikwete ni fisadi kwa sababu anaweza kufanya kazi na mafisadi bila tatizo? Au?

Anyways, samahani sana kama nitakuwa nimekukwaza na infact siku hizi Malecela mwenyewe alinikataza kufanya ninachofanya sasa, kwa hiyo I am out!

Respect.

Sauti ya umeme FMES!
 
Malecela.jpg


Makamu Mwenyekiti Mstaafu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Tanzania Bara, John Malecela, ametabiri kuwa wabunge wengi wa chama chake na wa upinzani wataanguka katika Uchaguzi Mkuu wa mwakani.
Malecela alisema kuwa kuanguka kwa wabunge hao kunatokana na kuwa wengi wanashinda wakitanua mijini na hawaendi kuwatembelea wananchi vijijini. Aidha, alisema kuwa hata CCM itakuwa na wakati mgumu wakati wa uchaguzi huo kwani wapinzani wameshajifunza mbinu mbalimbali zinazotumiwa na chama hicho katika chaguzi ndogo zilizopita tangu mwaka 2005.
 
*WASOMI WASEMA MALUMBANO YAO MTAJI KWA UPINZANI

Waandishi Wetu

KATIBU Mkuu wa CCM, Yusuf Makamba amepinga kauli ya makamu mwenyekiti wa zamani, John Malecela kwamba, chama hicho kitakuwa na wakati mgumu katika Uchaguzi Mkuu ujao.

Juzi Malecela alisema CCM itakuwa na wakati mgumu katika uchaguzi huo wa mwaka 2010 kwa sababu ya tuhumu nyingi za ufisadi na baadhi ya wabunge wake kushindwa kutekeleza ilani ya chama hicho ya mwaka 2005.

Kwa mujibu wa Malecela, vita dhidi ya mafisadi ni ngumu kwa sababu ndani ya CCM kuna baadhi ya watu wanaokichafua chama kwa tabia zao za kuungana na mafisadi.

Lakini, Makamba jana alisema ufisadi anaozungumzia Malecela kwamba utakisambaratisha chama hicho mwakani ni wa kufikirika kwa sababu mpaka sasa hakuna mwenye ushahidi unaodhihirisha kwamba fulani ni fisadi.

"Mimi siwajui hawa mafisadi. Hebu wewe nitajie jina la mtu mmoja ambaye una ushahidi kuwa ni fisadi," alisema Makamba.

Alipoulizwa kuhusu baadhi ya makundi ya mafisadi ambayo tayari yameanza kampeni ya kusambaza pesa za kuwaangusha kwenye majimbo wabunge walio mstari wa mbele katika vita dhidi yao, Makamba alisema, "siyo kweli ila ni jambo ambalo linakuzwa tu."

Makamba pia alisema Spika wa Bunge, Samuel Sitta atatetea kiti chake kwenye uchaguzi ujao licha ya mbunge huyo wa Urambo kudai kuwa kuna kundi la wabaya wake limeanza kujipitisha kwenye jimbo hilo kwa lengo la kumwangusha katika uchaguzi ujao.

"Kule (Urambo) nilipita, wananchi wengi bado wanampenda. Hakuna kipingamizi chochote, atashinda tu akiomba tena kugombea," alisema Makamba.

Hata hivyo, Makamba alisema kutakuwa na hali ngumu ndani ya CCM katika uchaguzi ujao wakati wa kipindi cha kura za maoni na kwamba wanaotetea nafasi zao watakuwa na wakati mgumu.

"Upinzani watakaoupata CCM utakuwa ni wa wenyewe kwa wenyewe ndani ya chama na siyo kutoka kwa vyama vya siasa vya upinzani.

Baada ya mchakato huo wa kura za maoni ambazo zitaiwezesha kupata wagombea wake, CCM watashinda kwa kishindo dhidi ya wagombea wa vyama vya upinzani," alisema katibu huyo wa chama tawala.

Makamba alifafanua kuwa, upinzani katika kura za maoni ndani ya CCM, utatokana na ongezeko la wanachama wenye sifa za kuwa viongozi ambao kimsingi sasa wanajipanga kugombea ubunge.

