Makosa makubwa sita wafanyayo wanawake kitandani

Matanga

JF-Expert Member
Nov 13, 2019
2,281
3,973
Nimewahi kuandika huko siku za nyuma makosa makubwa manne wafanyayo wanaume kitandani, ni makala ilipendwa sana na wote na ukienda kwenye blog yangu unaweza kuiona na kuisoma wakati wowote. Baadhi ya watu walinitafuta na kunitaka niandike pia na makosa wafanyayo wanawake kitandani ili kupata balansi. Na leo nimeona niwatolee uvivu na kuwaletea hii kwa ajili ya wanawake.

Inajulikana wazi na watu wote kuwa ni rahisi sana kumfikisha mwanaume kileleni kuliko kumfikisha mwanamke. Kumwamsha mwanaume na kumfikisha kileleni ni rahisi sana kama kumsukuma mlevi. Bali ni shida sana kumfikisha mwanamke kileleni hasa kama mwanamke anakuwa na makosa haya 6 awapo kitandani ninayoeleza kwenye hii makala.

Mapenzi ni Sanaa na hakuna mtu mmoja anaweza kukuambia anafahamu yote au anafahamu kila kitu kuhusu mapenzi au tendo la ndoa.

Makosa makubwa kabisa 6 wafanyayo wanawake kitandani

1. Kudhani mme ni mganga wa kienyeji

Kila mwanamke ni tofauti hasa linapokuja suala la nini anahitaji ili aweze kufika kileleleni.

Hata kama mwanaume ni mtu mzima na pengine ana uzoefu kuhusu tendo la ndoa bado hawezi kufahamu kwa kuhisi tu ni nini hasa huwa kinakuamsha hata unafika kileleni pengine hata kufika kileleni mapema kirahisi zaidi ISIPOKUWA UMEMWAMBIA.

Ni jambo la mhimu kuwasiliana unapokuwa kitandani na mwenza wako.

Mwambie mimi nikishikwa sehemu fulani au nikiwekwa hivi najisikia vizuri zaidi, mwambie ni mme wako na rafiki yako wa karibu kuliko mtu mwingine yeyote.

Wapo baadhi ya wanawake anaweza kuchepuka kwa sababu hii ndogo.

Anajuwa ni kwa jinsi gani na namna gani anahitaji tendo la ndoa ila hawezi kumwambia mmewe moja kwa moja bali atachepuka akalale na fulani ambaye anajuwa hivyo anavyopenda yeye huku akimwacha mme hajuwi anakosea wapi.

Wanaume siyo waganga wa kienyeji kwamba kwa kuhisi tu anaweza kufahamu wewe unapenda vipi na ni wewe ndiyo unawajibika kumwelekeza pole pole na kwa lugha ya upole na staha.

Kumbuka kumweleza kwa upole na kwa lugha ya staha kwani tofauti na hapo unaweza tena kuvunja ndoa bila kujuwa.

Kwa mfano umeolewa na mwanaume na kila ukilala naye dakika 3 au 4 tayari amefika kileleni na hawezi kurudia tena, usiamke tu kwa kejeli na pengine kama mtu usiyejitambua na kumwambia ‘wewe huwezi kitu yaani unazingua tu mimi ningependa uende dakika 20 bila kupumzika’!

Hapo unaweza kulipata ulilolitafuta – talaka ya haraka na unaweza kuonekana kumbe wewe ni kahaba mzoefu.

Ipo namna ya kudai haki yako bila kuonekana msumbufu na usiye na akili.

Mwambie mme wangu ahsante sana kwa huduma nimefurahia sana umetumia dakika 4 natumaini kesho utafikisha dakika 8 ili nione ikiwa nitafurahi zaidi ya leo. Kwa lugha ya upole na tabasamu.

Na pengine utaanza kumtafutia na kumpikia vyakula vizuri vinavyoongeza nguvu na kumhimiza kufanya mazoezi ya viungo mara kwa mara na kumuombea kwa Mungu.

