Malawi Yajiandaa Kuhalalisha Ukahaba

Herbalist Dr MziziMkavu

JF-Expert Member
Feb 3, 2009
42,318
33,125


3413526.jpg

Serikali ya Malawi Malawi inajiandaa Kuhalalisha Uhakaba Monday, October 26, 2009 8:37 AM
Serikali ya Malawi inajiandaa kupitisha sheria itakayohalalisha biashara ya ukahaba nchini humo kwa kuwaruhusu makahaba wafanye ukahaba kwenye majumba yao badala ya kusimama barabarani. hatua hiyo ya serikali ya Malawi inakusudia kuwalinda wanawake wanaojiuza barabarani kutokana na manyanyaso wanayopata kutoka kwa wateja wao.

Waziri wa masuala ya jamii na maendeleo wa Malawi, bi Patricia Kaliati akiongea na shirika la habari la Reuters alisema kwamba muswada wa kuruhusu biashara ya ukahaba majumbani nchini humo uko kwenye hatua za mwisho kupelekwa bungeni ili upitishwe uwe sheria.

"Tunataka watoke mitaani wakafurahie tendo la ngono kwenye majumba yao na hivyo kuepukana na kunyanyaswa kijinsia au kubakwa na wateja wao na hivyo kuwalinda na gonjwa la ukimwi", alisema Kaliati.

Ugonjwa wa ukimwi nchini Malawi yenye idadi ya watu milioni 13 umeishaua zaidi ya watu laki nane tangia ulipoingia nchini humo mwaka 1985.

Jitihada za kuwaelimisha watu kujikinga na ugonjwa huo zimesaidia kupunguza idadi ya waathirika toka asilimia 14 hadi 13. Madawa mengi yanayotolewa bure kwa waathirika yamesaidia kupunguza idadi ya vifo vya waathirika kwa asilimia 70.

Hata hivyo muswada huo wa kuhalalisha ukahaba tayari umeishakumbwa na upinzani toka taasisi mbali mbali.

"Malawi ni nchi ambayo raia wake ni waumini wa dini zinazokataza ukahaba kwa njia yoyote ile, hivyo lazima tusisahau kuzingatia mila zetu na imani zetu za kiroho", alisema Mavuto Bamusi, mwanaharakati wa kutetea haki za binadamu.

Waziri Kaliati aliutetea muswada huo kwa kusema lengo lake kubwa si kuhalalisha ukahaba bali kuwalinda wanawake wanaofanya ukahaba.

Miji mikubwa ya Malawi imekuwa na ongezeko la madada poa katika miaka ya hivi karibuni na miongoni mwa wasichana wanaojiuza wengine wana umri mdogo kuanzia miaka 12. http://www.nifahamishe.com/NewsDetails.aspx?NewsID=3413526&&Cat=2
 
Hawa wana akili sana. Hii biashara imeanza hata Yesu hajazaliwa.

Halafu leo mtu unajifanya unaipiga marufuku, hamna lolote. Hata kwa Waarabu na sharia law zao, ma PIMP wa Kirusi kibao.

Heri kuwaruhusu na kuwapatia shule jinsi ya kufanya kazi yao salama na mwisho watakuwa na ulinzi na watalipa kodi. Mbona mnapokea misaada ya Waholanzi? Mnafikiri hela zinatoka wapi? Ni kodi ya wauza bangi, umalaya, sex shop, madangulo na kila aina ya uasherati na ulevi......... that's Netherland baby!!!!!

Kuzuia hii biashara ni kupigana na ukuta.....
 
Pale New Happy Bar mbona ilifungwa?
Naskia vijana wa Lebanon...walimtisha Bonny wakamwambia "watamtundika msalabani" au ahamishe...ufuska wake, Mkuu pale weshaadhirika watu na heshima zao,siku hizi wanaponea Jozani na hapo nasikia wazee wa Miembebi wamechachamaa wametaka pafungwe maramoja...yaani panafanyika uzinifu jaharanasi.
 
Naskia vijana wa Lebanon...walimtisha Bonny wakamwambia "watamtundika msalabani" au ahamishe...ufuska wake, Mkuu pale weshaadhirika watu na heshima zao,siku hizi wanaponea Jozani na hapo nasikia wazee wa Miembebi wamechachamaa wametaka pafungwe maramoja...yaani panafanyika uzinifu jaharanasi.
Jozani napo pameshafungwa, pale palikuwa ni zaidi ya New Happy kwani bar ile ilikuwa ikifanya kazi masaa 24 hali kadhalika guest house yake. Hii ilikuwa ni tishio sana. Zaidi jirani yake Jitini nao wakaingia mkumboni na kuifanya Miembeni kuwa kitongoji kisicho lala!