Alijigamba kuwa CCM ina hazina kubwa ya viongozi wenye sifa, jambo ambalo litawapa wakati mgumu wanachama kuchagua.

Hata hivyo, kauli ya Malecela ilionyesha wazi kuwa, ndani chama hicho mambo si shwari kutokana na kuwepo na vita kali baina ya wabunge wanaojinadi kuwa wanapambana na ufisadi na wale wanaotuhumiwa kuwa mafisadi.

Kundi la wabunge wanaojinadi kuwa wanapambana na ufisadi limekuwa likituhumu kuwepo kwa njama za mafisadi kuhakikisha wapambanaji wote wanashindwa kwenye uchaguzi ujao, huku kundi jingine likionekana kutotaka kujitokeza hadharani.

Kutokana na hali hiyo, Malecela, ambaye ni mume wa Anne Kilango ambaye anachukuliwa kuwa mmoja wa vinara wa vita dhidi ya ufisadi, alisema tuhuma hizo zitawaweka baadhi ya wabunge kwenye hali ngumu katika uchaguzi ujao.

Malecela pia alisema baadhi ya wabunge wamekiweka chama hicho kwenye wakati mgumu kutokana na kushindwa kwenda kwenye majimbo yao na kutofuatilia utekelezaji wa ilani ya chama chao.

Wakati Makamba akieleza matumaini hayo ya ushindi wa CCM mwaka 2010, baadhi ya wahadhiri wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, wamesema CCM imepasuka katika makundi matatu na kwamba mpasuko huo unaweza kutumiwa na wapinzani kama mtaji wa kisiasa.

Wakizungumza na Mwananchi kwa nyakati tofauti jana, wasomi hao walisema CCM ya sasa ni tofauti na ile ya Mwalimu Julius Nyerere kwa kuwa imegawanyika katika makundi waliyoyataja kuwa ni ya Mtandao, Mpasuko, na CCM Asili.

Profesa Mwesiga Baregu alisema mpasuko huo ni baraka kwa Watanzania kwa kuwa unaweza kuleta mapinduzi ya uongozi kwa kuwachagua wapinzani.

"Inaonekana kuwa ndani ya CCM kuna mpasuko ambao unaweza kukipeleka chama hicho kubaya na kusababisha kuwakwamisha katika uchaguzi ujao wa mwaka 2010," alisema Baregu na kukishauri chama hicho kujipanga upya na kuondoa makundi hayo.

Alifafanua kuwa kundi la Mpasuko limekuwa likipigia kelele vita vya ufisadi na kuitaka serikali kuwachukulia hatua wahusika.

Alisema kimsingi makundi ya CCM Mtandao na CCM Asili yanavutana kimaadili na mtazamo juu ya uongozi.

"Kundi la CCM Mpasuko likisukumwa na kusaidiwa, linaweza kuingia katika kundi la CCM Asili ambao wanataka maendeleo ya taifa na si kujinufaisha mmoja mmoja," alisema.

Alisema kutokana na hali hiyo, CCM inapaswa kuwa makini katika uchaguzi ujao ikijaribu kujenga utaratibu wa kurudisha imani kwa wanachama kwa kushughulikia matatizo mbalimbali yanayokikabili.

Kauli ya Profesa Baregu iliungwa mkono na Profesa Issa Shivji aliyesema kuwa, ni ukweli ulio wazi kwamba, hali si shwari ndani ya CCM kwa kuwa imeanza kulea makundi.

"Mpasuko upo ndani ya CCM, na hii inaweza kuwa faraja kwa wapinzani kwa sababu watayatumia matatizo ya CCM kama muda mwafaka kwao kupitisha sera zao kwa wananchi, jambo ambalo wanaweza kufanikiwa kupata ushindi, wakati huo ndani ya CCM kunaweza kusababisha matatizo," alisema Profesa Shivji, ambaye ni mwanaharakati wa masuala ya ardhi.

Aliongeza kuwa, kutokana na hali hiyo, CCM ina kazi ya kuyarekebisha matatizo yake ili wananchi waweze kurudisha imani kwa chama hicho kikongwe na kwamba, hilo litaweza kusaidia kupunguza mmomonyoko.

