Makonda: Nimeajiri wanasheria saba, nawalipa 75% ya mshahara wangu

Msulibasi

JF-Expert Member
Dec 2, 2014
5,838
7,501
Huyo ndio mkuu wa wilaya Kinondoni amewaajiri kwa fedha yake waweze kusaidia Wananchi wasiojua sheria waweze kufanya mikataba ama kufungua kesi.

Clouds TV
 
Huyo ndio mkuu wa wilaya Kinondoni amewaajiri kwa fedha yake waweze kusaidi wananchi wasiojua sheria waweze kufanya mikataba ama kufungua kesi.Clouds TV

Mshahara wa DC ni kama 2mil. Hiyo 75% anayosema ni kama 1.5mil. Watu 7 watagawanaje 1.5mil kama mshahara kama huu si uongo??
 
Napata picha kipat yaani mishahara na maslahi ya wakuu wa wilaya ni makubwa sana . Maisha bora hayawezi kumfikia mwanachi asiye mwana siasa , wataongeza wilaya mikoa na majimbo pato lote la taifa linawalipa wanasiasa fikiri mawaziri 60 kish mnajiuliza uchumi unakua wanachi masikini unagharamia ulinzi ,usalama na utawala
 
Huyo ndio mkuu wa wilaya Kinondoni amewaajiri kwa fedha yake waweze kusaidi wananchi wasiojua sheria waweze kufanya mikataba ama kufungua kesi.Clouds TV

Huyu naye ache kudanganya Watu ..akadanganye watoto ..mshahara wa Mkuu wa wilaya take home 2m ..asilimia 75 ni Kama 1.5 m kwa wanasheria 7 Ina maana anawapa laki 2 kwa mwezi ....bado gharama za ofisi .....haingii akilini .
Yeye Kama dc anabaki na sh 500'000 ...tuseme anaishije kwa kuomba omba au kwa kutukana Watu apate pesa ...au hawa ndio ngombe wanaofugwa mjini ???
Nadhani Mkapa alikuwa sahihi ..kuporomoka kwa utumishi wa umma ..tulizoea wakuu wa wilaya ni civil servants wazoefu wana panda cheo ..lakini Sasa ni any one ...kiasi kimekuwa cheo bogus kuliko vyote NCHI Hii .... ...kazi za kuuza sura tu ..na bongo movie

Au aseme to kuwa anataka kumtoa Iddi Azan tumuelewe
 
Kwani tatizo liko wapi? Kwa hiyo mlitaka hao wananchi watetewe na nani? Bigup makonda komaa nao tu.
 
Wanasheria saba kwa 75% ya mshahra wake. . .,. . . . .Labda kama wanakula na kulala kwake. . . . wako mfuko gani wa pensheni na bima ya afya kampuni gani??!!

Tatizo la wakuu wa wilaya ambao hata hawajui mfumo wa kuendesha NCHI ....Mkuu wa wilaya ofisi yake Ina kitengo cha sheria ....Kina wanasheria ..akitoka hapo bado anao uwezo wa kuwatumia wanasheria wa manispaa ....,wakielemewa anauwezo wa kuomba mashirika ya kutoa misaada ya sheria ...Sasa iweje aanzishe ofisi mpya ...mwanasheria wa wilaya au manispaa wanaangalia tu ...au kawadharau Au ni wabovu awafukuze kazi .....mwenzake Korogwe alimuambia mwanasheria wa wilaya Ana degree wa chupi ...akaishia tume ya maadili na chupi akavikwa yeye kichwani !!!!
 
Hehehe hii nchi hii...!!!

Kwa hiyo hao wanasheria wapo chini ya ofisi ya wilaya au ofisi binafsi ya Makonda?
 
Umesema vema hapo juu mkuu. . . . .kuporomoka kwa utumishi wa umma
 
Huu ndio mwaka wa uchaguzi..tutasikia mengi sana. Tatizo "cheap popularity".

Kaonge asubuhi kabla hata hajaanza kazi nimeshangaa sana kwamba unawezaje kuanzisha taasisi ndani ya taasisi , yule kijana mtangazaji kamuuliza swali zuri sana kwamba hii nafasi ni ya kuteuliwa ,je akija mtu mwingine akakutoa hapo itauwaje? Hili jambo lilitakiwe lijadiliwe kwa kina na mamlaka ,to me its an abuse of power, huwezi kutangaza hadharani kuwa umewaajiri bora angesema huwa nawaomba wanisaidie kwa makubaliano fulani si ajira. Hatari moja wapo ni mgongano wa kimaslahi na wanasheria wa ukweli wa wilaya na pia inaweza kuwa taasisi ya kuchochea rushwa sedta ya ardhi hapo wilayani, mkuu wa mkoa fuatilia hili jambo
 
Hehehe hii nchi hii...!!!

Kwa hiyo hao wanasheria wapo chini ya ofisi ya wilaya au ofisi binafsi ya Makonda?

Kasema wako ofisini kwake ukiweza kupata video ya hicho kipindi ungalishangaa kama unamuona mkuu wa wilaya.Kuna siku huwa anazitoa kila wiki kwenda kufanya kazi katika kata naona huyu anakuwa mbunge labda
 
Ati nini? Yani atoe 75% ya mshahara wake kila mwezi!! Kwa mpango gani na utaratibu upi??
aache uzushi
 
Duh asilimia 75 ya mshahara wake ana tumia kulipa wanasheria,asilimia 25 ndio matumizi ya nyumbani,kununulia chakula,nguo,kusomesha watoto,kuwasaidia ndugu zake n.k,ingekuwa enzi zile ambapo uadilifu ulikuwa ndicho kigezo kikuu cha kumfanya mtu apewe uongozi au aendelee kuwa kiongozi angeweza kuulizwa hizi fedha anazo walipa wanasheria ana zitoa wapi?
 
Back
Top Bottom