Majirani wanamcheka mpenzi wangu

lucz

JF-Expert Member
Dec 7, 2013
218
41
Poleni na mihangaiko wana JF.

Naomba ushauri nifanyeje hapa nilipopanga majirani zangu wanamcheka mpenzi wangu walikuwa ndani wakicheka huku housegirl akiwa mlangoni nikaona housegirl naye anacheka huku akijibu eeh kaja aliponiona mimi akafunga mlango.

Mimi nilihisi wanacheka jinsi anavyo vaa siku za kazi. Kuanzia nguo hadi viatu upande wa viatu anavaa malapa ni kama ya kuogea sio kuvaa kwenda mjini. Upande wa mashati mara yamepauka au kua na tobo kabisa.

Mimi ni mtumishi serikalini yeye anauza duka la ndugu yake na kukaa kwa ndugu yake anadai ni kaka yake. Mimi pia kwa upande wangu nilishamuonya juu ya huo uvaaji kwa sababu nipo njiani na watumishi wenzangu nikikutana nae napita kama simjui yaani nashindwa hata kumtambulisha kuwa huyu ni shemeji yenu.

Wakati tunaanza mahusiano nilimpenda sana kiasi kwamba nikachukua hela kidogo nikaenda kumnunulia shati na tishirt nikampa hakuyachukua mpaka nilipo mlazimisha na hajawahi kuvaa hata siku moja. Mimi nilichohisi huko anakokaa wanamkataza kuvaa nguo ambayo hajanunuliwa nikamuuliza kwa nini havai hakunipa sababu inayoeleweka.

Ila siku za jumapili huvaa nguo nzuri na viatu vizuri hupendeza sana hadi nafurahi. Kuna kipindi nikaamua awe anakuja jumapili tu. Kumpenda nampenda lakini nashindwa nifanyeje kuhusu hili.
 
Unataka Punda ama mlio?
 
Wala waskuvunje moyo hao wanamtamani sku ya sku mkikaa flesh wanakunyanganya wanafiki wakubwa hao wala usjali mwaya wakakupa mawazo bute
 
Just live your life.
You only live once. Why making life complicated.
 
Hii ndo shida kuanza mapenzi ukubwani...dude habari hii ni ya kueleza watu wazima kweli? Kisha unajiita mtumishi serikalini? Serikali hii hii? Kweli tunahitaji kufanya mabadiliko makubwa mwaka huu!
 
ila mungu nisaidie i love smart man hata kidogo cjui ntawezaga kumpenda mtu ambaye always shabby, haijalishi yuko kazini au out nooo,
 
Back
Top Bottom