Wanu Hafidh Ameir Ashiriki Mkutano wa Kwanza wa Bunge la Pamoja la ACP-EU

Stephano Mgendanyi

JF-Expert Member
May 16, 2020
1,900
944
Wanu Hafidh Ameir, Mbunge wa Viti Maalum ameshiriki katika Ufunguzi wa Mkutano wa Kwanza wa Bunge la Pamoja la ACP-EU chini ya Mkataba Mpya wa Samoa uliosainiwa mwezi Novemba 2023.​

Wanu Hafidh Ameir ameongozana na Ujumbe wa Tanzania ulioongozwa na Naibu Spika, Mussa Azzan Zungu na Jestas Nyamanga ambaye ni Balozi wa Tanzania nchini Ubelgiji na Mwakilishi wa Tanzania katika Umoja wa Ulaya

Aidha, Naibu Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mussa Azzan Zungu (Mb), ameongoza ujumbe wa Tanzania katika ufunguzi wa Mkutano wa Kwanza wa Bunge la pamoja la ACP-EU chini ya Mkataba Mpya wa Samoa uliosainiwa Mwezi Novemba, 2023.

Katika Mkutano huo ujumbe wa Tanzania ulikubali mkataba mpya uangalie maslahi ya vijana na uwezeshaji wa wanawake katika nadharia ya kuufanya Mkataba wa Samoa uwe zaidi mikononi mwa wanajamii yaani ‘people centred agreement’.

Akizungumza katika Mkutano huo, Naibu Spika Zungu, aliweka msisitizo kuhusu mahusiano ya ACP-EU chini ya Mkataba mpya wa Ubia wa Samoa kwamba “kipaumbele kitolewe katika kuhakikisha maliasili zilizopo katika Nchi za ACP zinanufaisha wananchi wake kwa kusaidia uendelezaji wa viwanda vya kutengeneza bidhaa badala ya kusafirisha malighafi kwenda Nchi za Umoja wa Ulaya na baadae Nchi hizo kutuuzia bidhaa. Hii itakuza uchumi wa Nchi za ACP ikiwa ni pamoja na kuongeza ajira kwa vijana"
 
Attachments

  • WhatsApp Image 2024-02-24 at 22.51.03.jpeg
    WhatsApp Image 2024-02-24 at 22.51.03.jpeg
    54.4 KB · Views: 2
  • WhatsApp Image 2024-02-24 at 22.51.02.jpeg
    WhatsApp Image 2024-02-24 at 22.51.02.jpeg
    49.4 KB · Views: 3
  • WhatsApp Image 2024-02-24 at 22.51.03(1).jpeg
    WhatsApp Image 2024-02-24 at 22.51.03(1).jpeg
    66.7 KB · Views: 2
Wanu Hafidh Ameir, Mbunge wa Viti Maalum ameshiriki katika Ufunguzi wa Mkutano wa Kwanza wa Bunge la Pamoja la ACP-EU chini ya Mkataba Mpya wa Samoa uliosainiwa mwezi Novemba 2023.​

Wanu Hafidh Ameir ameongozana na Ujumbe wa Tanzania ulioongozwa na Naibu Spika, Mussa Azzan Zungu na Jestas Nyamanga ambaye ni Balozi wa Tanzania nchini Ubelgiji na Mwakilishi wa Tanzania katika Umoja wa Ulaya

Aidha, Naibu Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mussa Azzan Zungu (Mb), ameongoza ujumbe wa Tanzania katika ufunguzi wa Mkutano wa Kwanza wa Bunge la pamoja la ACP-EU chini ya Mkataba Mpya wa Samoa uliosainiwa Mwezi Novemba, 2023.

Katika Mkutano huo ujumbe wa Tanzania ulikubali mkataba mpya uangalie maslahi ya vijana na uwezeshaji wa wanawake katika nadharia ya kuufanya Mkataba wa Samoa uwe zaidi mikononi mwa wanajamii yaani ‘people centred agreement’.

Akizungumza katika Mkutano huo, Naibu Spika Zungu, aliweka msisitizo kuhusu mahusiano ya ACP-EU chini ya Mkataba mpya wa Ubia wa Samoa kwamba “kipaumbele kitolewe katika kuhakikisha maliasili zilizopo katika Nchi za ACP zinanufaisha wananchi wake kwa kusaidia uendelezaji wa viwanda vya kutengeneza bidhaa badala ya kusafirisha malighafi kwenda Nchi za Umoja wa Ulaya na baadae Nchi hizo kutuuzia bidhaa. Hii itakuza uchumi wa Nchi za ACP ikiwa ni pamoja na kuongeza ajira kwa vijana"
Asante kwa kurusha jiwe gizani!
 
Back
Top Bottom