Makamba akataa CCM kukutana na Chadema

....hao wakina Makamba wamebakia kung'ang'ana na CCM tu,,,,hata CCM ikiiiba mchana mchana na watu wanaona atasema hawajaiba,,,,THEY ARE BLINDED BY POLITICS!
 
Nilipomsikia Mbowe juzi akisema wako tayari kukaa na CCM kuzungumza nikajua issue yote kwinshee!! Ingawa nimelipenda sana jibu la Makamba, lakini bado wana chadema wana nafasi (wakiamua kwa pamoja) ya kukaa na kujadili na kupanga mikakati ya kurudisha hoja majukwaani (kwa wananchi). Kwa kipindi kirefu sasa (takribani miaka 3) CCM wamepoteza mvuto kwa wananchi katika kujibu hoja za wapinzani kupitia majukwaa ya kisiasa.

Nawashauri chadema wasirogwe kuongea na CCM wala serikali yake, wala wasiwe kimya kama wanavyofanya sasa, wajipange na waandae hoja nzito za kwa nini wanaamini NEC sio huru na umuhimu wa kuwa na Katiba mpya. Kisha kabla ya kikao cha bunge kuanza mwezi Februari mwakani wawe tayari wamezunguka angalau mikoa 10 mikubwa kuelezea hoja zao kwa wananchi.

Hii itawapa boost sana na kuwalazimisha CCM waanze ku react, na kutokana na uzoefu tulionao CCM normally hawako strategic katika ku react na mara nyingi wamekuwa wakijichanganya hovyo hovyo. Hii itawapa Chadema nguvu na support kubwa kutoka kwa wananchi na pengine serikali kukubali kuanza mchakato wa kuandaa katiba mpya.

Vinginevyo Chadema wameula achuya na wanatulazimisha tuamini kwamba ushindi wa viti vingi vya wabunge walioupata katika uchaguzi uliopita ulikuwa ni wa kubahatisha na sio matokeo ya mipango madhubuti ya muda mrefu ya kushika dola.

Mvurugano huu utawarudisha nyuma si tu chadema bali vyama vyote vya siasa na kusababisha ile ndoto ya kuing'oa CCM kuwa kitu kisichowezekana kwani wananchi watapoteza uaminifu kwa vyama hivi.

Nani atawaruhusu CDM wazunguke mikoa 10 mikubwa? Hiyo itachukuliwa kama mizunguko ya uvunjifu wa amani nchini.
 
haisemi hivyo lakini kanuni za Bunge zinaruhusu hoja kutolewa na ikipitishwa na kukubaliwa basi ina nguvu ya kisheria. Kwa hiyo utasikia hoja inaanza na "kwa vile ... "halafu litatolewa pendekezo la kuwafukuza Bungeni wale wanaoafiki waseme "ndiyo" (176 hivi watasema ndiyo) na wale wasiofiki waseme "hapana" karibu 46 watasema hapana. Waliosema ndiyo "wameshinda" nawabunge wa Chadema watatakiwa kuomba msamaha au kutoka kimoja Bungeni!


wanatoka kimoja bungeni kwa maana ya kuvuliwa ubunge kabisa au kutohudhuria vikao vya bunge? km ni kutohudhuira vikao vya bunge tu basi nashauri wajiandae na hoja za nguvu watakazotoa kwa wananchi ili wananchi wazidi kuichukia CCM, ila naamini hawawezi kufukuzwa bungeni maana CCM wanaogopa kimbunga cha wananchi, naona pia itakuwa ngumu kuwafukuza maana kisheria ndo wanaounda serikali kivuli bungeni.
 
SIKU moja baada ya Chadema kusema ipo tayari kuketi meza moja na serikali, chama tawala au taasisi nyingine yoyote kwa ajili ya mazungumzo, katibu wa CCM, Yusuf Makamba amesema chama hicho hakina muda wala sababu ya kuketi pamoja na wapinzani hao.

Mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe alisema juzi kuwa wako tayari kukaa meza moja na serikali au wadau hao ili kujadiliana nao kuhusu msimamo wao wa kupinga matokeo ya uchaguzi wa rais, madai ambayo yameimarisha hoja ya kuundwa kwa katiba mpya na tume huru ya uchaguzi.

Hata hivyo, Mbowe aliweka bayana kuwa mazungumzo hayo yasiwe ya kuweka mbele maslahi ya kisiasa na wala yasijikite kwenye kauli zinazotolewa na Makamba na katibu wa itikadi na uenezi wa CCM, John Chiligati na badala yake yaweke maslahi ya taifa mbele.

Lakini jana Makamba alisema chama chake hakina jambo lolote la kuzungumza na Chadema na kwamba sasa siasa zinahamia bungeni.


Makamba,ambaye huzungumza kwa mifano ya vichekesho na pia kutumia vitabu vitakatifu vya Biblia na Qorani, alianza kunukuu kifungu kitabu cha Methali 18:18 katika Biblia kinachosema: "Kura hukomesha mashindano; hukata maneno ya wakuu.

"Sisi wote tulikwenda kwenye uchaguzi, kura zikapigwa, aliyeshinda anajulikana na walioshindwa wanajulikana, sasa sisi tukutane na Chadema tuzungumze nini? Wao watafute watu wengine wa kuzungumza nao si CCM."


Kwa mujibu wa Makamba, kwa sasa siasa zinahamia bungeni na kwamba endapo Chadema wanataka siasa za nje ya Bunge, wasubiri tena mwaka 2015 wakati wa uchaguzi mkuu.

"Tutakutana bungeni kwenye kujadili sera, kwa sasa sisi tunaunda serikali," alisema Makamba ambaye katika Bunge la Tisa alikuwa mbunge wa kuteuliwa na rais.

Naye mkurugenzi mtendaji wa taasisi isiyo ya kiserikali ya kukuza demokrasia nchini inayoitwa Agenda Participation 2000, Moses Kulaba alipongeza uamuzi wa Chadema, lakini akaonyesha wasiwasi kama serikali itakuwa tayari kukaa na chama hicho.

"Ni jambo jema kwa Chadema kukubali maridhiano, lakini serikali itakuwa tayari kuzungumzia mambo haya," alisema Kulaba.


Kulaba alisema mapambano yaliyoanzishwa na Chadema yanatakiwa yawe chachu ya kudai mabadiliko ya katiba pamoja na tume huru ya Uchaguzi baada ya hii iliyopo kulalamikiwa tangu uchaguzi unaoshirikisha vyama vingi uliporejeshwa mwaka 1995.

"Kilio cha kudai hivi vitu kilianza tangu mwaka 2000, sasa inatakiwa Chadema iwe chachu ya mabadiliko hayo. Zanzibar wamefanya mabadiliko ya katiba; uchaguzi umeenda vizuri hakuna malalamiko kwanini ishindikane Tanzania Bara," alihoji Kulaba.


"Tume ya Uchaguzi ni chombo muhimu sana, lakini pamoja na malalamiko ya miaka yote, kutoka mwaka 1995 mpaka leo, (Jaji Lewis) Makame amekuwa mwenyekiti wa tume hiyo," alisema Kulaba.

Naye Mhadhiri wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam Bashiru Ally, alisema bado Chadema haijaweka bayana madai yao ili wananchi waweze kuwaelewa. Bashiru alisema baada ya waangalizi wa uchaguzi kutoa ripoti zao kamili, itakuwa ni wakati muafaka wa kujua kilichotokea katika uchaguzi huo.


- It makes a lot of sense, CCM wameelewa kwamba zile ni siasa tu za kawaida katika Demokrasia saafi sana, sasa wakapambane kwenye majukwaa ya siasa ndio itaeleweka nani ana hoja na nani hana!


- Kwa majibu haya ni very clear kwamba Mh. Chiligati, alikurupuka alipotishia kuwafukuza waliosusia na kutaka kuifanya a non ishu kuwa ishu for nothing!


William
 
Back
Top Bottom