Malaria sugu inanitesa! Dawa gani itanipa tiba ya kudumu?

Maombi kwa MUNGU WA MBINGUNI ni muimu sana, yeremia30:17, isaya 53:5b
Mke wangu alikuw na tatizo hilo muda mref sana juz kapima hana malaria hana typhod.
Ni PM nikupe namba za dr aliyetupa dawa. didas_6@hotmail.com
 
weka mambo hadharan na sie wengine tumjue huyo dr ili tupate tba. Jf ni uwazi na ukweli.
 
Hello,

Hata mie yamewahi kunikuta.

Tangu 2001, nilikuwa naumwa malaria na nilitumia SP ila hazikusaidia.

Ila dawa ni Malimao na vitunguu swaumu.

Chukua vitunguu swaumu vilivyomemwa kiganja kimoja, twanga vilainike, halafu kamulia limao moja au mawili. Acha vikae angalao kwa masaa 2 halafu weka maji salama, ya uvuguvugu ndo mazuri. Chuja na unywe.

Fanya hivyo mara 2 kwa siku, halafu angalau siku 3 au zaidi kwa uhakika zaidi.

Huo mpango pia inatibu typhoid sugu.

Pia kunywa maji mengi ili kuondoa sumu.

Dawa za asili kama vitunguu swaumu na malimao hazina side effects. Of course hivi ni vyakula
 
nashukuru sana, nichanganye na maji kiasi gani? nitafanya hivyo
 
ZINGATIA MAELEZO YA MPADMIRE NA VILEVILE JARIBU DAWA YA Artemisinin TOKA KITENGO CHA TIBA ASILI HAPO HOSPITALI YA MUHIMBILI,UBARIKIWE
 
kuna dawa toka upareni inaitwa mvoro unachanganya na chai au maji moto asubuhi na jioni,ndugu malaria itakua historia kwako!
 
Ooh,pole sana mkuu.dah,mi nikiugua malaria nnkinywa metakeflin napöna ndani ya masaa mawili na naweza kukata hata miaka kumi bila kuugua i think it has something to do with immunity and what i eat.mfano nakula sana vegetable hasa salad ilokamuliwa limao kwa sana.yaani naeza shindia salad.pengine you should watch what you eat kuugua malaria kwa mda mrefu is not normal SOMETHING IS WRONG WITH YOUR IMMUNITY.
 
Hata Ansah Miles yupo Sahihi.

Vitunguu swaumu vilivyotwangwa kwenye kinu ndo huchanganywa na malimao kama 2 hivi. Then acha kwa masaa 2 au zaidi.

Maji unachanganya wakati unapotaka kunywa, ni kikombe au glasi. Maji ya vugu vugu ndo safi, yawe salama.

Fanya hivo mara 2 kwa siku.

siku 3 hadi 5 zinatosha kabisa.

Baada ya hapo unaweza kujihakikishia kupona kabisa kwa kunywa chai ya Artemisia.
 
huo mchanganyko wa vitunguu na limao, naweza utumia zaid ya mara moja? Au nikishachuja mabak hayana kazi? Naomba majibu yako kwan nimeshaanza hlo zoez
 
Wana JF naomba msaada wenu, ni takribani mwaka sasa sijawahi kupata nafuu kutokana na huu ugonjwa. Je tatizo hili lipo au ni mimi tu? Nimetumia dawa nyingi, za hospital mpaka mitishamba, huwa napata nafuu ya muda mfupi na ugonjwa unarudi tena. Kwa yeyote mwenye kuijua tiba ya uhakika anijulishe.Nipo DSM, asanteni

Tindikali...labda nikuulize swali, umejuaje kuwa unaugua malaria sugu? Kila ukijisikia dalili unaenda hospitali kufanya kipimo cha malaria ukaambiwa una malaria kweli na labda wadudu wangapi? Kwa sababu dalili za malaria zinatokea pia kwa maginjwa mengine meengi tu, inaweza isiwe malaria kama hukufanya kipimo husika kikathibitisha.

Vile vile...ili kusema malaria ni sugu, ni lazima upime malaria ithibitike (kipimo cha slide ya kioo na darubini) kisha upewe dawa, na utumie dozi sahihi kama ulivyo andikiwa na daktari..kisha ukimaliza dozi upime tena malaria, kama itaoneka basi hapo waweza sema una malaria sugu na hizo dawa zimeshindwa kukutibu. Kifupi na hapo mfano hujatumia dozi ipasavyo, hujamaliza dozi, hujapima baada ya kumaliza dozi..huwezi kusema ni malaria sugu.

Kuna wakati tunapata malaria mara kwa mara (new infection) halafu tunalaumu ni malaria sugu...mfano, unapata dalili za malaria, unaenda hospitali na inathibitika ni malaria, unapewa dawa unatumia ipasavyo, unapona...kisha unarudi kwenye tabia/mazingira yako ya kawaida ya kutojikinga na malaria, unapata malaria upya (new infection)...hiyo sio malaria sugu, ni malaria mpya ambayo inabidi utibiwe.

Pia kuna dawa nyiingi sana za malaria ambazo zimeshazuiwa kutumika kutibu malaria kwa sababu wadudu wa malaria wamepata usugu dhidi ya dawa hizo..mfano Chloroquine, SP, na baadhi ya dawa zisizo mseto mfano Amodiaquine, Arinate, Artesunate (vidonge) etc ambazo pekee bila kujumlisha dawa nyingine ufanisi wake ni mdogo. Lakini hizi bado zinapatikana kwa wingi kwenye pharmacy, maduka ya dawa, na zhanati binafsi. Hizi zimeshathibitishwa kutotibu malaria kwa ufanisi, lakini utakuta baadhi ya madaktari au wagonjwa wanazing'ang'ania.

Dawa zilizothibitishwa kuwa na ufanisi wa juu kutibu malaria (hata malaria sugu) ni dawa mseto mfano Coartem/ALu, DuoCotexcin, na zisizo mseto Quinine (sindano na vidonge), Artemether (sindano) na Artesunate (sindano). Kuna nyingine nyiingi zipo kwenye majaribio au zimeshamaliza majaribio lakini ni za jamii ya Artemisinin mseto.

Ushauri wangu....zingatia hayo niliyosema hapo juu ili utambue kuwa ni malaria kweli au tatizo jingine? kama ni malaria, ni sugu au new infection? Kisha muone daktari atakupatia matibabu na ushauri jinsi ya kujikinga..na malaria haitakusumbua tena.

NB: MALARIA INAUA KULIKO HATA UKIMWI, SI WATOTO TU..HATA WATU WAZIMA. KUWA MAKINI NA HUO UGONJWA.
 
Ukishatumia dawa jaribu kujikinga na mbu wasikuume, na sometimes madawa yakiwa mengi sana kwenye mwili yanakufanya ujisikie vibaya kwani dawa zinaweka sumu kwa damu, hivyo usijizoeshe sana kula dawa, hizi wanafanya biashara tu na serikali imagine kila mwaka wanakwambua eti dawa hii ndio inayotibu malaria wanatutapeli tu kwa 10 % wanayopata jaribu kunywa maji, kula matunda mengi, epuka vyakula vyenye mafuta ya wanyama coz sometimes vinachangia kuufanya mwili ujisikie kama unaumwa kumbe huumwi
 
ukipona,
1. kumbuka kutumia chandarua kilichowekewa dawa...
2. haribu mazalia yote ya mbu....
3. fanya regular checkups...
kumbuka: prevention is better than cure.
 
Ukishatumia dawa jaribu kujikinga na mbu wasikuume, na sometimes madawa yakiwa mengi sana kwenye mwili yanakufanya ujisikie vibaya kwani dawa zinaweka sumu kwa damu, hivyo usijizoeshe sana kula dawa, hizi wanafanya biashara tu na serikali imagine kila mwaka wanakwambua eti dawa hii ndio inayotibu malaria wanatutapeli tu kwa 10 % wanayopata jaribu kunywa maji, kula matunda mengi, epuka vyakula vyenye mafuta ya wanyama coz sometimes vinachangia kuufanya mwili ujisikie kama unaumwa kumbe huumwi

Inawezekana kukawa na ukweli hapo kwenye nyekundu...lakini lazima uelewe kuwa katika nchi ambazo malaria ni 'janga la afya kwa jamii' (public health problem), matibabu yake yanasimamiwa na sera ya afya, kwa Tanzania sera ni dawa ya mseto (ALu) kwa malaria isiyo kali, na Sindano/drip za Kwinini (Quinine) kwa malaria kali au sugu. Hizo dawa zilizopo kama sera huchagululiwa kwa kuzingatia ufanisi (efficacy) wa dawa yenyewe, gharama, urahisi katika kutumia na kufuata uashuri wa daktari/mfamasia, na madhara (side effects) kutokana na tafiti mbali mbali za kisayansi zilizofanywa.

Uamuzi huo haufikiwa na mtu mmoja kwa kutaka 10% kama unavyofikiri. Kwanza tafiti lazima zifanywe, kisha debate mbali mbali kwa washika dau wenye taaluma tofauti...madaktari, wafamasia, watafiti, wanasayansi afya ya jamii, wachumi, watunga sera, vitengo mbali mbali vya wizara ya afya etc. Na pia uamuzi wa kutoa dawa kwenye sera ya taifa (kama ilivyotolewa Chloroquine, kisha SP) unazingatia mfumo huo huo. Tafiti lazima zifanywe kuthibitisha kuwa haifanyi kazi ipasavyo (hapa ikishindwa ufanisi kwa 20% tu basi haifai tena, pamoja bado ina ufanisi kwa 80%) kisha debate zifuate mpaka ufikiwe uamuzi wa kuitoa na kuweka nyingine kwa vigezo nilivyoainisha hapo juu.

Kwa hiyo si rahisi hii process huwa na usanii/biashara na serikali kufukuzia 10%....
 
ZINGATIA MAELEZO YA MPADMIRE NA VILEVILE JARIBU DAWA YA Artemisinin TOKA KITENGO CHA TIBA ASILI HAPO HOSPITALI YA MUHIMBILI,UBARIKIWE

Mkuu hii ndio dawa pekee iliyokoa maisha yangu. Ila maleria nayo ina nyanyasa sana nikirudi kwetu Taveta no malaria nikikaa hapa Manzese kwetu weee. Ila hio dawa ni chunguuuuu weeee
 
Inawezekana huumwi hata hiyo Malaria. I had the same problem. Kumbe ni aina ya kazi ninazofanya zinanichosha na ninahisi malaria na kumbe hata siyo. Nilikwenda kwa Dr mmoja akanipa ushauri wa maneno, na kuniuliza ninafanya nini. At that time, I was very busy na mambo ya makaratasi. After that ushauri, ikawa malaria ikitokea ninakwenda kupimwa sehem za kueleweka na kutumia dawa ya kueleweka, vyakula na maji kwa wingi. Sasa hivi nina muda mrefu kama miaka 5 sasa nimerelax.
 
Mkuu hii ndio dawa pekee iliyokoa maisha yangu. Ila maleria nayo ina nyanyasa sana nikirudi kwetu Taveta no malaria nikikaa hapa Manzese kwetu weee. Ila hio dawa ni chunguuuuu weeee

Nguli una uhakika ulipewa dawa ya Artemisinin? Chungu? Tangu nianze shiriki katika tafiti za dawa za jamii ya Artemisinin mwaka 2002 sijaona dawa ya jamii hiyo 'chungu'. Jaribu kucheck, sidhani kabisa kama ulipewa jamii ya Artemisinin.
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom