Makinda amepewa escot ya polisi?

huyo mama si wangemwamisha kwanza huko Kijitonyama maana kuishi mbali na town halafu na hiyo misafara kwa kweli inakera, Leo msafara wake ulikuwa unapita rightside ya barabara kwa jinsi foleni ilivyokuwa imefunga.

Ala, kumbe ni kweli?
 
Viongozi wenye stahili ya escort ni rais, makamu wa rais na waziri mkuu. Viongozi wengine hupewa escort pale wanapolazimika kuwahi katika shughuli muhimu ilhali ikihofiwa barabara zitakuwa hazipitiki kirahisi. Viongozi hawa ni spika wa bunge, mkuu wa majeshi, jaji mkuu, IGP, baadhi ya mawaziri, mabalozi na wakuu wa mashirika ya umoja wa mataifa.
 
Sasa Madcheda unapinga kwamba CAG hana Escort au Mutungusha hakumuona na Escort last week? Kwani Ulishinda Ali Hassan Mwinyi week yote nzima ukiangalia magari yanayopita na hukumuona CAG akipita? Hebu niweke sawa kidogo kamanda.

Labda mjomba wangu huwezijua,ny me nlikua nazan huyu bwana anasema spika anapewa escort full time si ndio?mana kma ni occasionally hawa watu wanapewa escort ila sio always jmn.
 
Wakuu, kila siku huwa napishana na makinda asubuhi akienda ofisini Dar. Huwa anakuwa kwenye Benz au sahangingi bila msafara wa polisi.

Leo jioni nimepishana na msafara wa pikipiki ya polisi na shangingi mbili nyeusi. Shangingi moja plate number yake ilikuwa imeangikwa S.

Sikuweza kuona nani walikuwa ndani kwenye kila gari. Dereva wangu aliniambia alimuona Makinda kwenye ile gari yenye plate numba ya S. Sina hakika kama ni kweli.

Kwa mwenye taarifa za uhakika, je ni kweli Makinda amepewa ulinzi na msafara wa polisi?

lazima ifahamike kuwa Spika ni mmoja wa mihimili mikuu ya nchi.

Yupo yeye, Jaji mkuu na rais.

Kifupi Spika hana escot yoyote kama ilivyo kwa jaji mkuu ila kama kutakuwa na kazi maalum. Hivyo ndivyo ninavyofikiri mimi
 
Viongozi wenye stahili ya escort ni rais, makamu wa rais na waziri mkuu. Viongozi wengine hupewa escort pale wanapolazimika kuwahi katika shughuli muhimu ilhali ikihofiwa barabara zitakuwa hazipitiki kirahisi. Viongozi hawa ni spika wa bunge, mkuu wa majeshi, jaji mkuu, IGP, baadhi ya mawaziri, mabalozi na wakuu wa mashirika ya umoja wa mataifa.

Majambazi wakiwa wanapelekwa kisutu... na wafungwa wakiwa wanawahi chakula segerea...
 
hata angepewa escort ya jeshi la wananchi,tatizo ni nini?si ni kiongozi wa mhimili mkubwa wa nchi au?
 
ukiona hivyo ujue kuwa maadui wa haki wamekuwa wengi, nchi wataiona chungu! hiyo sio eskoti bali ni ishara ya wao kukosa amani kwa sababu wanayowafanyia raia hayaendani na wao kutembea bila kuwa na eskoti! Pole sana mama yangu kwa kitanzi ulichojiwekea. Napendekeza viongozi wote wa CCM pamoja na familia zao wapewe eskoti ili maisha bora kwa kila mtanzania yatimie. OLE WENU AKINA KIKWETE MAANA MAOVU YENU YAMEKUWA SHUBIRI KWA MAISHA YENU!
 
hata angepewa escort ya jeshi la wananchi,tatizo ni nini?si ni kiongozi wa mhimili mkubwa wa nchi au?

Ni matumizi ya pesa zetu, na msafara wake unatufanya tuchelewe kwenye shughuli zetu. Hujambo wewe
 
mh. Sita alipoomba ulinzi walimkebehi kwa vile rostam hakuridhia, sasa makinda mtu wao ameboronga wanahangaika kumlinda, kama hizi taarifa ni za kweli inasikitisha.

Maspika wote waliotangulia sijawahi ona wakiwa na ulinzi/msafara, mh. Sita tunasali nae kkkt kinondoni alikuwa anakuja bila escot, hata msekwa sikuwahi ona akipewa escort (isipokuwa kuna siku alikaimu urais kwa mujibu wa katiba, labda kama nae kakaimu)

na bado mchecheto utazidi si amekubali kutumika na wenye dhambi, hakuna baraka hapo ni hofu tu kwa kwenda mbele.


kwa maandishi makubwa nakubali. Ukitenda dhambi au kushiriki kutenda au kufanikisha dhambi unakuwa na hofu. Bibi makinda ana hofu mbayaaaaaaaaa! Kama ulimwona baada ya kusema ushahidi uletwe kwa maandishi alikuwa anaongoza bunge bila confidence kabisa. Maana yake alikuwa nahofuuuuuuuuuuuu. Na bada ngoja mwezi wa nne tena mpaka presha impande.........teh teh teh teh teh!!!!!
 
Majambazi wakiwa wanapelekwa kisutu... na wafungwa wakiwa wanawahi chakula segerea...

Kwa sababu majambazi hawajathibitishwa kuwa na hatia , bado ni raia huru na wafungwa hawatembezwi barabarani labda kama wana kesi nyingine za kujibu.
 
Jamani, huyu ni kiongozi wa mhimili wa dola (utawala), kuna ubaya gani wa yeye kuwa na msafara na ulinzi?


Kiongozi hata mimi nashindwa kushangaa, kwa nchi tajiri kama TZ wangetakiwa hawa viongozi wote wanatumia helicopters hasa DSM kupunguza foleni. Ndio shida ya watu weusi wana wivu kweli wewe maisha bora kwa kilamtanzania yanaonekana wazi kabisa halafu unashangaa kiongozi mkuu kama spika akipewa escort ya polisi, hivi si ndio vipaumbele vya wananchi.
 
Barabara zenyewe ziko wpi kuwa na misafara mia kidogo, wanawasumbua tu wananchi watumie helcopter
 
nadhani ndugu zangu kuna ki2 tunajadiliana bila kujua tunachojadili,umeona akiwa na swipa au escort?swipa ni pikipiki inayotangulia mbele kuashiria watumiaji wengine wa barabara waache kuitumia,escort ni gari la walinzi ambalo wanaweza kuwa maafisa usalama wa police,jeshi,au tiss.wanaostaili n kupewa escort ni rais e1,makamu e2,rais wa smz e3,wz mkuu e4,wakamu wa 1smz e5,wa2 e6,wengine ni mkurugenzi wa tiss,mkuu wa majeshi,firt lady.
 
Viongozi wasipende sana escort. Kama kiongozi ni mbaya usije ukajihakikishia kuwa wale wanaokuescort wanakupenda na uko salama. Wajifunze kwa Kabila wa Kongo na viongozi wengine waliotunguliwa na walinzi wao. Escort sio suluhisho kuwa kiongozi anakuwa salama. Sita mbona hakuwa na escort. Nina uhakika Spika wa Sasa kwa kuwakumbatia mafisadi anatengeneza uadui kwa wananchi kila kukicha. Ndio maana ya kupewa escort.
 
Back
Top Bottom