Kwahiyo kama tayari unajijuwa ni staili ipi ukifanya unafurahia zaidi au inakufanya usisimke zaidi au ufike kileleni kirahisi zaidi usisite kumwambia mmeo lakini usisahau kutumia lugha nzuri ya upole na yenye staha yenye mwelekeo wa kujenga zaidi na siyo kubomowa.

Tofauti na wanawake wengi mnavyofikiri kuhusu wanaume linapokuja suala la tendo la ndoa ukweli ni kuwa wapo wanaume wengi sana wasiojuwa tendo la ndoa linafanyikaje na wengine wapo mpaka wanaoa hawajawahi kushiriki tendo la ndoa na mtu mwingine yoyote.

2. Kutokuanzisha kamwe hitaji la tendo la ndoa

Wanawake wengi na hata baadhi ya wanaume huwa wanadhani kwamba ni mwanaume pekee ndiye anawajibika kuanzisha kutaka hitaji la tendo la ndoa.

Yaani ipo hivi; kila mara mtakaposhiriki tendo la ndoa anayekuwa alianza kusema twende kitandani au nasikia hitaji la tendo la ndoa kwenye ndoa nyingi huwa ni mwanaume!

Hilo ni kosa kubwa na wanaume wengi hawapendi hii tabia ila wengi wao hawana ujasiri wa kukuambia.

Hakuna kitu mwanaume anapenda kama kuambiwa mme wangu twende kitandani au mme wangu leo najisikia hamu ya kutaka kushiriki na wewe.

Kila mwanaume anapenda kuambiwa hivi.

Kama wewe ni mwanamke na unajitambuwa usiwe mjinga.

Siku moja moja mara moja moja kuwa wa kwanza kuhitaji jambo hilo.

Wapo wanawake yaani anajiona wazi ana ny*ge na anahitaji kushiriki lakini anakaa tu kimya na pengine akikutana na boda boda huko nje akamtaka anaweza kumpa kisa tu anaogopa kumwambia mmewe anahitaji tendo la ndoa.

Wapo wanaume wapo bize sana na kazi kiasi kwamba anaweza kumaliza wiki mbili hajakumbuka majukumu yake kitandani hivyo kumkumbusha au kumtaka siyo jambo baya na wanaume wengi wangependa kuwa na wanawake wa namna hiyo.

Mwanaume unapomkumbusha wakati mwingine kwamba unahitaji mkwaju ni ishara inayomjia kichwani kwake kwamba kumbe na wewe ni binadamu na kwamba kumbe huwa anakufikisha na kumbe ni kweli unamhitaji yeye kama yeye na siyo nyumba yake au gari lake au mali zake tu.

Wanaume wengi wakiambiwa hivyo na wake zao hujisikia vizuri sana na unaweza kumuona ghafla ana nguvu nyingi kuliko hata siku zingine alipoanzisha yeye kutaka mechi.

Hii ndiyo sababu makahaba wengi au nyumba ndogo nyingi wakikamata mme wako inakuwa ngumu kumrudisha tena kwako sababu wanaume ujinga wao wote upo hapo kitandani na kama hujuwi kukitumia kitanda chako vizuri kuna mwingine yupo tayari kumwamsha na kumtaka.

Tangu akiwa njiani kurudi nyumbani toka kazini mtumie ujumbe mme wangu leo ninahitaji dozi tafadhali usisahau. Hilo tu linaweza kumfanya apitie kwa fundi akombowe gauni lako ulilopeleka kushona hivi karibuni hata kama hujamwambia!

Kama kawaida mimi lazima nikushauri. Hata hapa patumie vizuri. Isiwe kila siku wewe ndiyo unaanza sababu tu nimekuambia wanaume wanapenda hivyo, hapana, fanya mara moja moja pengine mara 2 au 3 hivi kwa mwezi siyo kila siku baadhi ya wanaume wanaweza kukuona vibaya tena ukizidisha.

Wapo baadhi ya wanawake hutumia lugha ya ishara kwa mfano anaweza kuwasha taa ya rangi fulani chumbani au akaweka muziki fulani au akatandika kitanda kwa namna fulani au akavaa tu mavazi fulani na mmewe atajuwa leo anahitaji.