Sasa hivi upepo unavuma Daraja Bovu na mitaa fulani ya Bububu!
 
Sasa hivi upepo unavuma Daraja Bovu na mitaa fulani ya Bububu!
Vp washika dau ndo wale wale wa Jozani na Jitini...? kama hali itakuwa hivi basi wakaazi wa darajabovu watafaidi kuona 'maprado', nimeona rafu mbili tatu maeneo ya saateni,kambi ya JKU..karibu na maeneo yangu ya kujidai...silali kwa raha, mziki usiku kucha...na "watoto si riziki" na akina "dada fungu shilingi" wanakuwa wengi kila siku...yaani utafikiri si kambi ya jeshi vile...sijuwi siku hizi vp.
 
Hawa wana akili sana. Hii biashara imeanza hata Yesu hajazaliwa.

Halafu leo mtu unajifanya unaipiga marufuku, hamna lolote. Hata kwa Waarabu na sharia law zao, ma PIMP wa Kirusi kibao.
Mkuu, unaongea kama tupo karne ya 19 vile...hizi zama za UKIMWI,kuruhusiwa biashara ya ukahaba ndo akili sana...na kwakuwa biashara hii imeanza tokea Yesu hajazaliwa ndo akili yako imetoa leseni ya ku-appreciate...
 
Mkuu, unaongea kama tupo karne ya 19 vile...hizi zama za UKIMWI,kuruhusiwa biashara ya ukahaba ndo akili sana...na kwakuwa biashara hii imeanza tokea Yesu hajazaliwa ndo akili yako imetoa leseni ya ku-appreciate...
Mkuu sidhani kama kuna uhusiano wowote wa uhalalishaji na UKIMWI, kungekuweko basi Ulaya na America wangeongoza kwa Ukimwi na Tanzania mngekuwa wa mwisho maana kila siku defender na mafuta ya walipa kodi yametumika kuwakamata makahaba kuliko nchi yoyote ile duniani. Nenda Uholanzi, Ubelgiji malaya ni sawa na idadi ya wakazi wa Mbeya yote lakini umeona hesabu ya watu wenye UKIMWI huko? watu wanasema hawajawahi kumuona HIV +ve person wala kuhisi kuwa huyu ni HIV positive person.

Nchi zilizoruhusu abortion zimeokoa vifo vya akina mama wengi kuliko sisi tunaojidai wamaadili tumeua wanawake kuliko sehmu nyingine kusini mwa jangwa la sahara. Mkuu safiri kwa gari mida ya jioni Dar Es Salaam mpaka Kazungura/Livingstone/Kariba (mpaka wa Zambia kusini) Uone idadi ya watu wanaouza miili yao. Msamvu, Makambako, Tunduma, Ni balaa ila shida ni kuwa huwa hamuangalii,
 
Mkuu, unaongea kama tupo karne ya 19 vile...hizi zama za UKIMWI,kuruhusiwa biashara ya ukahaba ndo akili sana...na kwakuwa biashara hii imeanza tokea Yesu hajazaliwa ndo akili yako imetoa leseni ya ku-appreciate...
Unaongea kwa kiimani au unaongea kwa kutumia data?
 
Wakuu wk end tutatuwa tunapishana maeneo ya kusini tukielekea Malawi kujipumzisha..Tunabadirisha viwanja..Kutoka Kampala hadi kwa mzee Kamuzu Banda.! Natakiwa tu nunua spare tires mbili za ziada..!
 
Mkuu safiri kwa gari mida ya jioni Dar Es Salaam mpaka Kazungura/Livingstone/Kariba (mpaka wa Zambia kusini) Uone idadi ya watu wanaouza miili yao. Msamvu, Makambako, Tunduma, Ni balaa ila shida ni kuwa huwa hamuangalii,


Mkuu hizi hints mbona mlitucheleweshea sana jamani ?
 
Good decision, big up Malawi govt... then ziundwe sheria ndogondogo kama vile kutokuruhusu watoto wadogo kushiriki biashara hiyo n.k.

Tanzania tunajidanganya, ukahaba hapa ni mwingi kuliko nchi nyingi za afrika, tembeeni mabarabarani usiku muone... tembelea salon afu ujifanye unataka kujisaidia na wadada uone, tembelea kwenye massage clinic uone.

Big up tena Malawi. takwimu zitakazofuata baada ya miaka mitatu ijayo zitaonyesha kupungua sana kwa maambikizo ya ukimwi kwa wana malawi.
 
Back
Top Bottom