Makinda amepewa escot ya polisi?

Gurudumu

JF-Expert Member
Feb 5, 2008
2,349
261
Wakuu, kila siku huwa napishana na makinda asubuhi akienda ofisini Dar. Huwa anakuwa kwenye Benz au sahangingi bila msafara wa polisi.

Leo jioni nimepishana na msafara wa pikipiki ya polisi na shangingi mbili nyeusi. Shangingi moja plate number yake ilikuwa imeangikwa S.

Sikuweza kuona nani walikuwa ndani kwenye kila gari. Dereva wangu aliniambia alimuona Makinda kwenye ile gari yenye plate numba ya S. Sina hakika kama ni kweli.

Kwa mwenye taarifa za uhakika, je ni kweli Makinda amepewa ulinzi na msafara wa polisi?

Yup, Speaker ana msafara na ana official S-class pamoja na landcruisers...inategemea yuko wapi ndo anatumia one or the other, akienda kwao utapishana na landcruisers tatu au nne.

Yup, Speaker ana msafara na ana official S-class pamoja na landcruisers...inategemea yuko wapi ndo anatumia one or the other, akienda kwao utapishana na landcruisers tatu au nne.

Imeanza lini mkuu?

Mh. Sita alipoomba ulinzi walimkebehi kwa vile Rostam hakuridhia, sasa Makinda mtu wao ameboronga wanahangaika kumlinda, kama hizi taarifa ni za kweli inasikitisha.

Maspika wote waliotangulia sijawahi ona wakiwa na ulinzi/msafara, Mh. Sita tunasali nae KKKT Kinondoni alikuwa anakuja bila escot, hata Msekwa sikuwahi ona akipewa escort (isipokuwa kuna siku alikaimu urais kwa mujibu wa katiba, labda kama nae kakaimu)

Na bado mchecheto utazidi si amekubali kutumika na wenye dhambi, hakuna baraka hapo ni hofu tu kwa kwenda mbele.

Wakuu, kila siku huwa napishana na makinda asubuhi akienda ofisini Dar. Huwa anakuwa kwenye Benz au sahangingi bila msafara wa polisi.

Leo jioni nimepishana na msafara wa pikipiki ya polisi na shangingi mbili nyeusi. Shangingi moja plate number yake ilikuwa imeangikwa S.

Sikuweza kuona nani walikuwa ndani kwenye kila gari. Dereva wangu aliniambia alimuona Makinda kwenye ile gari yenye plate numba ya S. Sina hakika kama ni kweli.

Kwa mwenye taarifa za uhakika, je ni kweli Makinda amepewa ulinzi na msafara wa polisi?

Nimepigwa mkono muhimbili primary S apite mhhhhh nimeshanga hata spika msafara? Makubwa!

nahisi atakuwa anamkaimu rais kwa mujibu wa katiba coz jamaa hayupo na makam wake sina uhakika yuko pande zip maana hasikiki.

Jamani nami niombeeni Escort!

Najua wengi watauliza kwani we nani?

Mie ni mtanzania kama wengine.

nahisi atakuwa anamkaimu rais kwa mujibu wa katiba coz jamaa hayupo na makam wake sina uhakika yuko pande zip maana hasikiki.

Ikiwa hivyo wananchi hutangaziwa mkuu, na akiwa anakaimu msafara huwa Kama ule wa rais. Huu ulikuwa pikipiki moja na magari mawili tu.

Jamani, huyu ni kiongozi wa mhimili wa dola (utawala), kuna ubaya gani wa yeye kuwa na msafara na ulinzi?

unashangaa ya spika??? last week nliona CAG aly hassan mwinyi road akiwa na escot ya police!!!!

Hakika watanzania tunahitaji katiba mpya....wanaostahili kupewa escot wanaongezeka kila kuchwao. Ingawa sipingi wanaostahili kupewa escot nahisi kwa nchi yetu na tulipofikia imekua holela. Kwa foleni hizi naona kila mtu anapitishwa na escot siku hizi.

Wanaopewa escoti wanaongezeka kwa sababu wanafanya upumbavu. Maamuzi yao yamekuwa ya kijinga na kukosa burara. Kwa sababu hii lazima waogope. Nyerere alisema mkianza kuona tunalindwa kila mahali mjue tumeanza kuwaibia. Kuanza kulindwa na kusindikizwa ni uthibitisho tosha kwamba makinda hafanyi kazi ya wananchi bali kazi ya mafisadi.

unashangaa ya spika??? last week nliona CAG aly hassan mwinyi road akiwa na escot ya police!!!!

Hilo napiga kwa nguvu zote CAG hana escort hata siku moja. But anyway nilishaona kwa macho yangu jaji mkuu,mkuu wa majeshi,mkuu wa polisi wakiwa na escort na mama salma pia nlishakutana akiwa na escort pia

Watakoma maana kuna wahuni wamejipanga kuwafanyia vibaya, si uliona advertise zao kule kwenye msiba gongolamboto!!! walipiga 7 hewani na wakaondoka sasa watashindwa kumkamata Makinda???

Back
Top Bottom