Makongoro aibuka na kudai mafisadi wako 4 ndani ya CCM

Lunyungu

JF-Expert Member
Aug 7, 2006
8,873
1,894
mahanga.jpg


Naibu Waziri wa Kazi, Ajira na Maendeleo ya Vijana, Dk Makongoro Mahanga.

Na Na Leon Bahati

NAIBU Waziri wa Kazi, Ajira na Maendeleo ya Vijana, Dk Makongoro Mahanga amesema makada wa CCM wanaodai kupambana na ufisadi wanapaswa kudhibitiwa ili wasikivuruge chama kwa kuwa mafisadi ndani ya chama hicho hawazidi wanne.

Akizungumza na gazeti hili jana Mahanga ambaye pia ni Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya CCM, alisema makada hao wasipodhibitiwa watakivuruga chama na kukifanya kipoteze viti vingi vya ubunge kwa wapinzani katika uchaguzi mkuu mwakani, kwa kudhaniwa kimejaa mafisadi.

“Hawa wanaoitwa mafisadi wako wangapi? Mbona hawatajwi?” alihoji Dk Mahanga akibainisha kuwa tathmini yake inaonyesha kuwa kelele zote za ufisadi zinawalenga watu ambao hawazidi wanne ndani ya chama hicho, na kwamba miongoni mwao, tayari wameanza kushughulikiwa.

Alipotakiwa kuwataja hao mafisadi wanne, Mahanga alisema hiyo ni tathmini yake na hakuna haja ya kutaja majina yao kwa vile wanafahamika.

Kwa kauli hiyo, Dk Mahanga anakuwa mtu wa pili ndani ya CCM kupingana na Makamu Mwenyekiti Mstaafu wa CCM, John Malecela ambaye Ijumaa iliyopita alitoa kauli kutaka mafisadi wadhibitiwe kwa nguvu zote, ili wasikiweke chama katika wakati mgumu kwenye uchaguzi huo. Tayari kauli hiyo imepingwa na Katibu Mkuu wa CCM, Yusuf Makamba.

Lakini jana Dk Mahanga alisema ajenda ya ufisadi imekuwa ikitumiwa vibaya na watu ambao wanafikiri wanajijengea mazingira mazuri kisiasa ili washinde ubunge mwakani, lakini hawafikirii kwamba njia wanayoitumia inalenga kuiharibia CCM.

“Kuna watu ndani ya chama wamedhamiria kuiangusha CCM huku wakijifanya wanapambana na mafisadi ndani ya chama,” alisema Dk Mahanga jana katika mahojiano na Mwananchi Jumapili na kuongeza:

“Kama wapinzani wangesimama majukwaani wakisema ndani ya CCM kuna mafisadi, hakuna mtu ambaye angeshangaa kwa sababu malengo yao ya kisiasa ni kukichafua chama tawala ili kianguke na wao wachukue nafasi hiyo,” alisema Dk Mahanga ambaye pia ni Mbunge wa Ukonga.

“Suala hilo linapozungumzwa hadharani na wanachama wa CCM ni hatari. Hapa wanakichafua chama na ndio wanaosaidia vyama (vya siasa) vya upinzani,” alisema.

Naibu waziri alishauri: “Kama kuna tatizo, lipelekwe kwenye vikao na siyo kwenda kupiga kelele kwenye majukwaa na kukichafua chama machoni pa wananchi.”

Alipoulizwa kama haoni kulizungumzia suala hilo hadharani kutasaidia kuzuia ufisadi nchini, alisema: “Namna suala hilo linavyozungumzwa sasa, inaonyesha kana kwamba kuna kundi kubwa la wanaCCM wanaojihusisha na ufisadi, lakini ukweli ni kwamba watuhumiwa wa ufisadi, hawazidi wanne.”