Si vibaya ukienda mbali zaidi ukamwambia moja kwa moja baba Amina eee mwenzio leo nahitaji haki yangu.

3. Kuleta matatizo ya maisha kitandani

Kuna baadhi ya wanawake kitandani ndiyo mahakamani kwao yaani kila tatizo linalomsibu atalileta kitandani.

Chakula kimeisha, mtoto anadaiwa ada, kuna hela ya vikoba anahitaji, kuna gauni fulani zuri ameliona yote haya atasubiri wakati mpo kitandani ndiyo aseme!

Poleni sana wanawake wa tabia hii

Hakuna mwanaume anataka hilo.

Kitandani ni sehemu ya kusahau shida kwa muda hata kama zipo, ni sehemu ya kutoa stress zako zote na siyo kuzileta stress zingine tena.

Ukiwa kitandani zungumza muda mwingi mambo yanayohusu kitandani. Kama una shida fulani nikumbushe mchana baada ya kumaliza kula chakula au asubuhi wakati naelekea kazini siyo kitandani.

Mara nyingi mwanaume anajuwa unahitaji kitu fulani au hela fulani bila hata kumuomba au kumwambia na mwanaume mwenye akili atakupa au kukusaidia bila hata kuombwa au kukumbushwa.

Sasa nyinyi ndugu zangu tupo kitandani mara ooh nadaiwa vikoba mara mama mdogo anaumwa mara sijuwi nahitaji laki mbili nikanunuwe viatu! Uume utanisimama vipi hapo?

Ndiyo hapo kuanza kesema mme wangu amepoteza nguvu za kiume au hana hamu ya tendo la ndoa na mimi kumbe ni wewe mwenyewe ndiyo umemloga bila kujuwa.

Wanaume wengi wakitoka kazini huchagua kupita bar walewe na watulie na rafiki zao mpaka saa tano ndiyo anarudi nyumbani akifika moja kwa moja usingizi maana anaogopa kuwahi kurudi nyumbani atakutana na msululu wa matatizo kutoka kwa mkewe.

Ni kweli una tatizo, ni kweli una shida fulani, ni kweli unahitahi shilingi fulani, lakini angalia ni wapi unaniambia siyo kitandani. Kitandani ni sehemu ya mimi kujificha na kusahau kwa dakika kadhaa shida za huko duniani.

4. Kukubali kila anachoambiwa na mme

Kila mtu ana kemia yake na kila mtu kuna vitu anavipenda na kuvichukia.

Ikitokea kila unachoambiwa au kuombwa wewe unakubali tu ni hatari kwa afya yako ya ndoa.

Kama kuna kitu hupendi sema wazi bila kuficha wala kuogopa kuwa 'mimi staili hii mme wangu siipendi'.

Usiigize wala usiogope kuwa muwazi na mkweli kabisa 'mimi hicho ulichoniambia sikipendi na siwezi'.

Kama unaona siku hiyo ni vizuri mmeo atumie c*nd*mu mwambie nataka uvae leo au kama hupendi avae mwambie leo nataka kavu kavu, kama mmeo anapenda mfanye jikoni na wewe hujisikii mwambie nataka tukafanye chumbani nk

Hiyo ni mifano tu siwezi kuandika kila kitu mengine jiongeze na wewe.

Pointi yangu hapa ni kuwa usikubali lolote unaloambiwa au kuombwa na mmeo kitandani ikiwa wewe kwa nafsi yako hupendi.

Kama anafanya kwa fujo sana kuliko inavyohitajika mwambie nenda pole pole, lasivyo unaweza kuumia au kuchanika bila sababu na mdomo wa kukataa unao.

Wanawake wengi utasikia nilipata ujauzito huu kwa bahati mbaya nilimwambia mwenzangu atumie kinga na akakataa na yeye mwanamke akakubali!

Huo ni utahila.

Usikubali kila kitu hata ambavyo hupendi.

Ni mwili wako upo huru.

5. Kukaa tu kitandani kama gogo

Wapo baadhi ya wanawake yaani ni kama gogo au samaki aliyekufa

Hajuwi hata kukata kiuno

Yaani yeye avuliwe nguo, awekwe kitandani, achezewe, aandaliwe, aingiliwe yeye ni kimya tu haseguki wala kugunaguna japo kwa umbeya.

