BAK
JF-Expert Member
- Feb 11, 2007
- 124,789
- 288,020
Makamba amtaka Tambwe atubu
2009-03-26 12:32:29
Na Thobias Mwanakatwe, Mbeya
2009-03-26 12:32:29
Na Thobias Mwanakatwe, Mbeya
Katibu Mkuu wa Chama cha Mapinduzi (CCM), Yusuf Makamba, amewataka Hizza Tambwe na Lucy Rutainurwa kutubu kutokana na kushiriki kusema uongo walipokuwa vyama vya upinzani ili wananchi waichukie CCM.
Tambwe kabla ya kujiunga na CCM, alikuwa Mkurugenzi wa Habari,Uenezi na Sera Chama cha Wananchi (CUF) huku Rutainurwa alikuwa Mwenyekiti wa (TLP) Mkoa wa Dodoma ambapo wote walirejea CCM.
Makamba ambaye yupo katika ziara mkoani Mbeya, akiwa ameambatana na Tambwe kama Kaimu Katibu wa Kitengo cha Propaganda cha CCM makao makuu na Rutainurwa, aliyasema hayo jana wakati akiwahutubia wananchi wa Kata ya Uyole.
[COLOR="Red]``Tambwe na Lucy wakati wapo vyama vya upinzani walikuwa waongo sana, sijui watasema nini kwa Mungu, itabidi wakatubu kwa kushiriki kusema uongo,`` alisema Makamba na kumwita Tambwe jukwaani kuwaeleza wananchi waliokuwepo hapo sababu za kujitoa CUF na kujiunga na CCM.[/B][/COLOR]
[COLOR="Blue"]Makamba alikiri kuwa Tambwe wakati akiwa CUF alikuwa anaisumbua sana CCM na kwamba aligombea ubunge Temeke mara tatu mfululizo.
Pia bosi huyo wa CCM alisema hata Rutainurwa alikuwa anakisumbua mno chama chake wakati akiwa TLP na hata aliupogombea ubunge.
Kwa upande wake, Tambwe alisema CCM kamwe haitaweza kung`oka madarakani labda miaka 150 ijayo kwa sababu chini ya serikali ya serikali yake, wananchi wanaishi kwa matumaini kutokana na kuleta maendeleo makubwa nchini.
Tambwe alidai kuwa wapinzani wanapenda kutumia umaskini wa Watanzania kuwatia hasira.
Naye Rutainurwa alidai kuwa vyama vya upinzani siku zote vinapenda kuwashawishi vijana wanaokaa vijiweni kwa sababu ni wapiga kelele wazuri lakini kimsingi havina dira wala mwelekeo[/color]