Spika Anna Makinda kwa mara nyingine tena amewafunga midomo wabunge kwa kukataa hoja yoyote binafsi ambayo ilikuwa inataka kujadili swala la gesi ya Mtwara eti kwa kisingizio kwamba kuwa ni zito na nyeti, linalopaswa kujadiliwa kwa hekima kubwa na busara ya kutosha ili kupata muafaka wa kweli.
Swali ni kwamba wabunge waliochaguliwa na watanzania hawana busara za kutosha kujadili maswala la kitaifa???? na nina anapaswa ajadili maswala yetu??
Huu ni muendelezo mwengine wa kubananga demokrasia.
Sauti ya wabunge ni sauti ya wapiga kura wa Tanzania. She shouldn't stop people's voice. Ingawa kwa upande wake anadhani ni busara, wengi wa wabunge hata wa chama chake wanaona ni dhana ya UOGA kama nionavyo mimi. Auache huo uoga jambo lijadiliwe NOW
Menopose na upweke ni stress kila uendako
Heshima mkuu.kwa mtazamo wangu hili ni tusi baya sana kwa wazazi wetu wote na sio kwa huyu bibi tu kwani ukimshutumu mtu kwaajili ya kitu ambacho ni relating to or concerning nature. hapo ebu jaribu kumfikria mtu mwingine amwambie hivyo mama yako mzazi utajisikiaje? hata kama tunaichukui ccm pamoja na watu wake lakini tujaribu kuwasilisha hisia zetu kwa namna ambayo inaweza kuwa sio matusi. uliposema hivyo nimemwona mama yangu na nikajihisi vibaya sana
maswali yanazidi kuongezeka kila kukicha lakini ukweli ni kwamba binadamu mwenye akili timamu akiamua kukaa faragha na kutafakari kwa makini ni lazima ashangae ni jinsi gani posts muhimu za nchi hii watu wanaozishikilia walizipataje ukichukulia kuwa kuna binadamu wengine katika sayari hii ambao tayari wanafanya mambo tunayoyafanya!!dah!
huyu ndiye spika wa bunge...labda tukumbushane alipataje hiyo nafasi
Ila hujaona kama bi kiroboto kawatukana watanzania wote, wabunge ni wawakilishi wa wananchi sasa kama wabunge wooote hawana busara ya kujadili hoja nyeti( kwa tafsiri ya bi kiroboto) basi hata hao waliowachagua hao vilaza na wenyewe ni vilaza pia.Ameanza yeye wacha wengine wamalizie, hastahili tena kuheshimiwa.