Amekaa tu anasubiri wewe mwanaume ufanye kila kitu mpaka umwambie tayari nimemaliza twende tukaoge!

Huna hata aibu yaani

Kata kiuno japo kidogo na wakati mwingine mwambie nataka nije juu yako na wewe mwanaume uwe chini, onyesha namna fulani ya kwamba na wewe upo na unashiriki na siyo kumwachia mmeo majukumu yote

Mme atakuona wewe ni mshamba na hujuwi kitu.

Kama kawaida hapa tena lazima nikuonye.

Nenda pole pole, usijionyeshe kwamba wewe unajuwa kila kitu na vyote na kuwa unaweza hadi kumfundisha mmeo!

Nenda pole pole na kwa akili.

Usikutane tu siku ya kwanza na mmeo halafu akaona wazi kabisa umemaliza chuo kikuu, hapana, anza kwa kumuonyesha kuwa shule ya msingi umemaliza na unajiandaa kwenda sekondari.

Hii inafanana na ile ya kusubiri kila siku mmeo ndiyo aanze kutaka mechi.

Onyesha namna fulani kwamba upo na unafurahia tendo lenyewe na upo tayari na unapenda kushiriki.

Mtazame usoni mmeo na siyo kufumba tu macho wakati wote.

Usiwe gogo na usiwe kimya dakika zote za mechi.

Kama unaweza kulia lia, kama unaweza kutamka maneno yoyote machafu kuhusu tendo la ndoa tamka ila usikae kimya muda wote kwani inaweza kumuonyesha mmeo hufurahii tendo na pengine akaona kama vile hakufikishi popote.

Kumbuka kila jambo na wakati wake na sehemu yake.

6. Kudanganya kama umefika kileleni

Wanawake wengine ni wa ajabu sana yaani unaweza kubaki unashangaa tu

Unajuwa kabisa hujafika kileleni lakini unadanganya ili kumridhisha mmeo bila kujuwa unajidanganya mwenyewe.

Yaani dakika 3 tu tangu muanze mwanamke anaanza kupiga kelele na kulia akijidai wazi amefika kumbe ni uongo mtupu!

Kuwa mkweli na muwazi huku ukitumia lugha yenye staha mwambie kama unaweza tuendelee kidogo na siyo kuongopa umefika kumbe bado matokeo yake ukikutana na msukuma mkokoteni mwenye misuli yake akakukoleza vizuri kesho unaanza kuwa mchepukaji kumbe ni wewe tu hukuwa mkweli kwa mmeo.

Siyo wanawake wote wanaweza kufika kileleni kila mara wanaposhiriki tendo la ndoa lakini kudanganya ni hatari zaidi kwa furaha yako siku za usoni.

Na wanawake karibu wote wanafurahi sana maandalizi kabla ya tendo la ndoa.

Kwa kawaida wanawake wanaweza kufika kileleni dakika ya 8 mpaka ya 13 tangu muanze kushiriki tendo la ndoa (siyo wakati wa maandalizi). Wengine wanaweza kuchelewa mpaka dakika ya 15 wengine mpaka dakika 20.

Ukiona umetumia dakika 3 na mkeo akakuambia amefika ujuwe wazi anakudanganya.

Lingine la mwisho na ambalo sipendi kulielezea sana ni usafi duni wa mwili, mavazi na maeneo yako ya siri.

Ahsanteni kwa kunisikiliza.

Tunajaribu kwa namna na njia zozote tunazoweza kuweza kufikisha ujumbe huu kwenu na pengine ikiwezekana tuwe tumeweza kubadili maisha ya watu hasa ya mahusiano hata hivyo kazi hii kubwa haiwezi kufanikiwa bila ushirikiano wako.

Ikiwa wewe ni mwanaume na unaona kuna makosa mengine wanawake wanafanya zaidi ya haya niliyoandika hapa tafadhali niandikie hapo chini kwa faida ya wengine
 
Wanakusikiliza kwa umakini mkuu.
EkBt8U8X0AE1MgX.jpg
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom