Majibu ya Zitto juu ya shutma za kuhujumu CHADEMA

yani mkuu umeongea kitu cha maana sana.sijui tufanye nini ili wazo hili liwafikie mods. Tokea ID ya tuntemeke iliposimama kupost hapa pametokea ID's zaidi ya 10 zikianzisha mada mfu!kuna mmoja anaitwa taswira hakulala almost 30 hrs akimtetea zitto .sijui anawapa hela kiasi gani.

Wewe utakuwa sio mpenzi wala mwanachama wa CDM. Sera ya CDM ni democracy and freedom of speech as long as humtukani mtu wala huhatarishi usalama. Sasa hata kama mtu anatengeneza IDs 100, MODS watazifunga kama atasema matusi au kasha. Na kwa taarifa ni kwamba kuna live feed ambayo Mods wanaweza kutumia kugundua mpaka namba ya nyuma uliyopo wakati una post. Zitto mwenyewe pengine anakucheka tu unavyosema anatoa hela! Au kuna mtu anawapa pesa kumchafua?
 
Mh Zitto alishajibu shutuma za kina saa8 na wenzake siku nyingi sana kama ifuatavyo:

1) Vipi madai kuwa unatumwa na CCM ili kupunguza nguvu ya CHADEMA? Kama si kweli unadhani kwanini watu wanakuona kama pandikizi ndani ya CHADEMA?

‘Baadhi ya watu wanapandikiza chuki hizi kwa sababu zao wenyewe. Hawanisumbui maana najua ni kikundi kidogo cha watu wachache wenye malengo yao ovu. Wajue tu kwamba hawawezi kuwadanganya Watanzania ambao wanafanya maamuzi yao sio tokana na propaganda ila kutokana na matendo ya kila mmoja.

Onyo: Watu hao hawawezi kummaliza Zitto kisiasa bila kuiathiri CHADEMA maana the imaage of Zitto is so intimately intertwined with CHADEMA that you couldn’t attack Zitto without jeopardizing the image of Chadema, and vice versa.
Wanaoeneza sumu hii hawana nia njema wala mapenzi na CHADEMA. Hawaelewi siasa. Wanafurahisha maadui wa CHADEMA. Maadui wanawachochea kwa kuwapa habari za uwongo na wao wanadhani watammaliza Zitto. Huwezi kummaliza Zitto bila kuiathiri CHADEMA. Hawatafanikiwa.’

2) Ni kweli kuwa una mkakati wa kuhamia CCM kabla ya 2015?
‘Sijawahi wala kufikiria kuhamia CCM. Kama nilivyosema hapo awali, sijawahi kuwa mwanachama wa chama kingine chochote tofauti na CHADEMA. Namwomba mungu kuwa niondoke duniani nikiwa chama hiki hiki. Siamini katika kuhama vyama. Ninaamini katika mfumo imara wa vyama vingi nchini. Ninaamini katika demokrasia pana.’

3) Vipi tetesi kuwa wewe na Kafulila mmeanzisha chama na una mkakati wa kutimkia huko?

‘Swali hili na lililotangulia yanaonyesha kuwa hizi kweli ni tetesi tu. Sasa kama unasema nina mkakati wa kuhamia CCM. Tena kuna tetesi nimeanzisha chama na nataka kuhamia huko, sasa mimi nina vyama vingapi nitakavyohamia?

Sijawahi hata kufikiria kuanzisha chama cha siasa. Chama changu ni CHADEMA na sitaondoka CHADEMA.
Kinachonisikitisha ni kwamba kuna viongozi wa CHADEMA wamekula sumu hii na bila woga wanaisema kana kwamba ni kweli.

It is very unfortunate Kiongozi wa chama makini kama CHADEMA kuamini ujinga na kuingia kwenye mitego kama hii.
Nataka ijulikane wazi kabisa kwamba, CCM haitachoka kutugawa. Haitachoka kupandikiza chuki miongoni mwetu. Wameshajua udhaifu upo wapi na wahenga walisema kamba hukatikia?’

