Makamba akataa CCM kukutana na Chadema

CHADEMA wakomae na kudai marekebisho ya KATIBA, kwa kuendelea kutokutambua matokeo ya urais.

Makamba ameisha jua janja ya Mbowe. Baada ya CCM kusema wanapeleka Azimio Bungeni la kuwatoa CDM Bungeni, Mbowe ndio amekuja na staili hii ya kusema kukaa meza na Serikali. Na wakiendelea na msimamo wao huu CDM hawataliona bunge hii, watatolewa nje kwa azimio la bunge.
 
Hivi kwa nini CHADEMA wanachelewa kuweka wazi ushahidi kamili wa jinsi kura za nec na zile zilizosainiwa na mawakala jinsi zinavyotofautiana?Bado tu wanakusanya taarifa?Kuchelewa huku ndiko kunawafanya wananchi wapoteze imani nao.Chondechonde CHADEMA ebu kamilsheni hili,ili kuongeza nguvu ya madai yenu pia kuamsha upya imani na ari ya wananchi kudai kura zao zilizo bakwa.
 
Kama hawana jee?
 
haisemi hivyo lakini kanuni za Bunge zinaruhusu hoja kutolewa na ikipitishwa na kukubaliwa basi ina nguvu ya kisheria. Kwa hiyo utasikia hoja inaanza na "kwa vile ... "halafu litatolewa pendekezo la kuwafukuza Bungeni wale wanaoafiki waseme "ndiyo" (176 hivi watasema ndiyo) na wale wasiofiki waseme "hapana" karibu 46 watasema hapana. Waliosema ndiyo "wameshinda" nawabunge wa Chadema watatakiwa kuomba msamaha au kutoka kimoja Bungeni!

Hiyo ya Kuwafukuza Bungeni haitawavua ubunge wao, na cha zaidi Chuki kubwa ya Wananchi itakuja upande wa CCM, na Chadema wanaweza wakajiongezea umaarufu
Ni kweli Chadema wanaonekana kana kwamba wanagawanyika au wameganwanyika, hilo la kuongea na CCM halina maana kwa Chadema, waongee na CCM ili iweje? CCM ni Chama cha siasa kama NCCR ama CUF, point angekuwa waongee na serikali, lakini serikali gani ikiwa raisi hatambuliwi?
Kwa sababu Chadema ndio walioanzisha Move, basi wangekuja moja kwa moja kwa wananchi na kuwaelezea nini maana ya huo mchuno wao kwa JK, na wangesubiri impact ya watu, sasa hiyo nguvu ya watu ndio ingewafanya Chadema waitwe na serikali waje waongee, lakini ikiwa wewe ndio umeanzisha move na mwisho wa siku wewe tena ndio unaomba usuluhisi ina maana umeshindwa

Chadema inawapasa kuwa makini na njia pekee ya wao kukubalika tena ni kurudi kwa wananchi na kutengeneza suport kutokea huko, Nguvu ya wananchi ndio itaiamsha serikali
 
Nimesema hivyo ili nieleweke vizuri; kama Mwenyekiti na Katibu wake hawajui walitoka Bungeni kwa ajili gani huku Naibu na Kaimu nao wakiwa na upande wao nani awape umakini wa kuwasikiliza. Wakienda kwa wananchi watawaambia nini? Aidha waombe radhi kwa taifa kwa kuwafanya watu waamini walitoka kwa sababu walikuwa hawatambui jinsi Tume ilivyotangaza ushindi wa Rais na kutoka hapo ushindi wa Kikwete mwenyewe. Nadhani wanashindwa kujenga hoja yenye mantiki ambayo ni more balanced. Inashangaza wanashindwa kuarticulate a logical position na sasa wanachanganyana wenyewe.

Mzee MM nimekusoma vizuri sana na nakuelewa na kuungana na wewe. kweli wameonyesha udhaifu fulani. Lakini usife moyo na kuteleza sio kuanguka ndg yangu. Mimi napata wasiwasi sana na baadhi ya wana CDM tena wabunge vijana ambao walileta malumbano wakati wa uamuzi wa kutoka bungeni. HV NI KWELI HAWATUMIWI NA CHAMA CHA MAFISADI???? Maana hao ndio nadhani hasa wanachochea huo udhaifu. Wapo watu wanao tumiwa ndani ya CHADEMA kwa sasa. I DOUBT MUCH
 
Nimesema hivyo ili nieleweke vizuri; kama Mwenyekiti na Katibu wake hawajui walitoka Bungeni kwa ajili gani huku Naibu na Kaimu nao wakiwa na upande wao nani awape umakini wa kuwasikiliza. Wakienda kwa wananchi watawaambia nini? Aidha waombe radhi kwa taifa kwa kuwafanya watu waamini walitoka kwa sababu walikuwa hawatambui jinsi Tume ilivyotangaza ushindi wa Rais na kutoka hapo ushindi wa Kikwete mwenyewe. Nadhani wanashindwa kujenga hoja yenye mantiki ambayo ni more balanced. Inashangaza wanashindwa kuarticulate a logical position na sasa wanachanganyana wenyewe.

Hivi vyama, kama walivyo watoto, ni vizuri vikiwa vidogo..ni kama APPT Maendeleo sasaivi, huwezi kusikia wamevurugana. Nilishangazwa sana na kusikitika kusikia eti naibu katibu mkuu wa CHADEMA na wenzie waliamua kutoingia kabisa bungeni kwakuwa wao walipinga hoja hiyo lakini kura nyingi ziliikubali...uhuru wa kuamua haumaanishi kutokuunga mkono lililopitishwa na wengi kihalali. Si ni hawahawa wanasiasa ndo wanaotuimbia kila siku mambo ya demokrasia, sasa hili likisikika kuwa limefanywa na chama cha DEMOKRASIA na maendeleo, ndo tuelewe nini hapo. Mnavurugana kwenye mambo yasiyo na msingi wala maslahi kwa Taifa, at the expense of who?

Kutoka bungeni wakati raisi anahutubia kama ishara ya kuonyesha kutoridhishwa na jambo fulani sio issue kubwa, issue sasa ni kufanya kila liwezekanalo kuingia kwenye uchaguzi ujao na katiba mpya..na hilo linawezekana kwani hii nchi ni yetu sote. Sio ya waliotoka, waliogoma kuingia, wala waliobaki bungeni
 
Tusubiri February 2011 kukaa meza moja ni kupandishana vichwa au kuonyeshana nani anajua vifungu vya Katiba au Biblia, bora wale wabunge vijana na wasomi walishtukia mtego huo. Marekebisho ya Katiba ni lazima hata kama hayatajadiliwa Bungeni, muda ukuifika itabadilishwa tu si Msaafu, USA wamebadili mara ngapi? hata jirani zetu wamebadili, tusililete swala hili kimabavu watakaoumia ni kina nani? wenzetu wanatanua na Mashangingi wawe Chama tawala au wapinzani
 
Nafikiri MKJJ hujawaelewa Chadema hapa wanataka nini unaweza kuona kama weakness lakini is a planned mission.

Luteni,

I trully dig your strong faith and zealotry on Chadema. However the reality right now is that Chadema has Cheza Pata Potea and kama waliruka mkojo, wameanguka kwenye mavi yaliyokorogwa na mfinyanzi na yameanza kauka.

Wala msitudanganye ni plan, wame-dilute a bold plan with cheap and weak defense wakiogopa reaction. When we stated that they are not ready and they need to shape up their message, mlitulaani wengine na kutita wasaliti.

Leo hii wanachekwa mtu mzima hovyo!
 
Chadema wamejiweka wenyewe kwenye kona, of course hata kama mimi ni CCM siwezi kuzungumza nao kwa sababu right now they have chosen the point of weakness kutaka mazungumzo. Walipotoka Bungeni walikuwa upande wa nguvu, walipoparaganyika wakajiweka kwenye udhaifu na kama a tactical man nawaambia CCM wakatae kabisa kuzungumza na Chadema hadi Chadema waombe msamaha na kupiga magoti kuomba huruma ya wabunge wa CCM.

Ni kweli kabisa usemacho Mwanakijiji , mtu ukiisha poteza dira ujue hujui ufanyacho aisee, na hapo ndipo watu hukutumia watakavyo na kukuamrisha watakavyo. Ndivyo inavyotokea sasa kwa CDM
 
Hiyo ya Kuwafukuza Bungeni haitawavua ubunge wao, na cha zaidi Chuki kubwa ya Wananchi itakuja upande wa CCM, na Chadema wanaweza wakajiongezea umaarufu
Ni kweli Chadema wanaonekana kana kwamba wanagawanyika au wameganwanyika, hilo la kuongea na CCM halina maana kwa Chadema, waongee na CCM ili iweje? CCM ni Chama cha siasa kama NCCR ama CUF, point angekuwa waongee na serikali, lakini serikali gani ikiwa raisi hatambuliwi?
Kwa sababu Chadema ndio walioanzisha Move, basi wangekuja moja kwa moja kwa wananchi na kuwaelezea nini maana ya huo mchuno wao kwa JK, na wangesubiri impact ya watu, sasa hiyo nguvu ya watu ndio ingewafanya Chadema waitwe na serikali waje waongee, lakini ikiwa wewe ndio umeanzisha move na mwisho wa siku wewe tena ndio unaomba usuluhisi ina maana umeshindwa

Chadema inawapasa kuwa makini na njia pekee ya wao kukubalika tena ni kurudi kwa wananchi na kutengeneza suport kutokea huko, Nguvu ya wananchi ndio itaiamsha serikali

Kituko,

we have just finished the election, CCM wameshinda wana miaka mitano ya kurekebisha kila kitu na kuwafanya Chadema waonekane mafala hata kama leo wananchi wakichukia, they can not do anything until 2014 kwenye TAMISEMI and hopefully 2015 Uchaguzi Mkuu.

Do you trully think CCM watakuwa wamelaza gololi kuruhusu huu upuuzi wa ku-flipflop uwaangushe?
 
Nilipomsikia Mbowe juzi akisema wako tayari kukaa na CCM kuzungumza nikajua issue yote kwinshee!! Ingawa nimelipenda sana jibu la Makamba, lakini bado wana chadema wana nafasi (wakiamua kwa pamoja) ya kukaa na kujadili na kupanga mikakati ya kurudisha hoja majukwaani (kwa wananchi). Kwa kipindi kirefu sasa (takribani miaka 3) CCM wamepoteza mvuto kwa wananchi katika kujibu hoja za wapinzani kupitia majukwaa ya kisiasa.

Nawashauri chadema wasirogwe kuongea na CCM wala serikali yake, wala wasiwe kimya kama wanavyofanya sasa, wajipange na waandae hoja nzito za kwa nini wanaamini NEC sio huru na umuhimu wa kuwa na Katiba mpya. Kisha kabla ya kikao cha bunge kuanza mwezi Februari mwakani wawe tayari wamezunguka angalau mikoa 10 mikubwa kuelezea hoja zao kwa wananchi.

Hii itawapa boost sana na kuwalazimisha CCM waanze ku react, na kutokana na uzoefu tulionao CCM normally hawako strategic katika ku react na mara nyingi wamekuwa wakijichanganya hovyo hovyo. Hii itawapa Chadema nguvu na support kubwa kutoka kwa wananchi na pengine serikali kukubali kuanza mchakato wa kuandaa katiba mpya.

Vinginevyo Chadema wameula achuya na wanatulazimisha tuamini kwamba ushindi wa viti vingi vya wabunge walioupata katika uchaguzi uliopita ulikuwa ni wa kubahatisha na sio matokeo ya mipango madhubuti ya muda mrefu ya kushika dola.

Mvurugano huu utawarudisha nyuma si tu chadema bali vyama vyote vya siasa na kusababisha ile ndoto ya kuing'oa CCM kuwa kitu kisichowezekana kwani wananchi watapoteza uaminifu kwa vyama hivi.
 
Gaijin, katika position ya weakness waliyo nayo Chadema sasa watakachofanyiwa ni Hoja itatolewa na mbunge wa CCM kutaka Chadema waombe msamaha ama sivyo wafukuzwe Bungeni.. guess what will happen?

Kufukuzwa Bungeni hakupo. Saana wanaweza kupewa adhabu ya kutohudhuria idadi fulani ya vikao endapo ipo KANUNI ya BUNGE iliyovunjwa ambayo haipo. Labda itungwe haraka mwezi Feb 2011 na ifanye kazi kuanzia Nov 2010! Mnakumbuka Wabunge wa Upinzani mwaka 2000 walitoka nje ya Bunge kupinga kupitishwa Bajeti ya SERIKALI? Walifanywa nini?
 
haisemi hivyo lakini kanuni za Bunge zinaruhusu hoja kutolewa na ikipitishwa na kukubaliwa basi ina nguvu ya kisheria. Kwa hiyo utasikia hoja inaanza na "kwa vile ... "halafu litatolewa pendekezo la kuwafukuza Bungeni wale wanaoafiki waseme "ndiyo" (176 hivi watasema ndiyo) na wale wasiofiki waseme "hapana" karibu 46 watasema hapana. Waliosema ndiyo "wameshinda" nawabunge wa Chadema watatakiwa kuomba msamaha au kutoka kimoja Bungeni!

trust me mkuu hili hawataweza never ever, itabackfire, nasema wananchi ndio watawamaliza CCM, hapo ndio CHADEMA umaarufu utaongezeka na hakuna sheria au kanuni ya kuwafukuza wabunge kususia Hotuba ya rais, hoja binafsi haitawezekana why...? hata Makinda mwenyewe, Jaji mkuu ameshasema hawajavunja sheria, mbona uwoga unakujia mkuu, vp? i know u r a comrade vp? usirudi nyuma mkuu, twende kanyaga, kuwa na CCM ni maafa
 
ras kuty umenena, na mimi nadoubt kuna watu wanatumiwa na chama cha mafisadi. kama maazimio yamefikiwa na wengi naamini ni maazimio ya chama huwezi kuwa kwenye chama then unasema mimi sikuafiki so what and for what, ili wananchi wajue kuwa haukuwepo kwenye move hiyo, chadema jipangeni mti wenye matunda ndo unapigwa mawe, keep it up!!!!
 
Ndg zangu cdm hamkuweza kutumia nafasi iliyojitokeza mtajuta,mgeomba ushauri kwa Raila mjue cha kufanya(timing),ilitakiwa kumfanya kikwete aapishiwe ikulu chini ya ulinzi mkali na ikiwezekana ucku.sasa kura zimeibiwa mnashindwa kutumia nguvu ya umma HAMUWEZI,subiri ss cha moto mtakikuta bungeni
 
haisemi hivyo lakini kanuni za Bunge zinaruhusu hoja kutolewa na ikipitishwa na kukubaliwa basi ina nguvu ya kisheria. Kwa hiyo utasikia hoja inaanza na "kwa vile ... "halafu litatolewa pendekezo la kuwafukuza Bungeni wale wanaoafiki waseme "ndiyo" (176 hivi watasema ndiyo) na wale wasiofiki waseme "hapana" karibu 46 watasema hapana. Waliosema ndiyo "wameshinda" nawabunge wa Chadema watatakiwa kuomba msamaha au kutoka kimoja Bungeni!

MKJJ, CCM haiwezi kufanya hilo kosa la kuwafukuza wabunge wa CDM bungeni. Kufanya hivyo watawasaidia sana CDM kisiasa kwa vile issue ita bring international attention kitu amabacho CCM hawataki na hawataweza kuhandle!!! But if that is what you wish, well keep on wishing Bro!!!
 
huyo anayesema wafukuzwe bungeni weee ndo uliwachagua? aliyewachagua ndiye mwenye sauti ya kuwakataa ambao ni wananchi na kama mnataka kuigundua nguvu ya umma wafanye hv stupidy idiot
 
haisemi hivyo lakini kanuni za Bunge zinaruhusu hoja kutolewa na ikipitishwa na kukubaliwa basi ina nguvu ya kisheria. Kwa hiyo utasikia hoja inaanza na "kwa vile ... "halafu litatolewa pendekezo la kuwafukuza Bungeni wale wanaoafiki waseme "ndiyo" (176 hivi watasema ndiyo) na wale wasiofiki waseme "hapana" karibu 46 watasema hapana. Waliosema ndiyo "wameshinda" nawabunge wa Chadema watatakiwa kuomba msamaha au kutoka kimoja Bungeni!

Mkuu, hapa hujaliangalia hili suala kwa pande MBILI. CCM hawawezi KUTHUBUTU kufanya hivyo, maana watakuwa wamejimaliza KABISAA.

Hiyo ni nafasi yao kama ulivyo sema, kama ikiingizwa hoja na mwana CCM,lakini kumbuka kwa wale walio wengi (wananchi, bado wanayo mapenzi na CHADEMA, wengi wanaliona hili suala la kutoka kama ushupavu uliofanywa na Wabunge wao na UKUMBUKE mass kubwa watahudhulia POPOTE CHADEMA watakapofanya mkutano ili kutaka kujua KWA NINI WALIFANYA HIVYO hasa mikoani, UKWELI WANYO HOJA, )wataichukulia hilo kama MABAVU.

Na chadema kwa mtazamo wangu HAWATAWEZA KUOMBA MSAMAHA, nasema HAWATAWEZA (mtazamo), so watatoka. CCM, wanalijua hilo kuwa CHADEMA watalitumia hilo kama mtaji wa siasa, KUWA WAMEKUBALI KUACHA POSHO ZOOTE KWA AJILI YA KUTETEA MASLAHI YA WANANCHI, ajenda ya ufisadi itaambatana na hiyo KWENYE operation sangara +

Pili, (mtazamo wangu), CHADEMA , wanafanya haya kwa wao ndio kambi ya upinzani, INAYOTAMBULIKA KIKATIBA NA KANUNI katika bunge, JE BUNGE LINAWEZA KUFANYA KAZI BILA KAMBI YA UPIZANI KATIKA NCHI ILIYO NA MFUMO WA VYAMA VINGI, (ikiwa vipo vyama vya upinzani vilivyoshida majimbo?) nahisi HAIWEZEKANI.

Ingekuwa ni kumfukuza mbunge mmoja mmoja , sawa, LAKINI SIO KUFUKUZA KAMBI NZIMA.

Nawasilisha.
 
Chadema wamejiweka wenyewe kwenye kona, of course hata kama mimi ni CCM siwezi kuzungumza nao kwa sababu right now they have chosen the point of weakness kutaka mazungumzo. Walipotoka Bungeni walikuwa upande wa nguvu, walipoparaganyika wakajiweka kwenye udhaifu na kama a tactical man nawaambia CCM wakatae kabisa kuzungumza na Chadema hadi Chadema waombe msamaha na kupiga magoti kuomba huruma ya wabunge wa CCM.

Mwanakijiji mimi naona hoja yako kwa pande mbili.

1. True advise to CCM

2. Au mtego

But

All in all ni mada yenye mashiko ya kujadiliwa.

Kwanza kabisa, madai ya Chadema according to katibu mkuu (aliyekuwa mgombea kiti cha urais wa muungano Dr. Slaa ni kupinga mchakato mzima wa NEC uliomweka madarakani Dr. Jakaya Mrisho Kikwete.Huo ndio ulikuwa msingi wa hoja iliyowafanya wabunge wa Chadema kutoka nje ya Bunge kususia Hotuba ya Rais ya Ufunguzi wa Bunge.

Chadema na sisi sote twafahamu kuwa, kwa katiba hii tuliyonayo, tume ikishatangaza basi there is no recall.Matokeo cannot be challenged kwenye chombo chochote cha haki pamoja na kuwa ni uhaini.

Walichofanya Chadema ni jambo moja muhimu sana.Kutomtambua Kikwete kama Raisi aliyechaguliwa na Wana wa nchi wa JMT na wanamtambua kama raisi aliyewekwa madarakani na tume (by-defacto) na ujumbe huu umefikishwa kunakopaswa na ndicho kinachomfadhaisha Kikwete pamoja na CCM kuwa Raisi aliyeko madarakani si kwa ridhaa ya wananchi BALI ni kwa ridhaa ya tume.Huu ndio ulikuwa ujumbe very bold and was echoed kisawasawa.

Nini ambacho CCM wanataka?

CCM wanataka Chadema imtambue Kikwete kama raisi aliyechaguliwa na wananchi ili wapate legitimacy ndani na nje ya nchi.Hicho ndicho kinachokosekana na Chadema wamewanyima.

Ni nini Philosophy ya matendo ya wabunge wa Chadema?

Ni wazi...kiini cha matatizo haya yote ni KATIBA.For what it worth kama katiba yetu ingeruhusu a people centered democratic processes haya yote yasingetokea. Tunachokikosa ni ule msimamo thabiti kupita hisia zozote za kiitikadi wenye kutetea misingi ya demokrasia komavu na kujali sauti ya umma.

The demands here goes beyond what some pundits see as short term benefits such as vyeo na masurufu ambayo wabunge watayapata or whether to be thrown out of the parliament abusively( without justice) using popularity in the house improperly to serve the interest of the few.

I bet that DR. Slaa and Chadema are thinking beyond this limit and that is precisely what bothers CCM and other allies

Nini kimefanyika?

Ili kupata legitimacy ya kuanza mabadiliko ya KATIBA, lazima uombe yule mwenye madaraka (government) kujadili mustakabali wa matatizo haya yote bila kujali itikadi yeyote na kuweka maslahi ya Taifa mbele ili wakikataa CHADEMA watakuwa na cha kuwaambia wananchi.

Nini kinafanyika sasahivi?

Nionavyo mimi CHADEMA wanajibu maswali ambayo wataulizwa hapo baadaye.Pasipo shaka wamefikiria mbali kuliona hili to clear all doubts katika njia ya Ukombozi.CCM hilo hawalioni, na hawataliona, kwa sababu hawataki kuliona, na gharama yake itakuwa kubwa asilani.

Nini kitafanyika?

CHADEMA wataenda SUPREME COURT:KWA WANA WA NCHI WA JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA ambapo watapata VERDICT yente kubeba ushindi wa kishindo ambao utatekelezwa rasmi 2015 NA MAHAKAMA hiyo iliyo kubwa kuliko MAHAKAMA zote katika JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA

CCM hawaoni mbali.Pengine kosa ambalo watafanya ni kupitisha azimio la kuwaondoa wabunge wa CHADEMA BUNGENI.Kufanya hivyo utakuwa ni msumari wa mwisho katika JENEZA la CCM and we flip OVER a NEW CHAPTER.

Hilo azimio litawasha moto ambao hautazimika kamwe hadi 2015 na hapo ndio wamewapa CHADEMA fursa ya kujijenga zaidi wakati CCM wanajitetea kwa mashataka ambayo CHADEMA watayapeleka kwa supreme court ya WANA WA NCHI WA JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA.
 
Gaijin, katika position ya weakness waliyo nayo Chadema sasa watakachofanyiwa ni Hoja itatolewa na mbunge wa CCM kutaka Chadema waombe msamaha ama sivyo wafukuzwe Bungeni.. guess what will happen?
mimi nitafurahi sana ccm wakitoa hoja ya kuwafukuza chadema bungeni
maana yake wataipeleka chadema popularity through the roof
 
Back
Top Bottom