Makundi ndani ya chama yawang'oa viongozi wa CCM tawi la UDOM.

nsami

Senior Member
Jun 11, 2010
175
8
Uongozi wa CCM tawi la UDOM college of Education chini ya mwenyekiti Nickson Mmanyi wiki iliyopita ulitangaza kujiuzuru uongozi baada ya wanachama wake kugomea uchaguzi wa viongozi uliotakiwa kufanyika siku hiyo huku mhe Mmanyi na katibu wake Ndg Egla Mamoto wakiwania kukomboa viti vyao.

Ni ktk kikao cha mkutano mkuu wa tawi kilichofanyika 5 June 2010 ktk ukumbi wa Halimashauri kuu ya CCM Mjini Dodoma kwa madhumuni ya kufanya uchaguzi huku candidates wote wa uchaguzi huo wakiwa ni viongozi wale wale (wasiotakiwa). Ndipo hoja ilitolewa na wajumbe ya kutokukubaliana na uchaguzi kwa kile walichodai mchakato wa kuwapata wagombea ulighubikwa na wingu la urafiki, ukabila na maslahi binafsi, na kutafsiriwa kuwa ni mwendelezo wa mnyukano wa makundi ya siasa za uchaguzi wa serikali ya wanafunzi uliofanyika mwezi uliopita.

Kufuatia hatua hiyo, viongozi wa muda waliteuliwa kuongoza tawi mpaka uchaguzi utakapotangazwa tena.
 
Ni siasa za vyuoni/ki-anafunzi.
Hivi maeneo ya kazi vyama vinaruhusiwa kufungua matawi? Au CCM inaruhusiwa.

Naona CCM imeanza mtindo wa kufungua matawi vyuoni! What for? Au ndo Ufisadi?
 
Back
Top Bottom