Alisema viongozi wana wajibu wa kushirikiana na wananchi wao ili kuhakikisha kuwa wanarekebisha mapungufu yao ili kukisaidia chama kupata ushindi katika uchaguzi ujao wa mwaka 2010.

Juzi, akikabidhiwa na Kanisa la Christian Mission Fellowship vifaa mbalimbali vya walemavu vyenye thamani ya Sh58 milioni, Malecela alionya kuwa, mafisadi wasipodhibitiwa watakisambaratisha chama.

Kuhusu uchaguzi hujao akasema: "Utakuwa mgumu kwa CCM hasa wabunge kwa sababu baadhi yao hawaendi majimboni na hawafuati ilani ya CCM. Ugumu mwingine upo katika suala zima la mafisadi," alisema Malecela na kuongeza:

"Vita dhidi ya mafisadi ni ngumu kwa sababu ndani ya CCM kuna baadhi ya watu wanaokichafua chama kwa tabia zao za kuungana na mafisadi." Habari hii imeandaliwa na Leon Bahati, Hussein Issa na Patricia Kimelemeta.

SOURCE: MWANANCHI.​

 
Kila mtu na aseme lake, hivi ni vita vya panzi. Kupingana kimtazamo tu inaonyesha CCM wenyewe hawajijuwi walivyo sasa au hawataki kukubali hali waliyonayo hivi sasa, Mzee Malecela kasema kweli, kwa kuwa hali ndivyo inavyo onekana kwa chama tawala hivi sasa, Makamba hataki kukubali kuwa huu ndio ukweli, anapingana na mtu ambaye nakijua chama nje ndani!!!
 
- Finally, CCM inaanza kuwa na demokrasia yaani kila kiongozi kusema maoni yake bila kutishiwa, sasa wahamishie kwenye taifa hii demokrasia yapo mpya!

Respect.

FMEs!
 
Huyu Malacela siyo wa kuaminika kuwa anapambana na ufisadi. Kwanza atangaze hadharani kuwa ameacha udhalimu wa kuhujumu demokrasia nchini. Malecela anafahamika kwa propaganda na kupanga mbinu za wizi wa kura za vyama vya upinzani. Miaka michache imepita tangu alipotuambia vijana wa vyuo vikuu baada ya kupewa kadi na NEC kuwa CCM inahitaji ushiriki wa vijana ili chama chake kibaki madarakani. Na ili hili lidumu akasema kuwa inahitajika kusema uongo, kuiba kura na hata kuua. Sasa mtu anayefundisha kuua anaweza kupambana na ufisadi. Au kwa kupokea zawadi za walemavu kutoka kwa wachungaji ndiyo anawahadaa watanzania kuwa ameacha uovu?
Malecela kwanza akiri hadharani kuwa ameacha uovu wote wa kuua demokrasia nchini na aombe radhi kwa kushirki udhalimu ndipo aaminike. Aache kushiriki katika wizi wa kura katika chaguzi ndogo za Ubunge na nyingine. Vinginevyo ni kama nyoka aliyejivua magamba lakini sumu bado anayo. Je katika hali ya sasa John Malecela ni wa kuaminika kuwa anapambana na ufisadi?
 
- Finally, CCM inaanza kuwa na demokrasia yaani kila kiongozi kusema maoni yake bila kutishiwa, sasa wahamishie kwenye taifa hii demokrasia yapo mpya!

Respect.

FMEs!
Respect FMES
Naomba kutofautiana na wewe. Unajua ili chama kiwe na uwezo wa kuongoza na kiwe na uwezo wa kujiendesha kinatakiwa kiwe na discipline ya hali ya juu. Sasa hivi tunachoona ndani ya chama ni uozo, hakun a kauli inayoweza kutoka na ikaitwa kauli ya chama, kila mtu ni msemaji na kila mtu ana opinion tofauti.

Inaweza kuwa demokrasia kama ingekuwa inatafutwa kauli ambayo ingeitwa kauli ya chama ambapo kwenye hatua ya mwanzo kila mtu angeweza kutoa maoni yake, sasa hivi hakuna kitu kama hicho. Hata hawa tunaowaita viongozi wa chama inaonekana hata kauli zao hazina nguvu na hazionekani kama ni kauli tooka kwa kiongozi, zinaonekana kama ni leymen opinion, sio kauli zilizotokana na msemaji kuchambua, naona ni uozo tu mkuu.
 
Ningependa sana nijue what is going on between Serukamba na Lowassa. Kila akiongea hana hata aibbu ya kumtetea Lowassa sijui anataka nini! Poor him!
 
Respect FMES
Naomba kutofautiana na wewe. Unajua ili chama kiwe na uwezo wa kuongoza na kiwe na uwezo wa kujiendesha kinatakiwa kiwe na discipline ya hali ya juu. Sasa hivi tunachoona ndani ya chama ni uozo, hakun a kauli inayoweza kutoka na ikaitwa kauli ya chama, kila mtu ni msemaji na kila mtu ana opinion tofauti.

Inaweza kuwa demokrasia kama ingekuwa inatafutwa kauli ambayo ingeitwa kauli ya chama ambapo kwenye hatua ya mwanzo kila mtu angeweza kutoa maoni yake, sasa hivi hakuna kitu kama hicho. Hata hawa tunaowaita viongozi wa chama inaonekana hata kauli zao hazina nguvu na hazionekani kama ni kauli tooka kwa kiongozi, zinaonekana kama ni leymen opinion, sio kauli zilizotokana na msemaji kuchambua, naona ni uozo tu mkuu.

- Huu ni mtizamo wako, wa kwangu ni demokrasia at work, sina tatizo kukubali kutokubaliana, kwa sababu safiki mtizamo wako!

Respect.

FMEs!
 
ccm WENGI NI TETRACYCLINE yaani rangi mbili. trust no one BUT true change.
 
Ningependa sana nijue what is going on between Serukamba na Lowassa. Kila akiongea hana hata aibbu ya kumtetea Lowassa sijui anataka nini! Poor him!


Ni Puppet, Msukule, Ndondocha, Joyce Wowowo.
Puppet hufanya kile BWana wake apendacho.
Jamaa hana Akili,Mawazo huru, Moyo wala uzalendo yatokeyapo mazungumzo hasi juu ya bwana wake Lowassa.
Hutumia uwezo, uzoefu, nia na hamu yake kumtetea nunda hata ikibidi kubeba aibu mithili ya ile ya kwenda uchi mbele ya mkweo na watoto.


Du!
 
- Finally, CCM inaanza kuwa na demokrasia yaani kila kiongozi kusema maoni yake bila kutishiwa, sasa wahamishie kwenye taifa hii demokrasia yapo mpya!

Respect.

FMEs!
Kwa hakika ni mwelekeo mzuri, lakini inafaa wengi wapate ujasiri na kuanza kuzungumza na wazungumze kwenye vile vikao rasmi, ni wakati wa kuachana na zidumu fikra...
 
- Mkulu wangu yaani a great thinker, hebu nijaribu kukuelewa na this post:-

1. Hivi kiongozi mhuni kama Malecela, anakuwa amechaguliwa na wananchi wa aina gani? Sio anaofanana nao? Sasa unafikiri in this case ya Mhuni Malecela, wananchi na viongozi waliomchagua Malecela kwenye uongozi wa taifa wanakuwa ni wa aina gani?

2. Kambarage hakuwa mhuni, sasa aliwezaje kufanya kazi kwa kumchagua mhuni Malecela, kuwa mpaka waziri wake wa nje? Na mpaka kuwa Makamu wa CCM, chama chake yeye mwenyewe Mwalimu? Eti si tumekubaliana kwamba Kikwete ni fisadi kwa sababu anaweza kufanya kazi na mafisadi bila tatizo? Au?

Anyways, samahani sana kama nitakuwa nimekukwaza na infact siku hizi Malecela mwenyewe alinikataza kufanya ninachofanya sasa, kwa hiyo I am out!

Respect.

