Malaika na shetani wanagawana maiti

Django

JF-Expert Member
Apr 15, 2013
354
147
Watu wawili walikuwa wameiba maembe katika harakati za kukimbia wakakibilia chumba cha kuhifadhia maiti bila kujua,na kwa bahati mbaya ilikuwa usiku na umeme ulikuwa umekatika jamaa wa mochwari walikuwa wametoka.

Wale wezi walivyokuwa wanaingia mule ndani walidondosha maembe mawili pale mlangoni kutoka kwenye kapu lao.
Walivyoingia wakaanza kugawana yale maembe hii yako... Hii yangu.... Hii yako.... Hii yangu...

Mara wale jamaa wa chumba cha maiti wakawa wanarudi walipofika mlangoni wakasikia jamaa wanagawana maembe hii yako... Hii yangu... Hii yako... Hii yangu... Wakaogopa wakaanza kuulizana mh... Malaika na shetani wamekuja wanagawana maiti? Wenye zambi anachukua shetani na wasiokuwa na zambi anachukua malaika.
mara wakasikia na zile mbili tulizoziacha pale mlangoni tuzipitie....
Wale jamaa wacha wakimbieee...
 
Back
Top Bottom