Kuhusu kuwepo kwa mtandao wa watu ndani ya CCM waliopanga mbinu za makusudi za kuwaangusha wabunge waliopo mstari wa mbele kwenye mapambano dhidi ya ufisadi, Mahanga alisema:

“Huo ni woga tu. Hakuna kitu kama hicho. Naunga mkono maelezo yaliyotolewa na Katibu wangu Mkuu (Yusuf Makamba) kupitia gezeti lenu (Mwananchi) toleo la leo jana akisema hayo ni mambo ya kufikirika,” alisema Dk Mahanga.

Alisema kuwa woga huo unatokana na baadhi ya wabunge kuwa na wasiwasi kwamba, wanachama wengine ndani ya CCM wanaweza kuchukua nafasi zao, hivyo kutumia suala la ufisadi kama njia ya kupambana nao.

Alitoa mfano kuwa katika jimbo lake tayari wamejitokeza wana-CCM saba wanaotaka kumrithi, lakini hapigi kelele kwa sababu anajua ni haki yao ya kikatiba na hana wasiwasi na yupo tayari kupambana nao kupitia michakato ya uteuzi ndani ya CCM.

“Hili liko wazi. Hata wengi wao mwaka 2005 kwenye majimbo yao walikuwepo wabunge ambao waliwaondoa na kuchukua nafasi zao,” alisema Dk Mahanga.

Alisema hata kama watu wachache wanaodaiwa kuwa ni mafisadi wakifukuzwa ndani ya CCM bado suala la wabunge kupata upinzani ndani ya chama litakuwa pale pale.

Aliwataka wana-CCM wenye nyadhifa mbalimbali kufahamu kuwa wapo wanachama wengi waliokuwa wanazitamani na hata sasa wanazitaka nafasi wanazozishikilia na wakati huo huo wapo wapya wanaojitokeza kuziwania.

Kwa upande wake, Waziri Mkuu wa Zamani, Cleopa Msuya amesema kwamba msimamo wa serikali kuhusu mafisadi unajulikana na tayari vyombo vyake husika vimeanza kuwashughulikia, hivyo akataka visiingiliwe,viachwe vifanye kazi yake.

“Mimi sina cha kusema juu ya hilo tatizo, tunaandika sana, hebu tuviachie vyombo vya utekelezaji vifanye kazi yake,” alisema Msuya ambaye alikuwa waziri mkuu katika utawala wa serikali ya awamu ya kwanza na ya pili.
 
anawabeza wenzake kwa kushindwa kuwataja
mafisadi halafu yeye anachomoa kuwataja hao 4!
ama kweli ukistaajabu ya musa utaona ya firauni.
 
Lunyungu,

Huyu jamaa ni mjinga kupindukia yaani siamini haya aliyoyasema!

“Suala hilo linapozungumzwa hadharani na wanachama wa CCM ni hatari. Hapa wanakichafua chama na ndio wanaosaidia vyama (vya siasa) vya upinzani,” alisema.
 
Sishangai na kauli ya huyu Makongoro kuwa CCm kuna mafisadi 4 tu!! Hii ni kauli ya mtu asiyejua maana ya ufisadi kwani huyu Makongoro mwenyewe ni fisadi aliyekubuhu na ndio maana akaondolewa kama naibu waziri wa miundombinu kwa kula rushwa za contractors wa barabara wachina; ushahidi ukiwa mara baada ya yeye na fisadi mwenzie kuondolewa[ kwanza alifikiri kuwa angepewa uwaziri lakini JK akamtolea nje kwani faili lake limejaa uchafu] barabara nyingi ikiwemo ile ya SAM NUJOMA -UBUNGO zikamalizika!! Makongoro ni mbunge fisadi ninaetegemea kuwa watu wa Ukonga watamtema safari hii.
 
yawezekana anawajumlisha Mramba, Yona, Chenge na yule Mweka hazina wa CCM kwenye kesi ya EPA

Kama ulikuwa kwenye akiri yangu vile, anataka kusema mafisadi wameshapelekwa mahakamani basi mambo ya ufisadi yaishe ndani ya CCM, tutayasema na kuwaunga mkono wabunge wa CCM wanaowasema mafisadi kama ataki ajinyonge
 
yawezekana anawajumlisha Mramba, Yona, Chenge na yule Mweka hazina wa CCM kwenye kesi ya EPA

Mkuu umenichekesha sana hapa, ina maana huyo aliyekuwa mweka hazina wa SISIEMU hana jina??? Ahhahaha ahahahaha ahahahaha ahaha teteteh. Mie namjua Rostam Aziz aliwahi kuwa mweka hazina SISIEMU. Wengine siwakumbuki.
 
