Lycaon pictus
JF-Expert Member
- Jan 31, 2021
- 7,238
- 12,751
Nimeona mdau mmoja analalamika kero ya jirani yake anayefuga ng'ombe. Kwa nini serikali za miji hazikatazi kufuga maeneo ya mjini, badala yake wanakataza kulima mahindi na alizeti, vitu visivyo na madhara yoyote kwa mji? Huwa tunawaza kinyume nyume sana. Binadamu alianza kusumbuliwa sana na magonjwa baada ya kuanza kufuga, magonjwa yetu mengi yanatoka kwa wanyama. Mfano mzuri ni mafua ambayo kiasili ni magonjwa ya ndege. Kufuga wanyama kwenye maeneo ya makazi ni kero kubwa, ukiacha magonjwa bado kuna kero ya harufu na uchafuzi mwingine wa mazingira.
Mtu akitaka kufuga akanunue eneo nje ya mji/jiji. Si sawa wala ustaarabu kufuga kwenye makazi ya watu.
Mtu akitaka kufuga akanunue eneo nje ya mji/jiji. Si sawa wala ustaarabu kufuga kwenye makazi ya watu.