Source: JF, 22 Nov 2012

Inaonekana wazi maadui wa Zitto wamekata tamaa na sasa wanaamua kumprovoke ili asuse na ahame CDM. Zitto, move on mungu atosha kuwa shahidi baina yao na wewe na siku zote penye ukweli uongo hujitenga.

Acha kuoanisha mada hapa, tunataka haje hapa alikatae kundi la Masalia, kwa sababu Masalia wamesema,wanamsapoti Zitto na Zitto ndiye alikuwa akifinance masalia ili kudhoofisha Chama,pamoja katibu mkuu wa Chama. SASA tunamtaka ZITTO Aje Hapa AWAKANE MASALIA. Sio kuunganisha unganisha Mada.

1.Swali Masalia Anawajua au hawajui?
2. Lengo kubwa la masalia yalikuwa ni nini?
3. Je ni kweli wewe ulikuwa unawadhamini Masalia?
4. Je Juliana,Mwampamba, Nchenga, Unawatambuaje?
5. Je kuna kundi linitwa kundi la zitto, Na Dhumuni kuu la hili kundi ni nini?
6.Tudhibitishie kwamba Maneno aliyo ongea Saanane si ya kweli?

Akishijibu hayo maswali, Tunaweza tukajua,tuweke wapi Msaliti au sio Msaliti
Tunampenda Zitto That why Tunataka aturudishie Imani kwake,kwa sababu kwa sasa hatuna Imani Tena Naye.
 
sidhani kama atakujibu.kwani zitto alipomjibu mamuya kilikuwa kikao halali cha chama?

ndipo hapo nilipokuwa nataka tuanzie kujenga hoja yetu,kama wao walivyotumia media kuchafua uongozi wa chadema,basi na sa8 anayo haki kabisa kutumia hizo hizo media kusafisha uongozi wa chadema
 
kumsafisha zito na ukweli wa ben ni sawa na kuosha kanzu njeupe na mkaa

Mkuu huu msemo wako unanikumbusha TAMBWE HIZZA alisema: 'Nikihama CUF nikazini na mama yangu' kwani yuko wapi saa hizi? .... CCM. Nenda ukamuulize alitimiza hicho kiapo?. Therefore, huo ni msemo wa kuishiwa hoja na kukata tamaa.
 
...hapa wanachadema lazima tukubali katika umoja wetu kuwa kuna mahali tulikuwa tuki "abuse the hospitality of democracy" katika chama..wapuuzi wanaojifedhehesha kisiasa ktk jf leo hii, kimsingi hawakuridhishwa na walikatishwa tamaa na matukio yaliyotokea wakati wa uchaguzi wa bavita.. hata zitto pia, sparking point ya kutiliwa shaka kwake ni uchaguzi uliopita wa mwenyekiti wa taifa wa cdm, na pia nia yake aliyoiweka wazi, ya kutaka ugombea uraisi (kupitia chadema)..bado najiuliza, wakati "mzee wa ujira mwia" anapitishwa kugombea ubunge wa maswa, hakukuwa na mwana cdm ambaye,alibaniwa ili tu, kumpatia "shibby" nafasi ambayo wala sihitaji kusema namna,ilivyompa kibri cha kupingana na chama ktk namna ambayo ni kama "ameshindikana"...chama chetu sio tu ni chama cha maendeleo, lkn pia, na kubwa kabisa ni chama cha demokrasia...na iendelee kuwa hivyo kimakwelikweli...tusiogope wala kuhofia demokrasia....lkn pia, kuna ukweli ambao lazima ueleweke kama ulivyo na ukubalike...chadema, leo hii iko juu zaidi ya imani zote, ukabila, ukanda,ujinsia na mengine yote ya aina hiyo...na tuchukue hatua stahiki kuadhibu wanaostahili adhabu ktk kadhia hii...kisha tusonge mbele tukiikumbatia kwa dhati kabisa demokrasia ndani ya chama...."aluta continua...mpaka ushindi kamili upatikane"
 
Hiki ndicho ninachokiamini pia. Huwezi kumshambulia kiongozi yeyote wa CHADEMA bila kuiathiri CHADEMA. Sasa ni kwanini yeye Zitto aliwaacha rafiki zake akina Mchange, Tuntemeke na kundi lake wafanye kazi ya kumchafua Dr. Slaa, huku akitambua kuwa kumshambulia kiongozi kama yeye na mwingine yeyote kuna athari kwa chama? Au hili lina madhara akishambuliwa yeye Zitto peke yake? Au anataka kusema bila Zitto CHADEMA haiwezi kusimama?

Mkuu unamjua Zitto vizuri??!
Tafuta post yake ya 2009 wakati akisema hagombei ubunge na ile anayosema kuhusu uchaguzi wa BAVICHA, mgombea aliyekuwa anamtaka yeye na matusi na tuhuma zake za ukanda na udini na speciffically kwa Dr Slaa.

Ukishasoma hiyo, then angalia kampeni za hawo vijana wake wasio na akili kwa viongozi wa CHADEMA na mwenyekiti wa BAVICHA.
Then urudi hapa, utatueleza kama umeelewa somo au lah!!

Kila la heri.
 
Acha kuoanisha mada hapa, tunataka haje hapa alikatae kundi la Masalia, kwa sababu Masalia wamesema,wanamsapoti Zitto na Zitto ndiye alikuwa akifinance masalia ili kudhoofisha Chama,pamoja katibu mkuu wa Chama. SASA tunamtaka ZITTO Aje Hapa AWAKANE MASALIA. Sio kuunganisha unganisha Mada.

1.Swali Masalia Anawajua au hawajui?
2. Lengo kubwa la masalia yalikuwa ni nini?
3. Je ni kweli wewe ulikuwa unawadhamini Masalia?
4. Je Juliana,Mwampamba, Nchenga, Unawatambuaje?
5. Je kuna kundi linitwa kundi la zitto, Na Dhumuni kuu la hili kundi ni nini?
6.Tudhibitishie kwamba Maneno aliyo ongea Saanane si ya kweli?

Akishijibu hayo maswali, Tunaweza tukajua,tuweke wapi Msaliti au sio Msaliti
Tunampenda Zitto That why Tunataka aturudishie Imani kwake,kwa sababu kwa sasa hatuna Imani Tena Naye.

sidhani kama ana huo udhubuti wa kuja hapa jukwaani kuwakana kwasababu wao wamedhibitisha kabisa kuwa zitto wanafahamiana nae kwa ukaribu,rejea utetezi wa mchange,alipokuwa anasema "walipokuwa wanasafiri pamoja na zitto pande za morogoro wakagundua kuwa nati za tairi za nyuma zimelegezwa"wengi tunampenda sana zitto lakin aje kwanza ayajibu hayo maswali.period
 
mkuu mkiwa vitani halafu adui akawa anawashambulia kwa nguvu na mkagundua kuwa kati yenu kuna anayeshirikiana na adui yenu, hatua ya kwanza ni kumuua huyo adui ndani yenu then mnapanga plan mpya ya mapambano.
Zitto, masalia and pm7 inabidi wauawe ndo ukombozi wa pili wa mtanganyika uendelee.

nimekupata; sasa ni bora tujenge hoja za kuitisha mkutano mkuu wa chadema ili tuwatimue haraka iwezekanavyo; au tuwaonye ili tuendelee kusonga mbele badala ya kurumbana kila kukicha - mwisho adui yetu ccm atatukuta hapa hapa.

Mnajua ccm wameishajua kuwa jukwaa hili lina siri nyingi za chadema - hivyo wanawatuma makids wao kama nape kuja kufuatilia ni kipi tunapanga.

Bora tufike hatua hapa tuwe tunaanika ubovu wa viongozi wa ccm tu basi, ubovu wa viongozi wa chadema iwe siri yetu na tushughulike nao ndani ya vikao halali vya chama.

