Majipu yaliyotumbuliwa kwa mbwembwe yarudishwa kimya kimya?

FakeID

Member
Feb 29, 2016
89
96
Yule aliyesema kwamba serikali inaendesha mambo yake kwa mizuka kweli hajakosea.

Upo uthibitisho kwamba watu ambao wamekuwa wakisimamishwa ama kufukuzwa kazi na serikali kwa mbwembwe za kwenye vyombo vya habari wameanza kurudishwa kazini. Kundi hili linawakilishwa na mkurugenzi wa michezo ambaye kuanzia wiki iliyopita yuko kazini akiendelea na kazi zake kama kawaida japo Uma haujataarifiwa juu ya uamuzi huo.
 
Mkuu mbona umechelewa sana kujua,, ngoja nikupe watatu...

Mkurugenzi wa Manispaa ya Kigoma ujiji alitumbuliwa na kurudishwa kimya kimya

Aliyekuwa RAS wa Mwanza Dr Feisal alitumbuliwa kwa mbwembwe nyingi yuko pale Tamisemi amechili tu anakula mshahara

Pia yuko jamaa yake Simbachawene ambaye ni mkurugenzi wa Manispaa ya Ilemela anaitwa John Wanga alitumbuliwa na Naibu Waziri Jafo halafu akarudishwa kimya kimya na aliporudi akahamisha watumishi nane waliomchoma kwenda kwenye shule za kata. Hapa waliokuwa na uchungu na nchi yao kwa kuibua ufisadi ndio wameadhibiwa. Hapa majipu yanatumbuliwa kwa Double Standards, wanaotumbuliwa ni Team Membe na Team Lowassa. Timu nyingine wanapiga kama kawaida
 
unajua mtu anapoisiwa kuwa na makosa kutokana na sheria za jamhuri inaruhusiwa kusimamishwa kazi kwa ajili ya kupisha uchunguzi na akikutwa hana kosa anarudishwa kazini.Na akisimamishwa lazma watu wajue ili asije tapeli watu......nini tatizo?
 
Kama waliwasimamisha mbele ya vyombo vya habari huku wakijidai wamejiridhisha, sasa kwanini wanawazidi share kimya kimya
 
Yule aliyesema kwamba serikali inaendesha mambo yake kwa mizuka kweli hajakosea.

Upo uthibitisho kwamba watu ambao wamekuwa wakisimamishwa ama kufukuzwa kazi na serikali kwa mbwembwe za kwenye vyombo vya habari wameanza kurudishwa kazini. Kundi hili linawakilishwa na mkurugenzi wa michezo ambaye kuanzia wiki iliyopita yuko kazini akiendelea na kazi zake kama kawaida japo Uma haujataarifiwa juu ya uamuzi huo.
Ni kweli kuna baadhi wanarudishwa!, akiwemo yule aliyekuwa Katibu Tawala wa Mwanza, Dr. Faisal Issa!.

Rais Magufuli alisema wazi, katika kutumbua majibu, hakuna atakayeonewa!, na kusisitiza ikitokea kuna aliyeonewa, atarudishwa!.

Pasco
 
unajua wapo watendaji wanafnya maigizo. wao wanadhani kutumbua mtu ndio utendaji kwao hivyo wanatafuta mtu wanaita vyombo vya habari na kutumbua ili waonekane wamefanya kazi na wanaendana na kasi ya kiongozi wao.

sasa inapobainika wao walifanya makosa kwa nini wasitumbuliwe wao maana kuna watu wamelalamika kuwa wafanyakazi wanatishwa na hilo linawezekana pale anapowekwa mtu juu yao ambaye hajui kazi wanazozifanya yeye anatumbua tu.

ni bora utolewe mwongozo kuwa iwapo mtu atatumbua mtumishi kwa uzembe wake yeye mtumbuaji basi ajiandae kutumbuliwa yeye.

Yule aliyesema kwamba serikali inaendesha mambo yake kwa mizuka kweli hajakosea.

Upo uthibitisho kwamba watu ambao wamekuwa wakisimamishwa ama kufukuzwa kazi na serikali kwa mbwembwe za kwenye vyombo vya habari wameanza kurudishwa kazini. Kundi hili linawakilishwa na mkurugenzi wa michezo ambaye kuanzia wiki iliyopita yuko kazini akiendelea na kazi zake kama kawaida japo Uma haujataarifiwa juu ya uamuzi huo.
 
So and so amesimamishwa kupisha uchunguzi... Uchunguzi ukionyesha hana kosa lolote anarudi kupiga mzigo. Ndio utawala bora ulivyo na ndio anachofanya Magufuli hamuonei mtu.
 
Yule aliyesema kwamba serikali inaendesha mambo yake kwa mizuka kweli hajakosea.

Upo uthibitisho kwamba watu ambao wamekuwa wakisimamishwa ama kufukuzwa kazi na serikali kwa mbwembwe za kwenye vyombo vya habari wameanza kurudishwa kazini. Kundi hili linawakilishwa na mkurugenzi wa michezo ambaye kuanzia wiki iliyopita yuko kazini akiendelea na kazi zake kama kawaida japo Uma haujataarifiwa juu ya uamuzi huo.
Yule Mkurugenzi wa Manispaa ya Dodoma nae nasikia yupo wizarani mzigo kama kawa
 
Ni bora kuchukua hatua Na kufanya maamuzi kuliko kutofanya maamuzi. Kinachoendelea ni kuwasimamisha watendaji wanaoshutumiwa Na ubadhirifu wa Mali Au madaraka serikalini ilikupisha uchunguzi. Nadhani nijambo Jema nasi lakubezwa.
 
1460802437707.jpg

Nadhani wanajaribu kuvunja record hiyo
 
Back
Top Bottom