Walipewa nafasi ya kujichagua waka shindwa na yeye akiwa kiongozi ulitegemea nini?Pole sana Urassa najua lazima utampinga huyu mama hata kama ana hoja za msingi ni vizuri unge declear interest zako (kabila) halafu ungemshambulia mama musori. Mimi binafsi sikupenda chama kumteua Mwanaume kuwateulia wanawake wawakilishi wa viti maalum mie kwangu hilo halijakaa sawa otherwise kama ndio katiba ya chama ipo hivyo na tuiheshimu.
MOSHI unaoendelea kufuka ndani ya Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) unaonekana kuficha moto.
Baada ya uchaguzi mkuu mwaka huu, hali ndani ya chama hicho inaonekana kutokuwa shwari hasa kutokana na mgawanyiko wa wazi unaojitokeza sasa.
Chachu zaidi ilijitokeza hivi karibuni baada ya Katibu Mkuu wa Chama hicho ambaye pia alikuwa mgombea urais, Dk. Willibrod Slaa, kukataa kutambua matokeo yaliyompa ushindi Rais Jakaya Kikwete, aliyekuwa akigombea kwa tiketi ya CCM.
Hali hiyo ndiyo iliyofanya baadhi ya wabunge wa chama hicho kususia pia hotuba ya Rais Kikwete, alipokuwa akizindua Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Novemba 18, Dodoma.
Tukio hilo lilitanguliwa na la kutohudhuria sherehe za kuapishwa kwa Waziri Mkuu, Mizengo Pinda, kulikofuatiwa usiku na hafla ya kupongeza wabunge, ambapo baadhi ya wabunge wa chama hicho walihudhuria.
Hatua hiyo ilisababisha mgawanyiko wa wazi, kwa baadhi ya wabunge kutoshiriki ususiaji huo na kutoa sababu zao walizoona ni za msingi.
Lakini, kana kwamba hiyo haitoshi, juzi Mwenyekiti wa Chama hicho wa Mkoa wa Mbeya, Sambwee Shitambala akatangaza kujiuzulu wadhifa huo ili kupisha uchunguzi wa tuhuma zilizoelekezwa kwake.
Shitambala aliwambia waandishi wa habari kuwa uongozi wa chama hicho kitaifa unamtuhumu kuhongwa Sh milioni 600 ili ahujumu chama chake na kushindwa kutwaa jimbo la Mbeya Vijijini.
Wakati hayo yanaendelea, huku uongozi wa juu ukikataa kuyazungumzia kuchelea majibizano, jana Mwenyekiti wa Baraza la Wanawake Chadema (Bawacha), Leticia Musori, alitangaza kukihama chama hicho na kujiunga rasmi na NCCR-Mageuzi. Kiini cha hatua hiyo ni uteuzi wa wabunge wa viti maalumu katika chama hicho.
Musori aliwambia waandishi wa habari jana kuwa hakushirikishwa katika uamuzi wa kuteua wabunge hao na kudai kuwa waliteuliwa kwa kufuata uhusiano na vigogo wa chama hicho.
Akizungumza wakati anakabidhiwa rasmi kadi ya NCCR-Mageuzi na Mwenyekiti wa Chama hicho, James Mbatia, Musori alisema uamuzi wake unatokana na wanawake kukosa haki na mfumo dume kuendekezwa ndani ya chama hicho kwa kutoshirikisha wanawake katika vikao vya uamuzi.
Alisema kitendo cha chama hicho kuendeleza uozo na udikteta katika kufanya uamuzi, huku pia kikiendeshwa kama kampuni ya wakubwa katika kufikia uamuzi mbalimbali.
Musori alisema uchaguzi halali wa Bawacha ulivurugwa na viongozi wa juu wa chama hicho, ili kutoa nafasi kutoa viti maalumu kwa wanaowataka badala ya kuachia vikao vya wanawake wa chama hicho kuamua kama zinavyoelekeza kanuni za Bawacha.
Musori alisema jambo lingine ni kutokubali utumwa wa Mwenyekiti Mbowe ambaye alidai hataki kupingwa katika uamuzi wake.
"Mimi nilikuwa nikipingana na Mbowe katika hoja mbalimbali ikiwa ni pamoja na kupinga utaratibu wa Chadema ambao Mwenyekiti anakuwa mtia saini ilhali yeye ndiye Mwenyekiti wa vikao vya Kamati Kuu, Baraza Kuu na Mkutano Mkuu, ambavyo kimsingi ndio vyenye mamlaka ya kusimamia Sekretarieti ya chama," alisema.
Aliongeza kwamba katika uchaguzi wa Bawacha, yeye alishika nafasi ya tano kwa kura zaidi ya 60 za wanawake wa chama hicho huku Suzan Lyimo akipata kura sita, Grace Kiwelo mbili na Halima Mdee saba, lakini hakuteuliwa katika uchaguzi wao wa wabunge 25 jambo ambalo si la kidemokrasia.
Alisema kutokana na uamuzi huo wa vigogo wa Chadema kuwanyima haki wanawake waliochaguliwa na wenzao, wengi watahama chama hicho ambacho alidai kipo kwa ajili ya maslahi ya wachache na hakina demokrasia.
Aliendelea kudai kwamba akiwa na cheo hicho cha Mjumbe wa Kamati Kuu ya Chadema, Mjumbe wa Baraza Kuu la Chadema na Mweka Hazina wa Umoja wa Madiwani wa Chadema na kukidhi vigezo vilivyowekwa na viongozi hao, bado hakuteuliwa kuwa mbunge wa viti maalumu kutokana na kumpinga Mbowe.
