Makada 201 CCM wahamia CHADEMA

Ba'mdgo

JF-Expert Member
Apr 17, 2012
230
46
MAKADA 201 wa Chama cha Mapinduzi (CCM), akiwemo Mwenyikiti wa Kitongoji cha Buhungu, Kata ya Kigongo, wilayani Chato, Mkoa wa Geita, wamejiunga na Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA).

Kujiunga CHADEMA kwa wana CCM hao kunatokana na mikutano ya vuguvugu la mabadiliko (M4C), inayofanywa na chama hicho cha upinzani katika************* maeneo mbalimbali likiwemo Jimbo la Chato, ambalo Waziri wa Ujenzi, John Magufuli ndiye mbunge wake.

Makada waliotimkia CHADEMA kwa nyakati tofauti ni kutoka Kijiji cha Muganza, Kasenga, Busaka na Igando, Kata ya Bwera ambapo walidai kuchoshwa na mwenendo wa siasa za CCM, hali ambayo imewasababisha waendelee kuwa na maisha magumu huku viongozi wao wakiendelea kuneemeka.

Mbali ya makada hao wengine waliojiunga na CHADEMA ni Katibu wa Umoja wa vijana wa CCM kata ya Muganza Paulo Malulu, Katibu wa Tawi la CCM Kijiji cha Mkombozi, Christopher Charles na Mwenyekiti wa kitongoji cha Buhungu Kata ya Kigongo, Razaro Busumabu.

Akizungumza muda mfupi baada ya kumalizika kwa mkutano huo, kwenye Kata ya Muganza, Katibu Mwenezi wa CHADEMA Wilaya ya Chato, Alex Mukama, alisema wananchi wa Jimbo la Chato wamekipokea chama hicho tofauti na awali waliogopa kujitokeza hadharani.

Kwa upande wake Katibu wa CHADEMA wa Wilaya ya Chato, Mange Ludomya, aliwataka wananchi kukipa kisogo CCM kwa kuwa kimeshindwa kuboresha maisha ya wananchi kwa miaka yote.


SOURCE:
TANZANI DAIMA
 
Safi ila wamechelewa sana, walipaswa kuwa wameyafanya hayo kabla ya Oct 31th 2010.
 
tunawakaribisha,ila tabia za kigamba waziache huko huko,cdm ni kupiga kazi bila posho.
 
Kwi kwi kwi kwiiiiiiiii.....jamaa wa kafu anaulizwa mafanikio ya v4c anasema wamevuna mlinzi wa Kamanda Lema A-town...Hongereni makamanda wetu hakuna kulala mpaka kieleweke!!!!!
 
Ahaah! kumbe vikada vidagaa mimi nilidhani ni makada mapapa.
 
Ahaah! kumbe vikada vidagaa mimi nilidhani ni makada mapapa.
Kweli we Mtata kama ID yako, kada kwako wewe mpaka awe Mukama, Nape au JK? Viongozi wa ngazi ya chini ndio makada muhimu sana kwa chama na ndio wapo karibu mno na wanachama/wananchi
 
KARIBUNI PEPONI , ILA HUKU CDM KUNAHITAJI KUJITOLEA ZAIDI PAMOJA NA KILA MMOJA KUFANYA KAZI, TUWE PAMOJA.:welcome::welcome::welcome:
 
MAKADA 201 wa Chama cha Mapinduzi (CCM), akiwemo Mwenyikiti wa Kitongoji cha Buhungu, Kata ya Kigongo, wilayani Chato, Mkoa wa Geita, wamejiunga na Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA).
Kujiunga CHADEMA kwa wana CCM hao kunatokana na mikutano ya vuguvugu la mabadiliko (M4C), inayofanywa na chama hicho cha upinzani katika************* maeneo mbalimbali likiwemo Jimbo la Chato, ambalo Waziri wa Ujenzi, John Magufuli ndiye mbunge wake.
Makada waliotimkia CHADEMA kwa nyakati tofauti ni kutoka Kijiji cha Muganza, Kasenga, Busaka na Igando, Kata ya Bwera ambapo walidai kuchoshwa na mwenendo wa siasa za CCM, hali ambayo imewasababisha waendelee kuwa na maisha magumu huku viongozi wao wakiendelea kuneemeka...
Safi sana.
 
Kule CCM kuwapitisha wale magwiji wa UFISADI nchini kwa maana ya MAPACHA WATATU kuwa ni sehemu na vinara wa uongozi wao tukielekea 2015 si tu kwamba itakua imedhihirishia Umma wa Tanzania ya kwamba GAMBA KWAO NI MWIKO KULIVUA 'HATA IWEJE', hapana;

isipokua, kubwa zaidi hapa ni kwamba sasa Wana-CCM kwa ujumla wao wamelitangazia taifa kuwa UFISADI ni sera rasmi ya chama chao na kwamba hata kutokee vugu vugu la mageuzi la kiwango gani nchini wao ni mbele kwa mbele kwa sana.

Kiama cha CCM ni kule kukumbatia kwa sana hii sera ya ajabu na kero kubwa kwa taifa letu. Kwa kifupi, CCM kaburi lake ni UFISADI uliotukuka na kutamalaki kila idara ya chama hicho na serikali yake na sasa kuzaa mbegu chipukizi kwenye NEC-CCM hii mpya.
 
Hivi ni nani atakizuia hiki kimbunga? Kuna vigogo nawaona tayari wanataka ku-jump from he CCM sinking ship!
 
m4c itavuna wa tz wengi tena kwenye majimbo ya viongozi maarufu. lakini cdm wanatakiwa kuwa makini ktkt kuwapokea watu wengine kwasababu wanahamia cdm baada ya kukosa uongozi ccm kwahiyo nia yao ni kutafuta maslahi yao binafsi na kutaka kufanya cdm kama daraja la kutokea kimaisha.
 
Back
Top Bottom