Lunyungu,

Huyu jamaa ni mjinga kupindukia yaani siamini haya aliyoyasema!

Niliwahi kusema hapa nikapondwa, mambo haya hayahitaji kwenda darasani. Yaani kujua kuna fisadiz SISIEMU unahitaji kusoma kitabu? Nashangaa huyu jamaa ni waziri, mmh haya makubwa.
 
mwenye email yake au simu ya mkononi naomba ampatie haya majina.
Mafisadi ndani ya CCM
mkapa
apson
mboma
chenge
mgonja
rostam
dr idrisa
karamag
lowassa
arthur
mo-Dewji
JK
makamba
londa
naomba muendeleze list halafu apelekewe Dr makongoro ili awatete hao mafisadi ili akisafishe chama chake chenye mayai ya ufisadi, rejea Generali Ulimwengu.
 
Ni muhimu sana watu kuzichukulia kwa makini kauli zote zinazotolewa na madaktari feki kwa vile wameshaonyesha tabia ya kusema au kufanya jambo lolote linalowawezesha kujiongezea heshima binafsi kwenye jamii hata kama jambo hilo si la uhakika.
 
mwenye email yake au simu ya mkononi naomba ampatie haya majina.
Mafisadi ndani ya CCM
mkapa
apson
mboma
chenge
mgonja
rostam
dr idrisa
karamag
lowassa
arthur
mo-Dewji
JK
makamba
londa
naomba muendeleze list halafu apelekewe Dr makongoro ili awatete hao mafisadi ili akisafishe chama chake chenye mayai ya ufisadi, rejea Generali Ulimwengu.

Labda alimaanisha walio Dar
Hao na hawa hapa chini ni wa - kitaifa;

Yusuf Makamba
Makongoro Mahanga
Basil P. Mramba
Lau Masha
Nimrod Mkono
Vicent Mrisho
Patrick Ruta
 
Last edited:
Ila tusimlaumu sana kwa kusema CCM ina mafisadi wanne tu. Ina wezekana definition yake ya ufisadi ni tofauti na tujuavyo sisi. Ama kweli Tanzania tumepewa kila kitu lakini tumenyimwa viongozi.
 
Acheni dr atetee chama chake cha kifisadi maana kikanguka mwakani naye atakuwa pabaya kwakuwa mafisadi wote watahitajika kupelekwa kwa pilato.
 
Geoff;

Huyu jamaa ana degree ya kwanza na ya pili nzuri tuu, pia ana CSP (T) ile professional award ya materials management and procurement.

Sasa akajipa u Phd kutoka chuo feki. Akaharibu kila kitu.

Inachotakiwa ni kuitwa kwenye vikao vya chama awataje hao mafisadi. Ila kwa upeo wake ukimuuliza atakutajia wale waliojiuzulu (mawaziri) watatu na Rostam Aziz.

Hao ni rahisi sana kuwataja ukiwa ndani ya CCM.
 
Hawa ndio viongozi ambao tunategemea wawe mstari wa mbele katika kusukuma gurudumu la maendeleo.No wonder we are still poor.Kweli akina Makongoro hawa ndio watakao_mobilize resources?

Kweli twahitaji 'dictator' mwenye moyo wa kizalendo,ili tupige hatua kwenda mbele.Katika kuijenga Tanzania ninayoitamani hawa akina Makongoro hawatufai kabisa.Angekuwa Kingunge tungesema labda ni uzee,sasa huyu nae....

Hawa ndio wasioutaka 'waraka' uleeee....
 
Hivi hawa jamaa si bora wangekuwa wanakaa kimya tu! Maana kila wakiongea ni utumbo tu... Hovyo hovyo!!
 
Back
Top Bottom