Majimbo yenye wabunge wa chadema

brother, listi yenu inazidi kupungua kwani huko kagera kuna mgombea wenu mmoja wa chadema kajitoa sasa sijui nini kapewa any way watu kama hawa ndio wanataka kupewa ridhaa ya kuongoza ni hatari sana kwani yaliyowakuta wa zambia mwaka 1991 bado hawajayasahau baada ya kumtupa kenneth kaunda na kumpa madaraka mlokole chiluba! Matokeo yake kila mtu anayajuwa! Mlokole aliifilisi nchi na sasa kesi yake bado inaendelea!
Chadema wacheni kuhadaa wananchi uwezo uwezo na nia ya kuongoza hamna labda sababu na hiyo haitoshi kama hamna uwezo na nia ya dhati!

Tukuite mnajimu au mpiga madogoli. Siku zote hakuna umasikini mbaya kama umasikini wa mawazo. Kama ni mmoja wao ama umedhurika na fikra fifi nakupa pole sana. CCM siku zote wamekuwa wakitumia mifano ya nchi zilizoshindwa kuonesha ubaya wa vyama mbadala. Mbona zilizofanikiwa hamtumii kuonyesha uzuri wa mabadiliko (Kwa kukusaidia Kenya).
Na isitoshe katika darasa la mambumbumbu yupo anaekuwa wakwanza, pengine mafanikio mnayojivunia wewe na serikali yako ya CCM ni kama ya yule mbumbumbuanayeshika nafasi ya kwanza darasani. Kukuthibitishia madai yangu kamwe CCM haijivunii mafanikio ya kimaendeleo kulinganisha na nchi nyingine. Ndio maana mpaka leo Tanzania ni kati ya nchi masikini sana duniani, wakati ni kati ya nchi zenye utajiri sana duniani.
Mtaji wa ujinga unatumiwa sana na CCM. Mpaka siku utakapogundua unafanywa mjinga ndipo utakapo kata shauri la kujikomboa toka katika utumwa wa kiakili.
 
Mfamaji unajidanya mwenyewe..Hivi huijui Serikali iliyopo madarakani. Si nyingine bali ni ya CCM NI KWA ARI MPAYA NGUVU MPRA N KASI MPYA imeweza kutekeleza mipango ya maendeleo Tanzania yote ikiwemo walipokuwa Wabunge wa Chadema. Hivyo siyo kwa sababu wao wapo ndiyo mipango ya maendeleo imetekelzwa bali ni kwa upendo Kwa wanachi iliyonayo chama cha CCM , Ndiyo maana majimbo hata yaliyoongozwa na Chadema maendeleo yapo. Unajidangaya mwenyewe Kaka!! CCM ndiyo chamA bora mpeni kura za ndiyo DK. Jakaya Kikwete kwani anastahili sifa!!!!!
 
Huyu hana la kusema,watu kama hao wapo kila chama,mbona CCM wengine wamekimbilia upinzani.Hiyo ipo hasa kwa wale wenye ubinafsi,akaona ajiunge nao moja kwa moja.
 
tukuite mnajimu au mpiga madogoli. Siku zote hakuna umasikini mbaya kama umasikini wa mawazo. Kama ni mmoja wao ama umedhurika na fikra fifi nakupa pole sana. Ccm siku zote wamekuwa wakitumia mifano ya nchi zilizoshindwa kuonesha ubaya wa vyama mbadala. Mbona zilizofanikiwa hamtumii kuonyesha uzuri wa mabadiliko (kwa kukusaidia kenya).
Na isitoshe katika darasa la mambumbumbu yupo anaekuwa wakwanza, pengine mafanikio mnayojivunia wewe na serikali yako ya ccm ni kama ya yule mbumbumbuanayeshika nafasi ya kwanza darasani. Kukuthibitishia madai yangu kamwe ccm haijivunii mafanikio ya kimaendeleo kulinganisha na nchi nyingine. Ndio maana mpaka leo tanzania ni kati ya nchi masikini sana duniani, wakati ni kati ya nchi zenye utajiri sana duniani.
Mtaji wa ujinga unatumiwa sana na ccm. Mpaka siku utakapogundua unafanywa mjinga ndipo utakapo kata shauri la kujikomboa toka katika utumwa wa kiakili.

wewe ndio unataka kuwa mpumbavu kwa kudanganywa na chadema kuwa watakuletea maendeleo! Huu ndio ujinga maendeleo gani hayo ambayo chadema watakuja nayo? Hakuna chama chochotecha upinzani barani afrika kilichowaletea raia wake maendeleo! Unatoa mfano wa kenya, huu ni uongo wa dhahiri nani kakuambia kenya wanaafadhali sasa baada ya moi kuondoka? Hivi wewe umefika kenya tangu wapinzani waingie madarakani?

Kenya ile ya enzi za kenyata huwezi kulinganisha hata kidogo na hawa viongozi walioko madarakani! Kenya ya sasa ina masikini wengi wa kutupwa kuliko kenya ileeee ninayoijiwa mimi!, leo kenya barabara zote ni mashimo tupu na maji machafu yanayonuka kinyesi yametapakaa kila mahali utatapika! Watu hawana kazi na ujambazi ndio usiseme! Waliowengi hawana uwezo wa kununua dawa hospitalini na wodi zimejaa wagonjwa mpaka mdomoni! Haya ndio maendeleo unayosema! Enzi za kenyata na moi mambo hayakuwa hivyo! Ilikuwa ukiingia kenya hasa jiji la nairobi utafikiri uko jiji la london au new york! Nidhamu ilikuwa inaonekana kila mahali ni taa za barabarani leo kenya imekuwa giza huwezi kutoka nje baada ya saa moja usiku! Sasa hayo ndio maendeleo eee!

Na hawa viongozi walioko madarakani kazi yao ni kushindana nani ndio bosi kuliko mwenzake ni kibaki au ni raila!
Sasa wewe unataka kutuletea kama hayo hapa kwetu tz! Ati chadema wanafaa kuongoza! Uwozo mtupu! Katu hatuwezi kufanya ujinga waliofanya waafrika wengine kwa kuiga demokrasia za kijinga wanazolazimishwa na mabwana zao wa ulaya na amerika ati afrika tunahitaji demokrasia never ever for ever!!! Watanzania tumeshtuka hatudanganyiki!!!

Kura kwa ccm zimwi likujualo halikuli likakwisha!
 
Back
Top Bottom