Sokomoko
JF-Expert Member
- Mar 29, 2008
- 1,915
- 127
Sokomoko, Huyu mama Naomi Kaihula, yuko kwenye siasa tangu muda mrefu, ni mwanaharakati wa siku nyingi, wewe umemjulia CBE, sisi ametufundisha Tambaza, enzi hizo akiwa kasichana fulani.
Hoja yako ya msingi ambayo nakubaliana nayo, kama Chadema, ingepata kiti kimoja tuu cha ubunge wea upendeleo, then mtu stahiki kukikalia, alitakiwa awe ni Mwenyekiti wa BAWACHA, no one else!, sasa imepata vitu lukuki na bado hayupo, then kuna jambo.
Hakuna ubishi kuwa Chadema, kimeshaonyesha njia, kimesimama kuhesabiwa na hesabu zimeshaanza kuleta bajibu ya vema, na zinategemea kubalance mwaka 2015. Kwenye mada yangu kule nyuma, nilisema, Chadema, hawajajipanga, ili hesabu zibalance vizuri, nilisema nina matumaini watautumia muda huu kujijenga na kujipanga ili hesabu zao zibalance vizuri 2015.
Ili mtu fulani yoyote kupata sifa za kuchaguliwa kuiwakilisha Chadema kwenye ubunge wa viti maalum, lazima kuna sifa na vigezo valivyotumia, wengine walishakuweko huko miaka 5 iliyotangulia, walifanya nini mle mjengoni kustahili kuendelea?. Uchaguzi wa wabunge hao, umeendelea kukybikwa la ile ile dhana inayoitafuna Chadema, huku viongozi wa Chadema wakiendelea kuikanusha, Chadema can't survive in denial!, ni kama kansa, inakula ndani kwa ndani!.
Kwa maoni yangu binafsi mimi kama Pasco wa JF ambaye sio mwanachama wa chama chochote cha siasa bali ni mshabiki wa demokrasia ya kweli ndani ya bunge, Chadema, hawakumtendea haki Mwenyekiti wao wa Bawacha kunyima Ubunge mteremko, lakini pia huyo Mwenyekiti, ameonyesha udhaifu mkubwa kuihama Chadema ambayo sasa ni more promising na more prospective opposition na kujiunga na chama kinacho chechemea!.
Mimi nimekutana na huyu mama mwaka 2003 nilipaanza diploma yangu pale CBE na mpaka namaliza Advance yangu mwaka 2008 nimemuacha ni kweli huyu mama ni mwanaharakati wa TNGP na ninafahamiana vizuri sana na kwakwe huwa namtembelea ni kama mama yangu sina ubaya nae wowote wala chuki na huyu musori simjui na wala hanijui ila kama mpenda haki sijaridhika na chama kuchagua "mwanaume awachague wanawake wakawawakilishe wanawake"