Yangu ndo hayo!
 
sidhani kama ana huo udhubuti wa kuja hapa jukwaani kuwakana kwasababu wao wamedhibitisha kabisa kuwa zitto wanafahamiana nae kwa ukaribu

Hata Zitto akija yatakuwa malumbano tu. Nilitegeme mumsifu kwamba amekuwa na ushujaa wa kuvumilia. Masalia, mabaki zote hizi ni propaganda chafu dhidi ya Zitto. Majibu yake ndio hayo kwamba yeye ni CDM na hatahama CDM. Cha kufanya ni kuthibitisha, to date, ni kosa lipi ambalo ameshawahi kufanya la kuvuruga chama. Saa8 alikuwa anazungumzia 'thought iliyokufa'. Hamna hoja ya msingi hapo.
 
Tunaomba ndugu ZZK aje hapa mwenyewe kutoa neno , kama alikuwa anapata muda wa kuja kuchukua sifa za kijinga kama zile za Rais wa Mtwara , anashindwa nini kuja kusafisha hali ya hewa hapa kama kweli anaonewa ?
Freshthinking , hakuna anayebisha uwezo wa kufikiri wa ZZK ila ndo hivyo sasa ,tamaa na uchu wa madaraka unamuharibia future yake , hapa kajikwaa tu ila akiendelea na fikra hizi mgando, ATANDONDOKA KABISA KISIASA
 
Huyu mtu anaitwa ZZk ananikera kwa kauli zake za tambo zisizokuwa na hata chembe za busara,majigambo tu,nani kakwambia wewe ndio nguzo ya CDM ,jitahid uwe unakaa na watu wazima uwe unachota busara kama akina mnyika sio kuwa bize na walimbwende...............utajavuna aibu wewe...........
 
Tunaomba ndugu ZZK aje hapa mwenyewe kutoa neno
Freshthinking , hakuna anayebisha uwezo wa kufikiri wa ZZK ila ndo hivyo sasa ,tamaa na uchu wa madaraka unamuharibia future yake , hapa kajikwaa tu ila akiendelea na fikra hizi mgando, ATANDONDOKA KABISA KISIASA

Zitto ana majukumu mengi kuliko maadui zake. Yuko masomoni na pia ana mambo mazito ya kusimamia kabla ya kikao cha bunge kijacho. Au umeshasahau hoja za mabilioni ya Uswiss? It needs a lot of time and thinking kaka.
 
Zitto anapotoshwa na Kafulila, kale kajamaa sijui kanamzidia wapi, ukikaona huwezi kudhaania ndie driving force ya Zitto.

mkuu umenivunja mbavu,eti kale kajamaa.ni kweli kajamaa kamachachari sana.kamekaa kiuchonganishi sana.
 
Hata Zitto akija yatakuwa malumbano tu. Nilitegeme mumsifu kwamba amekuwa na ushujaa wa kuvumilia. Masalia, mabaki zote hizi ni propaganda chafu dhidi ya Zitto. Majibu yake ndio hayo kwamba yeye ni CDM na hatahama CDM. Cha kufanya ni kuthibitisha, to date, ni kosa lipi ambalo ameshawahi kufanya la kuvuruga chama. Saa8 alikuwa anazungumzia 'thought iliyokufa'. Hamna hoja ya msingi hapo.
Uvumilivu gani unaousemea wakati alikuja hapa siku ya thread ya kwanza akaishia kumkana Ben na kutishia hadi uhai wa Panya bana , ni nini kinachomfanya sasa hivi atulie kama amemwagiwa maji baridi ?
 
wakati mwingine naamini busara ni kukaa kimya,lakini kwa hili kunahitajika ufafanuzi wa ziada,kwa smartness ya zitto sidhani kama alikua hajui harakati za marafiki zake wa karibu.
 
Uvumilivu gani unaousemea wakati alikuja hapa siku ya thread ya kwanza akaishia kumkana Ben na kutishia hadi uhai wa Panya bana , ni nini kinachomfanya sasa hivi atulie kama amemwagiwa maji baridi ?

CCM nawashangaa sana, yaani mmeshupalia ZZK aje mwenyewe atoe neno, ili muendeleze mpasuko ndani ya CDM? Zitto keep silent, be focused with more serioes issues kuhusu taifa letu. Watanyamaza tu, title za thread zitaisha! Kila watakazotowa zitaunganishwa na zilizopita hadi wakate tamaa. Its Freshthinking!
 
Back
Top Bottom