Kalunguine
JF-Expert Member
- Jul 27, 2010
- 2,543
- 134
Mwanzo wa Anna Makinda katika nafasi ya Uspika unaonyesha kuwa hakufaa kuwa Spika. Kama hawezi kusoma na kuzielewa kumbukumbu sahihi za bunge ni sababu tosha ya kumfanya asifae kuwa Spika wa bunge la Tanzania. Kwa kusema kwake kuwa hajui maana ya neno fisadi zaidi ya mwizi wa mme wa mtu inaonekana ama hazisomi Hansard au akisoma haelewi, na hivyo hafai kuwa Spika. Neno fisadi linaeleweka vizuri katika siasa za Tanzania kuwa ni mwizi mkubwa wa mali za umma, mali za wananchi wa Tanzania. Zaidi ya kufahamika vizuri miongoni mwa raia wa kawaida wa Tanzania neno fisadi limetumika mara nyingi katika kumbukumbu sahihi za bunge yaani Hansard likiwa na maana hiyohiyo ya wizi mkubwa wa mali za umma. Makinda anaposema fisadi ni mwizi wa mke wa mtu ina maana viongozi wa serikali ya CCM wanatumia ofisi za serikali kuiba wake za watu?
Neno ufisadi linametumika mara sita katika Hansard ya tarehe 15.02.2008. Lipo kurasa za 53 (mara mbili), 54 (mara mbili), 47 (mara moja), 59 (mara moja). Vilevile neno ufisadi limetumika katika Hansard ya tarehe 31.01.2008 katika ukurasa wa 74. Zaidi ya hapo neno ufisadi limetumika katika Hansard ya tarehe 28-29/11/2007 na linaonekana ukurasa wa 84. Anna Makinda akasome kurusa hapa chini. Zaidi ya kutumika katika siasa za Tanzania neno ufisadi na mafisadi limetumika pia katika nchi za Afrika Mashariki hususani Kenya likiwa na maana hiyohiyo ya wizi wa mali za umma. Kwa kumkumbusha linaambatanisha pia video inayoelezea mapambano ya ufisadi wa wizi wa mali za umma nchini Kenya. Tena Mwai Kibaki anasema wezi wa mali za umma hawafai kuishi. Sasa inakuwaje leo Spika wa bunge la wananchi wa Tanzania aseme kuwa hajui ufisadi ni nini? Kwa kauli yake hiyo hakufaa kuongoza chombo cha wananchi wa Tanzania. Bunge siyo chombo cha mafisadi ni chombo cha wananchi.
1. http://www.parliament.go.tz/Polis/PAMS/Docs/HS-10-11-2008.pdf, 15.02.2008
2. http://www.parliament.go.tz/POLIS/PAMS/Docs/HS-10-3-2008.pdf, 31.01.2008
3. http://www.parliament.go.tz/bunge/docs/richmond final.pdf
YouTube - Kibaki Apinga Ufisadi