Sauti ya umeme FMES!
Samahani mkuu, nilijua nitakukwaza maana kuna watu walijaribu kunitahadhalisha kabla, lakini hayo yalikuwa ni mawazo yangu na nimemnukuu Nyerere maana aliyasema pia kwenye kile kitabu chake cha Hatima ya uongozi.
Na najua Malecela amechaguliwa na watu. Na unajua c wote waliochaguliwa walichaguliwa kwa sababu kweli walikuwa ni watumishi wazuri, hapana. Kuna sababu nyingi tu zinazoweza kumfanya mtu achaguliwe hata kama hafai.
Ndio sababu sioni ajabu EL kuwekewa zuria wakati ana tuhuma kubwa za rushwa. Na sintaona ajabu kama wamasai watamchagua tena kuwa mwakilishi wao.
Na sioni ajabu Chenge akipokelewa kama mfalme wa wasukuma wakati wote tunajua nini alichofanya. Na sintaona ajabu kama atarudishwa bungeni na chama chake.
Na sioni ajabu hata rais akichagua fisadi Makamba na kumpa ukatibu mkuu wa chama chenu pamoja na tuhuma za ufisadi alizo nazo.
Nasema sintaona ajabu.
Samahani sana kaka kama nimekukwaza ila hapa nilitoa maoni yangu tu hata kama yanachoma moyo. Tuvumiliane tu.
 
Malecela kwanza akiri hadharani kuwa ameacha uovu wote wa kuua demokrasia nchini na aombe radhi kwa kushirki udhalimu ndipo aaminike. Aache kushiriki katika wizi wa kura katika chaguzi ndogo za Ubunge na nyingine. Je katika hali ya sasa John Malecela ni wa kuaminika kuwa anapambana na ufisadi?

Cigwiyemisi John Samwel Malecela ni mtu mmoja atakayekumbukwa katika historia ya Tanzania kama kada wa CCM na Waziri Mkuu wa JMT aliyepigana kufa na kupona kuzuia upepo wa mageuzi mwaka 1991. Cigwiyemisi John Samwel Malecela alifikia hatua ya kuwafananisha wanamageuzi na sisimizi wa kusiginwa tu na kufilia mbali.

Kama si kwa Mwalimu kuingilia kati na kusema kuongelea mageuzi si dhambi, hakuna mwana CCM hata mmoja - si kiongozi wala mwananchama (mwenye kadi), aliyebariki mfumo wa vyama vingi. CCM ilijikuta inalazimika kusalimu amri na kukubali mageuzi kutokana na nguvu zilizokuwa nje ya uwezo wake japo kwa shingo upande.

Sera ya ufisadi ndani ya CCM ilianza pale ilipokataa kuridhia kuandikwa kwa katiba mpya iliyoendana na hayo mabadiliko makubwa. Hiyo iliwapa nafasi ya upendeleo maalum katika hatua zote za mwanzo tangu katika usimamizi na uandikishwaji wa vyama vipya. CCM imeendeleza hivyo hivyo ubabe wa kuwa mchezaji na mwamuzi vyote kwa pamoja.

  • Wakahatamia katiba na kuifanya ajenda yao binafsi - ufisadi namba moja.
  • Wakatwaa mali zote zilizochangiwa kwa pamoja -- ufisadi namba mbili.
  • Wakafunga milango ya kudai haki na usawa- ufisadi namba tatu.
  • Wakateua kada wao kuongoza tume ya uchaguzi - ufisadi namba nne.
  • Wakabuni hila chafu chafu za kubaki madarakani - ufisadi namba tano
Kote huko Cigwiyemisi John Samwel Malecela alikuwa kamanda muhimu.

Na sasa Cigwiyemisi John Samwel Malecela, mzee aliyetakiwa kung'atuka na kuwaachia wajukuu wake ulingo wa siasa anasema mbinu mpya ziko jikoni zinapikwa ! Anayejaribu kutenganisha CCM na hii kasi ya ufisadi tunayoshuhudia sasa hivi ni heri akanunue miwani. Mwana CCM anayedai yeye si fisadi na kuwaelekezea vidole makada wenzake ndani ya CCM ni limbukeni wa kutupwa - and that's a memo !!
 
Back
Top Bottom