Ambassador
JF-Expert Member
- Jun 2, 2008
- 933
- 75
Jana tulikuwa na boss mzungu mahala tunakula stori mara akaanza kutuuliza maana ya majina ya maeneo mfano Mwananyamala, wasahikaji wakawahi mtoto nyamaza na kumtafsiria kwa kingereza. Alipouliza Kijitonyama mmoja akasema kijito is a stream and nyama is meat. Tulibaki hoi kwa vicheko.
Nasikia baadhi ya majina ya maeneo yanatokana na historia ya mahali hapo au tukio muhimu lililotokea wakati mengine yanahusishwa na watu maarufu walioishi mahali hapo, wakati majina mengine hayana maana.
Hebu tuchangie majina ya miji/maeneo tunayoyafahamu na maana yake, tukianza na hilo la Kijitonyama.