Alisema amechukua uamuzi wa kuhamia NCCR - Mageuzi ili aendeleze mageuzi baada ya kufanya utafiti na kuona kuwa chama hicho ndicho kinamfaa na kusisitiza kuwa tatizo si kupata uongozi kwani alikuwa na vyeo vingi ndani ya Chadema.
Akimpokea mwanachama huyo na kumkabidhi kadi, Mbatia alitoa rai kwa wanasiasa kuzingatia haki kwa kila mmoja, kwani bila kutoa haki Taifa haliwezi kwenda vizuri, na alitaka haki ianzie kwenye familia hadi Taifa.
Septemba mwaka jana, kutokana na kilichoonekana ni mchezo mbaya ndani ya Chadema katika kutafuta uongozi wa Baraza la Vijana (Bavicha), kulitokea kutoelewana kambi, moja ikiwa ya Mwenyekiti Freeman Mbowe na nyingine ya Naibu Katibu Mkuu, Zitto Kabwe.
Mvutano huo ulisababisha uchaguzi kufutwa na Baraza la Wazee na hivyo aliyekuwa akiwania nafasi ya uenyekiti, David Kafulila wa kambi ya Zitto, kuhama chama na kujiunga na NCCR-Mageuzi na sasa ni Mbunge wa Kigoma Kusini kupitia chama hicho.
Mkuu hii habari iko hapa tangu juzi, next time check kama kuna stori inayofanana na ile unayotaka kupost kabla hujaposti ya kwako kuturahisishia na sisi wachangiaji na wasomaji.
Aliongeza kwamba katika uchaguzi wa Bawacha, yeye alishika nafasi ya tano kwa kura zaidi ya 60 za wanawake wa chama hicho huku Suzan Lyimo akipata kura sita, Grace Kiwelo mbili na Halima Mdee saba, lakini hakuteuliwa katika uchaguzi wao wa wabunge 25 jambo ambalo si la kidemokrasia.
Dr Kitila Mkumbo kama sikosei wewe ulikuwa ni consultant katika kutafuta nani aingie kwenye ubunge wa viti maalumu wa Chadema. Kwa kuzingatia vigezo ulivyoweka na points walizopata wale wote walioomba nafasi ya ubunge wa viti maalum kupitia chadema, je waweza tueleza hayo aliyoyasema huyo mama yana ukweli kiasi gani????
mkuu, sidhani kama chadema inaongozwa na kuwa moerated na JF... and i am worried kama ulichouliza ndio utaratibu wa kupata details...
ninachoona ni kuishi kama tulivyozoea wengi, kubwabwaja, kutokufuata utaratibu wa kujua jambo na kudandia terni kwa mbele. if one reads what you have written, atabaki na maswali yafuatayo
- hivi huyu wa wapi hajui taratibu za kupata taarifa za kuitendaji hasa chamani?
- katumwa na huyo mama?
- au ndiye huyo mama?
- vipi kamuandikia kitila kwenye public forum wakati tuna pm options?
Ushauri wangu, unaweza kuwa na swali la msingi, lakini jaribu kufuata njia za msingi... otherwise swali lako la msingi linaweza kuwa kama kauli za vijiwe vya kahawa na konyagi
thanks
acid
Dr Kitila Mkumbo kama sikosei wewe ulikuwa ni consultant katika kutafuta nani aingie kwenye ubunge wa viti maalumu wa Chadema. Kwa kuzingatia vigezo ulivyoweka na points walizopata wale wote walioomba nafasi ya ubunge wa viti maalum kupitia chadema, je waweza tueleza nani alipata nini??? Maana huyo mama analalamika kuwa kwa vigezo vya points vilivyowekwa alipata points 60 na alishika nafasi ya tano akiwa juu ya watu kama Lucy Owenya, na Halima Mdee. Je hayo aliyoyasema huyo mama yana ukweli kiasi gani???? Isijekuwa ana msingi mzuri wa kulalamika na hasa ukizingatia nafasi aliyokuwa nayo ndani ya Chadema
Naema hivi.............kama hujipendi, hebu thubutu kutangaza nia ya kugombea uenyekiti wa CHADEMA, weeeeeeeee!!!!!!!!!!!!!! kamuulize Zitto kama hukuipata fresh. Chama kina wenyewe babu weeeee....... wengine wapiga debe tu.
Naema hivi.............kama hujipendi, hebu thubutu kutangaza nia ya kugombea uenyekiti wa CHADEMA, weeeeeeeee!!!!!!!!!!!!!! kamuulize Zitto kama hukuipata fresh. Chama kina wenyewe babu weeeee....... wengine wapiga debe tu.
Kila siku CHADEMA CHADEMA CHADEMA HII IKOJE,MAANA YAKE NINI?HAYA NI MAELEZO MAFUPI;
- Ni chama mbadala wa ccm
- Ni chama kilichokuwa na wabunge wengi zaidi wa upinzani katikati bunge la JMT
- Ni chama kilichoshika kasi ya aina yake kwa ukuaji wa Democrasia Tanzania
- Ni chama chenye msimamo kisichoyumba mpaka sasa
- Ni chama kinachoongozwa kwa mujibu wa katiba na sheria za Nchi
- Ni chama chenye itikadi ya kisiasa
- Ni chama kilichoenea sehemu zote Tanzania pamoja na mapungufu ya bajeti yake
- Ni chama pekee kilichodiriki kuyakataa matokeo ya urais waziwazi bila kuficha
- Ni chama kilichodhihirisha ulimwengu kuwa rais aliyeingia madarakani kaingia kwa wizi wa kura kwa kutoka nje ya bunge wakati alipotaka kuanza kuhutubia bunge.
- Ni chama kitakachosimamia uundaji wa katiba mpya mpaka sasa.
- Ni chama kilichoonesha UPINZANI wa kweli ndani na nje ya bunge.