Makala ya Jenerali Ulimwengu: Magufuli na utawala wa madoido uliokosa mfumo

Mtu mwenye njaa ni dhaifu kutokana na njaa aliyonayo.Ndani ya udhaifu wake kuna nguvu kubwa ya kuogopwa na mwenye nguvu!.
 
Hata tukihoji kama hajatekeleza tutamfanya nini wakati tume ya uchaguzi anateua yeye? Jeshi la polisi ndio hilo wengi wana vyeti fake kwa hiyo chochote wanachoambiwa ni lazima watekeleze bila kuhoji, yaani nifae kwa jua nikufae kwa mvua.
Mjadala ulikua unahusu viwanda lakini naona umezungumzia mambo mengi sana kwa wakati mmoja.
 
Naam, mwenye macho na zone na mwenye masikio na asikie... Namkumbuka sana hayati mchungaji Christopher Mtikila...
Hahaha Mtikila angesheanda kufungua kesi mahakamani siku nyingi ,R.I.P Mzee Mtikila
 
Mjadala ulikua unahusu viwanda lakini naona umezungumzia mambo mengi sana kwa wakati mmoja.

Mjadala huu ulikuwa hauhusu viwanda bali ni utawala wa madoido, huku kwenye viwanda ni sehemu ya ufafanuzi kulingana na mjadala ulivyokuwa unaendelea. Kwa hiyo hayo mengi unayosema wewe ni sehemu tu ya ufafanuzi wa utawala huo wa madoido.
 
Unatoka nje ya mada na kuanza kuanzisha mada yako ndogo..ambayo ndio pana zaidi kuliko hii ya viwanda tuliyokua tunajadili mwanzo.
 
Unatoka nje ya mada na kuanza kuanzisha mada yako ndogo..ambayo ndio pana zaidi kuliko hii ya viwanda tuliyokua tunajadili mwanzo.

Mkuu huu ni mjadala huru hatufungwi na eneo moja, maana mleta mada tunayochangia hakuna mahali kataja viwanda, wewe ndio ulisema auze gazeti ajenge kiwanda. Sasa hapo kulikuwa na uhusiano gani na mada ya huyu muanzisha uzi kuhusu utawala wa madoido? Hili la viwanda ulilichomeka wewe kama kejeli, ila kama unataka tujadili viwanda anzisha uzi wako tuje huko na sio kuleta kejeli kwenye post za wengine.
 
Fredrick Sumaye alikiri JPM ni mtendaji mzuri, lakini akaonya, " huyu mtu anahitaji kuwa nyuma ya mtu, lazima awepo wa kumshika mkono". tahadhari hii ilimaanisha nini?
Kauli hii inaweza kuwa na maana mbili au tatu hivi: 1) hakufaa kuwa raisi bali angeweza kubakia na uwaziri hasa wa wizara ya ujenzi. 2) hakufaa kuwa raisi bali angeweza tu kuwa waziri mkuu. 3) anahitaji kusimamiwa au kuwekewa gavana.

Kwa bahati mbaya katiba aliyoapa kuilinda ndiyo anayotumia kuvunja baadhi ya sheria, eg, shera ya manunuzi ya umma, sheria ya vyama vya siasa ya 1992.
 
Chadema miaka yote mmekuwa mkiponda katiba ya nchi ni mbaya sana na haifai kabisa.!!!

Ghafla mwaka huu mmegeuka watetezi wakubwa Wa hiyo katiba kuwa ni nzuri sana na lazima ifuatwe.!!

Tuwaulize je kwa hiyo hamna haja ya katiba mpya??

Chadema acheni unafiki hautawafikisha popote.
 
Ulimwengu kaisha kabakiza hasira tu lazima akubali tu kwamba zama zao zimekwisha kabisa ni wakati wa kizazi kipya.
Dah, we ndo umeisha kweli kweli. Badala ya kujibu hoja unazungumzia mtu ambaye hata makala yake tajwa hujaisoma. Kweli kizazi kipya bado kinahitaji cha zamani. Yaani umechoka sana!
 
Mtaweweweseka sana lakini God is with this man na tutatoka bakini na mstumsini yenu mgando ya kushindws kwa serikali hii, haitashindwa hata kidogo.
 
Katika makala iliyosomwa DW Ulimwengu amemsifia Magufuli kwa kuifumua bandari, TRA, kutimua wafanyakazi hewa, kurudisha heshima ofisi za umma. Lakini akasema serikali yoyote ingeweza kufanya hayo kama si chama hicho kutekwa mafidi...

Kwa upande wa wale wanaomkosoa, amesema wanaona ni mtu anayendesha nchi kwa madoido badala ya mfumo. Anasema kuzuia bunge live, kuchukua maamzi ya papo kwa papo, kutokubali kushauriwa na kwa sehemu fulani kudaiwa kutofuata sheria kwenye maamzi yake ni mambo yanayoongeza upinzani dhidi yake. Anasema miezi sita ya pili itaonyesha kama atashinda upinzani unaozidi kukua dhidi yake
Ulimwengu ni kiungo mahiri wa wanafiki, miaka 10 yote ya JK alikuwa akiandika makala ndefu kuonyesha jinsi alivyoshindwa na kuwa ccm lzm iondolewe madarakani 2015.

Imefika 2015 na ccm kurudi madarakani kwa kishindo!!

Lkn Ulimwengu ameanza tena porojo zile zile zilizoshindwa 2015!( Doing the same thing again and again but expecting different results) !!!

Ulimwengu jipime ,kama ulishindwa kawa JK, kwa JPM utashindwa vibaya pamoja na wanafiki wenzio wanaokulipa
 
Mjadala huu ulikuwa hauhusu viwanda bali ni utawala wa madoido, huku kwenye viwanda ni sehemu ya ufafanuzi kulingana na mjadala ulivyokuwa unaendelea. Kwa hiyo hayo mengi unayosema wewe ni sehemu tu ya ufafanuzi wa utawala huo wa madoido.

Madoido + kukurupuka + uchochezi
 
Back
Top Bottom